Mwandosya alimfanya Nini Kibaya Jk ,Hatokisahau[source:hotuba ya JK -UWT] | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandosya alimfanya Nini Kibaya Jk ,Hatokisahau[source:hotuba ya JK -UWT]

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Phillemon Mikael, Oct 23, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ' .....itakuwa ni aibu sana na ajabu pia utakuwa hujatenda haki kwa kumbagua ambaye hakukuchagua natolea mfano wangu katika uchaguzi uliopita,Prof Mark Mwandosya HAKUSHINDA LAKINI KWENYE SERIKALI YANGU NILIMUWEKA LICHA YA KUWA NILIFANYIWA MAMBO YA AJABU SANA AMBAYO NI VIGUMU KUYAVUMILIA LAKINI KAMA MWANASIASA LAZIMA UWE MKOMAVU....." Jakaya Kikwete ,DODOMA,22nd october 2012.

  NOTE :- JK Tunayemjuwa na visasi kweli atakuwa alifanyiwa jambo baya ...hadi "alie" na mwandosya amsamehe hivi hivi kweli.......kwenye nchi nyingine angetakiwa kutoa maelezo aeleweke ...ili kama jambo alilofanya mwandosya lilikuwa baya watu wapime..
  ISIJE IKAFIKIA MAHALI WATU WAKAMUHISI VIBAYA NA MASAHIBU YANAYOMKUTA MWANDOSYA..

  - INTERGRITY YA MWANDOSYA IPO MAJARIBUNI KUWA MIAKA YOTE HII KIKWETE ANAMPA KAZI SIO KWA AJILI YA UWEZO WAKE WA KIUTENDAJI BALI KWA KUHOFIA MANENO YA WATU .....WANAOJUWA UGOMVI WAO...AU ULE MSEMO WA KUMUWEKA ADUI KARIBU UMMALIZE AU UMLAINISHE.....MWANDOSYA AFIKIRIE MARA MBILI...NDIO MAANA AMEPEWA KAZI JAPO NI MGONJWA???

  NINAPATA MASHAKA MAKUBWA SANA NA UWEZO WA RAIS KIKWETE WA KU REASON HADI KUFIKIA KUTAMKA HAYA MANENO HADHARANI....BILA KUFIKIRIA MADHARA YAKE KWAKE KISIASA NA MAHUSIANO...AU NDIO KUTUBU?
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,474
  Likes Received: 5,858
  Trophy Points: 280
  It goes back many years ago......at the then the Ministry of Water and Energy where they were a minister and a principal secretary....
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimeona kwenye Tanzania daima, mpaka sasa najiuliza Prof. Mark alimfanya nini baba mwanaaisha sipati jibu... may be kupitia uzi huu wataweka wazi...

  Kumbe kumteuwa mtu ni Ukomavu wa kisiasa?
   
 4. Mkuu rombo

  Mkuu rombo JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  asante mkuu kwa maelezo yako ngoja 2ngoje waje wadau
   
 5. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2012
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Kama kiongozi anapaswa kuweka wazi alichofanyiwa kibaya na waziri wake,vinginevyo Mwandosya ajiuzulu kwa hiari yake na aseme ukweli nini KIBAYA alimfanyia Rais au akanushe ili record yake iwe safi
   
 6. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2012
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  Mh! Kama bosi analia hivyo hadharani, yawezekana kuna kiza kinene nyuma ya pazia.
   
 7. B

  Ba'mdgo JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kama kwel alitamka hayo basi ndio maana ni alimteua kuwa waziri asiyekuwa na wizara maalumu
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  MoD mbona umeihamisha huu uzi muhimu ...ambao ni siasa ...TUNAOMBA UURUDISHE KWENYE SIASA WATU WAUJADILI BRO...MKUU SANA!! HESHIMA MBELE!!....TUNATAKA WANAOJUWA UGOMVI WA MWANDOSYA NA JK ...TUUJADILI...

  SIO JAMBO DOGO HILI MKUU...HADI RAIS NA AMIRI JESHI MKUU "ANALIA"..!!
   
