Mwandishi wa ThisDay/Kulikoni afariki ghafla

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Taarifa iliyosambazwa na UONGOZI WA MEDIA SOLUTION WAMILIKI WA THISDAY NA KULIKONI:


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MWANDISHI wa habari mwandamizi Godrefy Mhando (63) amefariki dunia leo asubuhi jijini Dar es Salaam kwa matatizo ya moyo.

Mhando ambaye hadi kifo chake alikuwa mhariri msanifu wa gazeti la Kulikoni, linalochapishwa na Kampuni ya Media Solutions Limited amefariki leo asubuhi muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya Burhani.

Familia ya marehemu ikielezea kuhusu kutokea kwa kifo chake, ilieleza kuwa Mhando leo asubuhi alikuwa amejiandaa kuelekea kazini, lakini kabla hajaondoka nyumbani, alijisikia vibaya, hasa kubanwa na kifua na mapigo ya moyo kuongezeka, ndipo alipopelekwa hospitali ya Madonna, iliyopo Tabata.

Hata hivyo, madaktari walishauri apelekwe hospitali ya Amana, ingawa familia iliamua kumpeleka hospitali ya Burhani ambako alifariki dunia hata kabla ya kuanza kupatiwa huduma.

Mhando aliwahi kuajiriwa na Kampuni ya magazeti ya Chama Cha Mapinduzi ya Uhuru na Mzalendo ambako alifanya kazi kwa muda wa miaka 30 kabla ya kustaafu mwaka juzi kujiunga na Media Solutions Limited kama mwajiriwa wa muda (part-time staff).

Alizaliwa mwaka 1944 jijini Dar es Salaam na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya Mchikichini kuanzia mwaka 1952 hadi 1955 na kuendelea na shule ya kati ya wavulana ya Uhuru hadi mwaka 1959 alikohitimu.

Kuanzia mwaka 1960 hadi mwaka 1964 alijiunga na Shule ya Sekondari Kiungani, Zanzibar na baadaye kwenda Chuo cha Kimataifa cha Mawasiliano ya Umma cha Szechoslovakia ambako alisoma uandishi wa habari na kutunukiwa stashahada.

Alirejea nchini na kuanza kazi Uhuru na Mzalendo akiwa mwandishi wa habari na mwaka 1990 hadi 1991, alikwenda Ujerumani kwa masomo ya Sayansi ya Jamii katika chuo cha Magdeburg ambako alitunukiwa stashahada.

Mhando ameacha mke na watoto kadhaa. Taratibu za mazishi zinapangwa na familia ya marehemu Mhando nyumbani kwake Tabata Segerea, eneo la Mangumi.
 
RIP mzee Godrefy Mhando, bwana alitoa bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe.
 
hakika kwake tumetoka na kwake ndio marejeo yetu.
mungu amlaze pema
 
Duh.. tunawapa pole familia ya Ndg. Mhando, wafanyakazi wa This Day na Kulikoni na jamaa na marafiki wote kwa msiba huu. Poleni sana.

Requiem in Pacem (RIP)
 
Nilikutana na Mhando siku moja tu, lakini he made a lasting impression on me.

He was a charming, kind and warm person, very friendly to all he met, even for the first time. He was willing to go out of his way to help others. He will be truly missed.

Innalillahi wa Innalillahi Raaj'un! Hakika Kwake Yeye Tumetoka, na Hakika Kwaye Yeye Twarejea!
 
mungu ampuzishe kwa salama na amani bwana Godfrey Mhando.

nnaomba kuuliza TIdo Mhando na huyu ni ndugu au majina yamefanana?
 
Hawana uhusiano na Tido Mhando, ila wana nasaba na Jimy Mdoe
 
RIP mhando,Bwana ametoa na bwana ametoa.jina lake lihimidiwe..Mikoba yako naamini bado ipo na tutaendelea kumkoma ntani giladi kama kukuenzi.Amin
 
Back
Top Bottom