Mwandishi wa Mwananchi ashambuliwa na askari akitekeleza majukumu yake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) Zanzibar, Jesse Mikofu ameshambuliwa na askari wa vikosi vya SMZ wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi leo asubuhi Jumatano Aprili 21, 2021.

Mikofu amekumbwa na kadhia hiyo baada ya kuwapiga picha askari hao wakati wakitekeleza jukumu lao la kuwahamisha wamachinga waliopanga bidhaa zao barabarani katika eneo la darajani.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadh Juma Haji amesema hana taarifa za tukio hilo na kuahidi kutoa ushirikiano zitakapomfikia.

ashambuliwpiiiic

Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) Zanzibar, Jesse Mikofu
Akisimulia hali ilivyokuwa, Mikofu amesema pamoja na kupigwa, kuvutwa, kutakiwa kugaragara kwenye maji machafu na kupiga push-up, vifaa vyake vya kazi ikiwemo simu ya mkononi aliyoitumia kupiga picha vimeharibiwa.

“Nilifika darajani na kukuta askari wanabeba meza zilizokuwa zikitumiwa na wamachinga na kuzipandisha kwenye magari yao, nikatoa simu na kuanza kupiga picha, nyuma yangu wakatokea askari wakanihoji nikajitambulisha na kuonyesha vitambulisho.”

“Hawakuridhishwa wakanipeleka kwa kiongozi wao ambako huko ndiko nilikokutana na adhabu, niliambiwa nikae chini ninyooshe miguu, nipakate mawe makubwa wakiniambia niyabembeleze kama mtoto,” amesema.

Pamoja na adhabu hiyo Mikofu aliendelea kupigwa na askari hao wakimtaka kuonyesha picha alizopiga na baadaye kumlazimisha kubadili nywila kwenye barua pepe yake.

“Kiongozi wao akaandika namba yake kwenye simu yangu ili nimtumie zile picha nikazituma, wakaniambia nibadilishe passwords (nywila) nikagoma, akaitwa askari mwingine akabadilisha palepale, kisha wakanilazimisha niipige ile simu kwenye mawe hadi ivunjike, sikuwa na namna nyingine nikafanya hivyo,” amesisitiza.

asmbuliwapicccccc

Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) Zanzibar, Jesse Mikofu
Amesema pia akaelekezwa kuingia kwenye dimbwi la maji ya mvua yaliyotuama na kugaragara kwenye maji hayo na baada ya kitendo hicho aliruhusiwa kuondoka katika eneo hilo.
IMG-20210421-WA0054.jpg
 
Kama ilikuwa ni zoezi la amri halali ya kiongozi kuwapiga picha wanapotekeleza majukumu yao kuna tatizo gani hadi astahili mazila yote hayo?
 
Hivi haya mambo yameanza znz r lini?tulikua tunayasikia bara duuuh huu ni zaidi ya unyama,ngoja tusubiri mwisho wake kila zama na wakati wake,inasikitisha saaaana
 
Hivi angegoma kutimiza amri hizo ingekuwaje? Maana kazitimiza, bado kapigwa na kufanyiwa unyama wote huo! Kama mimi nagoma toka mwanzo na liwalo liwe!
 
“Hawakuridhishwa wakanipeleka kwa kiongozi wao ambako huko ndiko nilikokutana na adhabu, niliambiwa nikae chini ninyooshe miguu, nipakate mawe makubwa wakiniambia niyabembeleze kama mtoto,” amesema.



dahhhh nimecheka ila inasikitisha sana asee
 
Pole sana ndugu mwandishi, Sheria ichukue mkondo wake haraka. Hao maaskari wafukuzwe. Ila nimecheka kishenzi hapo kwenye kubembeleza mawe hahah. Pole sana.
 
Uyo kamanda Awadh juma ni nuksi kabisa hafai,alikuwa uku dar alishawai kukamata gari ya mke wa marehemu balozi Mahiga
 
Jina la mwandishi linaonekana kama mtu wa huku bara hapo mateso yamezidi kwa chuki, Wanzanzibar wabaguzi sana hasa Wapemba
Unaweza kukuta hao waliofanya huo ubaya pia wametokea huku
Kwa kawaida yao wazanzibari hawana tabia hizo
 
Halafu utakuta wamefunga(naamini hivyo,usilete ujuaji) Mungu ana kazi sana aisee..
 
Back
Top Bottom