 9. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Siasa kweli kazi kwa mambo haya lakini ukweli mwandosya ni mwema sana kuliko baba Riz one mzee wa kulipiza visasi
   
 11. baba juniho

  baba juniho Member

  #11
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 22, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Tanzania ni nchi changa tena sana ila chakusikitisha naona kila kukicha tunakuwa na viongozi wasio na upeo hakika tunahitaji mageuzi alisi tusichague chama tumpime mtu ana uwezo kiasi gani
   
 12. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Wametoka mbali Mark na JK...
   
 13. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,526
  Likes Received: 5,673
  Trophy Points: 280
  Mods hii ni siasa bana! rudisha kule!
   
 14. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tujikumbushe ya 2008...

  HASIRA za wanamtandao waliojeruhiwa na sakata la Richmond sasa zimeelekezwa mkoani Mbeya kuhakikisha viongozi wawili maarufu mkoani humo, Profesa Mark Mwandosya na Dk. Harrison Mwakyembe wanamalizwa kisiasa, Raia Mwema imeambiwa.
  Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili lilizipata mjini Mbeya, hivi karibuni, hasira dhidi ya Mwandosya na Mwakyembe ambao wote ni wajumbe wa NEC ya CCM, zimejengeka baada ya Edward Lowassa kulazimika kujiuzulu uwaziri mkuu kutokana na taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kumhusisha na kashfa ya Richmond. Kamati hiyo iliongozwa na Dk. Mwakyembe.
  Aidha, ushindi wa Profesa Mwandosya katika kinyang'anyiro cha kuwania ujumbe wa NEC (Mbeya) dhidi ya Tom Mwang'onda, mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Cornel Apson, umeacha majeraha mabichi CCM mkoani Mbeya.
  Taarifa za uhakika ndani ya chama hicho mkoani Mbeya zinasema kwamba maandalizi ya tuhuma nzito dhidi ya wanasiasa hao wawili ambao pia wana mahusiano ya karibu, yamekwisha kukamilika na kwamba kilichobakia ni kuwaandikia barua za kuwaita kujitetea katika kikao cha Chama kinachotarajiwa kuitishwa hivi karibuni.
  "Maandalizi ya mkakati huu yalianza siku nyingi wakati wa uhai wa Katibu wa CCM mkoani Mbeya, Silvester Kikungwe (marehemu) na sasa inadaiwa kuwa yamekamilishwa na Mwenyekiti mpya wa CCM wa mkoa, Nawab Mulla," alisema ofisa mmoja wa CCM mkoani humo ambaye kwa sababu za wazi hakutaka jina lake litajwe.
  Ofisa huyo alitoa mfano wa kikao cha Wazee wa Mkoa kilichoitishwa na Mulla kwa lengo la kutoa tamko la kuwatuhumu Mwandosya na Mwakyembe kuwa wanadhoofisha chama, lakini ikashindikana baada ya viongozi wa dini waliohudhuria kikao hicho kupinga utoaji wa tamko hilo bila kwanza wahusika kuitwa kujitetea. Profesa Mwandosya na Dk. Mwakyembe hawakuitwa katika kikao hicho kilichofanyika Februari mwaka huu mjini Mbeya.
  Raia Mwema ilipomtafuta Mulla kueleza kwa undani suala hilo, iliambiwa kuwa alikuwa Dubai, lakini Katibu wake msaidizi, Zongo Lobe Zongo, alithibitisha kwamba kutakuwa na kikao cha CCM Mkoa wa Mbeya hivi karibuni, ingawa alisema hajui ajenda zake.
  "Kwa sasa Mwenyekiti yuko Dubai, lakini ninajua kuwa kutakuwa na kikao siku za karibuni. Ajenda sizijui, kwa sababu sekretarieti ndiyo inayopanga…Wao ndio wanaweza kujua na inawezekana wao wamejadili wakati Mwenyekiti hayupo," alisema Zongo.
  Hata hivyo, alipodokezwa kuhusu kuwajadili wanachama, ambao CCM Mkoa wa Mbeya inadai wanakigawa chama, Zongo alidai kwamba Mwenyekiti wake hawezi kuruhusu ajenda kama hiyo kujadiliwa kwenye kikao.
  Lakini Raia Mwema imethibitishiwa na vyanzo vingine vya habari kwamba kesi inayotungwa dhidi ya Profesa Mwandosya, Mbunge wa Rungwe Mashariki na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, ni ya tuhuma kwamba ameanza mapema maandalizi ya kugombea urais mwaka 2010 kinyume cha taratibu za Chama, na kwamba akipita mitaani mkoani Mbeya baadhi ya watu humwita "Rais" , "Rais". Tuhuma hizo pia zilipata kuandikwa na gazeti moja la wiki lililo karibu na wanamtandao hao.
  Kuhusu Dk. Mwakyembe, taarifa zinasema kwamba tuhuma zake zimebadilishwa. Awali alikuwa anatuhumiwa kwa kumuunga mkono Profesa Mwandosya katika hicho kinachodaiwa kuwa ni maandalizi ya mapema ya kuwania urais mwaka 2010, lakini sasa anatuhumiwa kwa ukosefu wa utiifu kwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa (Mulla).
  Kinachodaiwa kuwa ni ukosefu wa utiifu kwa Mwenyekiti wa Chama wa Mkoa ni hatua ya Dk. Mwakyembe kukubali kupokewa na umati mkubwa wa watu siku aliporejea Kyela baada ya kuwasilisha ripoti ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu Richmond ambayo hatimaye ilisababisha kujiuzulu kwa Lowassa, mawaziri Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha.
  Inadaiwa kwamba Mulla alimkataza asishiriki katika mapokezi hayo kwa kuwa hayakubarikiwa na Chama, na kwamba alikasirika zaidi baada ya Dk. Mwakyembe kueleza wakati akihutubia umati huo kwamba alikuwa amezuiwa na yeye (Mulla) kushiriki katika mapokezi hayo.
  Kwa mujibu wa Ofisa huyo wa CCM Mkoa, barua zenye tuhuma dhidi ya wanasiasa hao wawili tayari zimekwisha kutawanywa kwa baadhi ya wabunge wa CCM wa mkoa huo na kwamba njama hizo za kuwamaliza kisiasa Profesa Mwandosya na Dk. Mwakyembe zinaeleweka kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa kitaifa wa CCM walio kwenye mtandao na inadaiwa wameubariki mpango huo.
  Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa nchini wanaamini kwamba kama kutokuelewana huko kwa CCM mkoa wa Mbeya hakutashughulikiwa, chama hicho kitaupoteza kabisa mkoa huo kwa wapinzani katika uchaguzi wa mwaka 2010.
  "Kampeni hii ya kuwamaliza kisiasa kama itafanikiwa itaiumiza sana CCM mwaka 2010. Kwanza Profesa Mwandosya na Dk. Mwakyembe wana ushawishi mkubwa si tu kwenye majimbo yao bali vilevile mkoa mzima na pia miongoni mwa wabunge wenzao," alisema.
  Profesa Mwandosya hakupatikana jana kwa simu kuzungumzia suala hilo, lakini Dk. Mwakyembe yeye alipopatikana hakupenda kulizungumzia suala hilo mbali ya kukiri kusikia kuwepo kwa tuhuma hizo dhidi yake.
   
