Mwandishi ZNZ akamatwa kwa 'Uchochezi!!!'! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandishi ZNZ akamatwa kwa 'Uchochezi!!!'!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Oct 26, 2007.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna habari kwamba Mwandishi wa Habari wa IPP wa PST, Nipashe na Guardian amekamatwa kwa uchochezi Zanzibar. na pia kuna habari kwamba waandishi wa TVT na RTD wamepata ajali Korogwe wakiwa njiani kwenda Moshi kumzika Salome Mbatia. Habari zaidi baadaye
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Oct 26, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  duh.. hii sasa mbaya..
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ni mwandishi gani huyo? na uchochezi gani alioufanya?

  tuhabarisheni
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2007
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Duuh...!
  Makubwa haya
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2007
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mmmh .....
  fanya utupatie habari kamili
   
 6. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2007
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mhh..haya tunasubiri habari zaidi
   
 7. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  halisi maendeleo ya hii stori vipi?
   
 8. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hizi ajali naona zitawafanya waweke umuhimu unaotakiwa katika sekta ya barabara na usafirishaji.

  Je, ni uchochezi wa namna gani ambao huyo mwandishi ameshikiliwa?
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Naomba radhi jana kwa kupotea kutokana na matatizo ya kiufundi. Hii ndio habari kamili kama ilivyosambazwa na mwandishi mwingine wa habari wa Zanzibar, Jabir Idrissa.


   
 10. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Na jabir idrissa, Zanzibar

  Jeshi la Polisi limeshindwa kumfungulia mashitaka mwandishi wa habari wa kampuni ya The Guardian Limited, Mwinyi Sadallah, na badala yake ametakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi kila Jumatatu asubuhi.

  Hakuna muda maalum uliowekwa wa mwandishi huyo kuwa anaripoti kituoni Mwembemadema yalipo makao makuu ya Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi.

  Sadallah ambaye amekuwepo hapa kwa miaka 11 sasa akifanya kazi ya uandishi wa habari chini ya kampuni hiyo, alipewa amri hiyo jana baada ya kufika kituoni hapo saa 3 asubuhi kama alivyotakiwa Ijumaa ya wiki iliyopita alipoachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili, akiwemo binafsi, kila mmoja akisaini dhamana ya maandishi ya sh milioni moja.

  Alikamatwa Oktoba 26 akiwa ofisini kwake Weles, Kikwajuni, na kufikishwa Mwembemadema alikotakiwa kusaini hati ya mashitaka akidaiwa kuwa amefanya uchochezi kwa kuandika habari zilizomhusu Rais Amani Abeid Karume zikisema kuwa ameuza kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mafuta kinachomilikiwa na kampuni ya Gapco.

  Alipofika jana alitakiwa tena kusaini hati hiyo, lakini aliposhikilia kukataa, safari hii akiwa na wakili Hamidu Mbwezeleni wa mjini hapa, alichukuliwa alama za vidole na kujazwa kwenye fomu nne tofauti kabla ya kuamriwa kutoka na kufuatana na maofisa wa Idara ya Upelelezi ya Mkoa hadi Makao Makuu ya Polisi Kilimani.

  Wakili huyo alisisitiza kuwa raia ana haki ya kukataa kusaini hati ya Polisi na kutoa maelezo yoyote na kwamba ni sheria kusema kuwa atafanya hivyo mbele ya Mahakama.

  Kutoka Mwembemadema, Sadallah alipelekwa kitengo cha picha na kupigwa picha mara mbili ambazo hakuelezwa zinatumika kwa ajili ya kitu gani.

  Baada ya kitendo hicho, alielezwa kwamba yuko huru isipokuwa atahitajika kuripoti kituoni Mwembemadema, kila Jumatatu saa 3 asubuhi. Atakapofika, aonane na ofisa upelelezi aitwaye Khatib Juma na asipokuwepo amuone Koplo Abbas au Mwita.

  Wiki iliyopita, Sadallah baada ya kufika kituoni, aliambiwa kuwa atashitakiwa chini ya Sheria ya Magazeti ya mwaka 1988 ya Zanzibar . Kifungu kinachozungumzia habari za uchochezi, kinasema mtu akitiwa hatiani kwa kosa hilo , anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka mitatu jela.

  Habari alizoandika mwandishi huyo na kuchapishwa kwenye toleo la Nipashe la Septemba 24, mwaka huu, zilitokana na malalamiko ya mwananchi mkazi wa Chwaka, Ramadhan Mohamed Vuai, dhidi ya kuporwa kiwanja chake cha urithi kilichopo eneo la Kipilipilini ambacho sasa pana kituo cha mafuta cha Gapco.

  Kwa mujibu wa habari hizo, mwananchi huyo alieleza kuwa amelazimika kufungua kesi kwenye Mahakama ya Ardhi ya Zanzibar kudai haki yake ya kumiliki ardhi ambayo imeporwa bila ya idhini yake, hatua iliyokwenda kinyume na sheria.

  Katika malalamiko hayo, Vuai anadai kuwa alipofuatilia kiwanja chake kwa kampuni ya Gapco, walimweleza kwamba wao hawawezi kumsaidia kwa lolote kati ya madai yake, kwa kuwa wamepata eneo hilo kwa idhini ya Rais Karume ambaye walidai ananufaika na asilimia 30 ya biashara.

  Mwananchi huyo aliamua kumuandikia Rais Karume binafsi, akimuomba amgawie sehemu ya asilimia hiyo ili naye anufaike na eneo hilo ambalo amekuwa akilitegemea kwa maisha yake.

  Hakupata majibu ya barua hiyo na badala yake baadhi ya maofisa wa Ikulu walimtaka asifuatilie tena hapo kwa kumueleza kuwa Rais hahusiki na suala hilo .

  Barua aliyomuandikia Rais Karume, ni moja ya vielelezo vyake katika kesi aliyofungua akiomba mahakama ibatilishe umiliki wa kiwanja hicho na kumrudishia kwa sababu ana hati halali za kukimiliki.

  Ametaka kituo hicho kivunjwe kwa amri ya mahakama hiyo, alipwe fidia ya asilimia 30 ya mauzo yaliyokwishafanyika hapo, tangu kituo kilipoanza kutoa huduma. Kesi hiyo namba 67 ya mwaka 2007, haijaanza kusikilizwa.
  Ends
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2007
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Pole kamanda Mwinyi Sadallah...
   
Loading...