Mwandishi wa Kwizera Fm George Bahamu atupwa porini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Mwandishi George Bahamu ambaye ni mwakilishi wa redio Kwizera Fm iliyoko Ngara kwa Mkoa wa Tabora ametupwa porini na watu wasiojulikana.

Amefanikiwa kuachiwa simu na kusambaza ujumbe kupitia namba yake ya 0714 825366 kuwa ametekwa.

Binafsi yangu nimemtafuta asubuhi hii na kuongea nae na amesema alikutana na watu ambao walimhoji na baadaye kujikuta ametupwa kwenye pori asilolijua.

Hadi sasa anatafuta msaada wa kufahamu njia ili atoke porini.

Tunaendelea na jitihada za kutafuta msaada wa kumuokoa hasa kwa kuwasiliana na Jeshi la polisi.

Waandishi mlioko Tabora tusaidiane kufuatilia tukio hili.

Edwin Soko

========

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa, amesema kuwa Mwandishi wa Habari wa Radio Kwizera, mkoani humo George Bahamu, anayedai kutekwa na kutelekezwa porini huenda alikuwa na mambo yake binafsi kwa sababu mtekaji hawezi kukuacha kienyeji tu.

Akizungumza na EATV &EA Radio Digital, leo Desemba 5, 2019, Mwakalukwa amesema kuwa mtu yeyote aliyetekwa hawezi kupiga simu yake mwenyewe na kutaja eneo alipo.

"Huyo wala hajatekwa alikuwa na mambo yake binafsi, mtu aliyetekwa hawezi kuongea kwa simu na akasema jamani nipo mahala fulani, kwahiyo nimemtuma OCD akamuangalie anaweza akawa na mambo yake ya ajabu, pengine mambo ya wanawake, mnapenda tui 'destroy' Tasnia yenu ya Habari, mtu anayetekwa hapigi simu na watu hawakuachi kienyeji tu" amesema RPC Mwakalukwa.

Inadaiwa kuwa Mwandishi huyo ametoweka jana jioni Desemba 4, 2019 na asubuhi ya Desemba 5 alijikuta ametupwa katikati ya Pori, lililopo maeneo ya Ipuli mkoani humo, ambapo pia Kamanda Mwakalukwa amemuagiza Afisa Upelelezi kufika eneo la tukio.
 
Kama ana smartphone mwambieni awashe location, kisha aingie kwenye google map, na aulize alipo. Akishajua alipo aulize njia ya kufika sehemu changamfu.

Au aitume hiyo location kwa whatsapp kwa watu wake wa karibu ili wamfuate. Aingie whatsapp kisha contact anayotaka kuitumia location, abonyeze vile vipini vilivyo sehemu ya kutype, achague location, kisha atume.
 
Well said, aingie WhatsApp then aende "share location"
Kama ana smartphone mwambieni awashe location, kisha aingie kwenye google map, na aulize alipo. Akishajua alipo aulize njia ya kufika sehemu changamfu.

Au aitume hiyo location kwa whatsapp kwa watu wake wa karibu ili wamfuate. Aingie whatsapp kisha contact anayotaka kuitumia location, abonyeze vile vipini vilivyo sehemu ya kutype, achague location, kisha atume.
 
Duuu wameanza tena... Ila hawa wa safari hii inaelekea sio wabaya kivile

Back
Top Bottom