 15. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Yeah! The story going around by then had a woman involvement in it. The Prof had to resign and went back to his teaching post!
   
 16. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  nami nasubiri mwenye details za hili,japo mwaka 2007 wakati ya uchaguzi wa wajumbe wa nec mkoa pale mbeya niliona purukushani za hapa na pale,apson mwangonda ilisemekana alikuwa anaungwa mkono na jk na mwandosya alikuwa haziivi na jk,japo kwangu nilidhani labda ni mambo yaliyosababishwa na kuomba ridhaa ya chama mwaka 2005 kwaajili ya urais,lakini kwa kilio hicho nadhani kuna jambo zito nyuma tusilolijua.pia nimetazama picha hapo juu ambapo jk anaonekana kuteta jambo na mwandosya lakini akiwa na ulinzi mzio,je mwandosya ni hatari kiasi hicho.naendelea kusubiri naweza cha kujifunza jambo na nitawatafuta wazee wanaowajua watu hawa wote wawili.
   
 17. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #17
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,474
  Likes Received: 5,858
  Trophy Points: 280
  And the woman is of fair skin and currently lives in Upanga..............used to be a cashier at the Ministry
   
 18. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  My hat is off to you Sir!
   
 19. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,474
  Likes Received: 5,858
  Trophy Points: 280

  Even now as a grandmother she still sparkles......and drives a posh thing
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wanawake na Maendeleo is a woman involved
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...