Mwandosya na Slaa waahidi kusimamia watoto wa Marehemu Mwangosi

Mkurabitambo

JF-Expert Member
Feb 3, 2010
230
57
MAZISHI ya Mwandishi wa Habari, Daud Mwangosi yalifanyika jana katika Kijiji cha Busoka kilichoko wilayani Rungwe, Mbeya na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.

Katika mazishi hayo, viongozi hao wawili kila mmoja alitangaza kuwasomesha watoto wa marehemu Mwangosi ambaye alifariki dunia
Septemba 2, mwaka huu baada ya kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu wakati polisi walipokuwa wakisambaratisha
mkutano wa Chadema.

Akitoa salamu zake katika mazishi hayo, Profesa Mwandosya alisema yupo tayari kumsomesha mtoto wa kwanza kati ya wanne
wa Mwangosi, Nehemia ambaye anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Malangali. Alisema atamsomesha mtoto huyo kidato cha tano na sita na ikiwa atafaulu na kukosa mkopo wa elimu ya juu, atamsomesha mpaka atakapomaliza elimu yake ya juu.

Dk Slaa kwa upande wake, alisema amewasiliana na rafiki yake ambaye yupo tayari kuwasomesha watoto wawili wa Mwangosi ambao wote wapo shule ya msingi. Mtoto wa mwisho wa marehemu hajaanza masomo. Pamoja na kuwasomesha watoto hao, alisema Chadema kimetoa Sh2 milioni za rambirambi kutokana na msiba huo.

Vijembe msibani Awali, Profesa Mwandosya na Dk Slaa walitoa kauli zinazoonyesha kupigana vijembe vya kisiasa, baada ya waziri huyo kumtaka Dk Slaa aache kufanya kampeni za kuingia Ikulu mwaka 2015 msibani. Kauli hiyo ya Profesa Mwandosya ilikuja
baada ya Dk Slaa kutaka polisi waliohusika na mauaji hayo wachukuliwe hatua za kisheria kwa sababu wanajulikana.

"Tunashangaa wamekamatwa watu wengine na kuwaacha waliohusika na mauaji hayo, tunawajua kwa sababu wameonekana hadharani, hakuna siri kwa hilo," alisema Dk Slaa. Akizungumza baada ya kauli hiyo ya Dk Slaa, Profesa Mwandosya aliwataka wanasiasa wa vyama vya upinzani kuacha kutumia misiba kutafuta kura za urais mwaka 2015.

"Natoa pole sana kwa familia na tasnia nzima ya habari nchini. Hiki ni kipindi kigumu, lakini tuviachie vyombo husika vifanye uchunguzi wa mauaji haya," alisema Profesa Mwandosya na kuongeza:

"Lakini nichukue fursa hii kuwaomba wanasiasa waache kutumia misiba ili kujipatia umaarufu katika kutafuta kura za urais mwaka 2015." Katika mahubiri yake msibani hapo, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Busoka, Mathayo Mwanjemele alikemea mauaji hayo na kuwaomba wahusika wajitokeze hadharani kabla Mungu hajawaumbua.

"Waliohusika na mauaji haya wajitokeze na kutubu kwa wananchi kabla adhabu ya Mungu haijawakuta," alisema. Alisema ufike wakati
Serikali iwe inakiri uzembe unaofanywa na watendaji wake ambao umekuwa ukitokea mara kadhaa.

IGP Mwema asimamia uchunguzi Kabla ya mazishi hayo, mwili wa Mwangosi ulifanyiwa uchunguzi na wataalamu wa afya kutoka Dar es Salaam, huku IGP Said Mwema akishuhudia. Baada ya kumalizika uchunguzi huo, usiku mwili wa marehemu ulisafirishwa kuelekea
Mbeya kwa mazishi. Mwili huo ulipofika Tukuyu, umati mkubwa ulijipanga barabarani na kupunga mkono, huku wengine wakiusindikiza kwa baiskeli na pikipiki hadi kijijini, Busoka.

