JMWAKA
JF-Expert Member
- Jun 18, 2012
- 694
- 574
Ndugu marafiki na watanzania wenzangu, taarifa zinasambaa kwenye mitandao mbalimbali za kijamii zikilenga kuaminisha umma kwamba nimetoa tamko kuhusu lile linaloelezwa kama "shambulizi" dhidi ya Maaskofu wa Kanisa. Ujumbe huo sio wa kweli, ni wa uzushi na ni wakugushi. Hivyo basi ni ujumbe wa kupuuzwa. Nikiwa Mwalimu, Mbunge, na Waziri mstaafu nina nafasi pekee ya mawasiliano na viongozi wa Serikali, Waheshimiwa Masheikh na Maaskofu, na Taasisi nyingine kwa njia zinazoweza kuleta matokeo chanya.
Mimi ni muumini wa uhuru wa kujieleza na kutoa mawazo. Huu umekuwa msingi wa maendeleo na kukua kwa uelewa kwa karne nyingi. Hata hivyo kusambaza taarifa za uongo sio tu ni dhambi bali ni kosa la jinai, na bila shaka kitendo hicho kina madhumuni hasi.
Mark Mwandosya,
Lufilyo
Busokelo
8 Juni 2018
Ameyaandika hayo kwenye mtandao wa twitter.