Majeruhi wengine Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mafinga, Dk Peter Mwenda alisema mbali na marehemu
Mwangosi, watu wengine 10 walijeruhiwa, wawili kati yao walitibiwa na kuruhusiwa. Alisema waliobaki hospitalini hapo hali zao
zinaendelea vizuri.

Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Hussein Kweha (27), Edson Iddy (22), Alfred Kibitanyi (27), Hamad Musa (37), Yeremia Kulwa (45) na
Christopher Pesa (30). Alisema majeruhi hao walidai kwamba walikuwa katika mkutano wa ndani wa Chadema na askari waliwataka kutulia kabla ya kuwashambulia kwa marungu na vitu vyenye ncha kali.
 
Dah! Mungu awabariki na awazidishie ktk hilo la kusaidia hawa watoto wa kamanda DM

Habari ya Mwandosya na Dr Slaa kuwasomesha watoto wa marehemu Mwangosi limenifariji sana hasa nikikumbuka ile picha ambayo Dr Slaa alionekana akikumbatiana na mtoto wa Marehemu ambayo ilinitoa machozi.
 
Yatima hawa wasingetokea kama si Dr Slaa kulazimisha maandamano,nafsi inamsuta kusomesha mtoto moja sioni faida yake achukue na mke kabisa.
 
Yatima hawa wasingetokea kama si Dr Slaa kulazimisha maandamano,nafsi inamsuta kusomesha mtoto moja sioni faida yake achukue na mke kabisa.

Kwani aliyeuawa alikuwa anaaandamana, msigeuze mada, aliyekufa kwa kipigo cha polisi ni mwandishi na ameshughulikiwa na polisi zaidi ya sita hii si bahati mbaya.ipo siku mtatoa majibu sahihi
 
Hizi ni kama Hadithi tu hata Sie wengine tulipofiwa tuliambiwa hivyo hivyo na Ndugu zetu ila akili ni kumkichwa kwa Mtoto... maana Yatima Hadeki wanaweza wakatelekezwa anytime... hapa mimi ningeomba wawasaidie kupata wanasheria wazuri ili waidai Serikali Fidia kwa kifo kilichosababishwa na wao Serikali kupitia Jeshi la Polisi tena ni kifo cha kukusudia kabisa mimi kwa Upande wangu hawa watoto wanatakiwa kusomeshwa na Serikali Shule yeyote watakaopenda watoto au walezi wao Pia Fidia isiyozidi Billion 2 matibabu yao yawe juu ya Serikali hadi wafikishapo umri wa Kujitegemea... Sio Slaa au Mwandosya au Mtu yeyete Kulea Mtu Baki huwa ni Ngumu Watoto Wasaidie Kuidai Serikali Fidia Kubwa tu Huo Ndio Msaada....
 
Kwani aliyeuawa alikuwa anaaandamana, msigeuze mada, aliyekufa kwa kipigo cha polisi ni mwandishi na ameshughulikiwa na polisi zaidi ya sita hii si bahati mbaya.ipo siku mtatoa majibu sahihi

Angalia chanzo,M4C inalaana ndani yake hata kama ni mkakati wa kuchukua dola si kwa njia hii.Inasikitika kuona CDM hakuna wanachama bali kuna wafuasi na kila atakachonena kiongozi wao wafuasi wanafuata hata kama kina madhara.
 
Hoja za kufikirika hizo kaka, huna haki ya kuzungumzia idadi ya wanachama wa cdm kama hujaja na takwimu hapa.
 
Hizi ni kama Hadithi tu hata Sie wengine tulipofiwa tuliambiwa hivyo hivyo na Ndugu zetu ila akili ni kumkichwa kwa Mtoto... maana Yatima Hadeki wanaweza wakatelekezwa anytime... hapa mimi ningeomba wawasaidie kupata wanasheria wazuri ili waidai Serikali Fidia kwa kifo kilichosababishwa na wao Serikali kupitia Jeshi la Polisi tena ni kifo cha kukusudia kabisa mimi kwa Upande wangu hawa watoto wanatakiwa kusomeshwa na Serikali Shule yeyote watakaopenda watoto au walezi wao Pia Fidia isiyozidi Billion 2 matibabu yao yawe juu ya Serikali hadi wafikishapo umri wa Kujitegemea... Sio Slaa au Mwandosya au Mtu yeyete Kulea Mtu Baki huwa ni Ngumu Watoto Wasaidie Kuidai Serikali Fidia Kubwa tu Huo Ndio Msaada....

Mkuu umeongea jambo la msingi sana ila haya yangetekelezeka kama tungekuwa na serikali ila jiulize tunayoserikali makini?
 
Mkuu umeongea jambo la msingi sana ila haya yangetekelezeka kama tungekuwa na serikali ila jiulize tunayoserikali makini?

Serikali Makini Hatuna ila Tukishtaki na haki ipo wazi fidia Zipo wazi kabisa Serikali itatia akili...
 
Yatima hawa wasingetokea kama si Dr Slaa kulazimisha maandamano,nafsi inamsuta kusomesha mtoto moja sioni faida yake achukue na mke kabisa.

Kwanini mnapenda kuhalalisha makosa kwa hisia zenu za chuki binafsi?
 
Mimi nafikiri wanasiasa na waTz kijumla mlitakiwa waende mbali zaidi kwa watu kujitokeza kuisaidia familia hiyo. Kwani wanasiasa wote hao wanasaidia kusomesha vipi kuhusu maisha ya vijana hao ikiwemo pamoja na mjane?
 
Yatima hawa wasingetokea kama si Dr Slaa kulazimisha maandamano,nafsi inamsuta kusomesha mtoto moja sioni faida yake achukue na mke kabisa.
ID yako inamaana ya rap moja ya Twanga pepeta kwa hiyo we akili zako zimekaa kimuziki muziki tu ndo maana unaongea vitu vya kijinga kiasi hicho.
 
Ni jambo la hekima kwa wanasiasa hawa wawili kujitolea kuwasomesha hawa watoto wa marehemu Mwangosi swali ninalojiuliza ni kwamba leo hii hawa wanasiasa wapo ndio wanaweza kutekeleza hizo ahadi zao ,je mara watakapokuwa hawapo kwasababu zozote zile hilo jukumu la kuwasomesha hawa watoto litabebwa na nani?

Ndio maana naungana na wazo la kumtafuta mwanasheria ambae atafungua kesi dhidi ya serikali kuhusu mauaji ya marehemu Mwangosi na kudai fidia ambayo ikilipwa itatumika kuwasomesha watoto wa marehemu!!
 
Vipi kuhusu mjane atapata wapi kujikimu kama alikua anamtegemea mumewe, kilema cha maisha kwake.
 
Yatima hawa wasingetokea kama si Dr Slaa kulazimisha maandamano,nafsi inamsuta kusomesha mtoto moja sioni faida yake achukue na mke kabisa.
Acha kukurupuka unajua maana ya YATIMA? Aliyefiwa na mzazi mmoja hawezi kuitwa yatima.
 
Yatima hawa wasingetokea kama si Dr Slaa kulazimisha maandamano,nafsi inamsuta kusomesha mtoto moja sioni faida yake achukue na mke kabisa.
sio kosa lako tatizo ni uwezo wako mdogo wa kufikiri ambao unatokana na kuungua mtindio wa ubongo ulipokuwa mtoto
 
Acha kukurupuka unajua maana ya YATIMA? Aliyefiwa na mzazi mmoja hawezi kuitwa yatima.
Asante kwa kutambua hilo,kwa hiyo mnampango gani na mjane? tafadhalini msije mkavalisha kabooooom!
 
Back
Top Bottom