Mwandishi wa Kimarekani akamatwa Tarime: Aingia nchini kinyume cha sheria; apiga picha waliouawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandishi wa Kimarekani akamatwa Tarime: Aingia nchini kinyume cha sheria; apiga picha waliouawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rejao, May 27, 2011.

 1. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  POLISI katika Kanda Maalumu ya Tarime-Rorya, wamemkamata raia wa Marekani kwa tuhuma za kupiga picha maiti za mauaji ya mgodini Tarime na kuzituma nje ya nchi bila kibali.

  Joyceline Tembi anayehisiwa kutumiwa na wafadhili wa nje wa vyama vya upinzani nchini, anadaiwa kuingia nchini kama mtalii akitoka Uganda.

  Alikutwa akiongozana na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika vurugu zilizotokana na mauaji ya watu hao yaliyofanywa na polisi baada ya kuvamia Mgodi wa North Mara Barrick.

  Kamanda wa Polisi wa Tarime na Rorya, Costantine Massawe alisema jana kuwa Joyceline alikutwa akipiga picha za matukio ya vurugu zikiwemo miili ya watu wanne kati ya watano waliouawa wakati kundi la watu zaidi ya 800 walipovamia mgodi huo wa Nyamongo.

  “Ameonekana akiongozana na wafuasi wa Chadema kila mahali, hali inayofanya tumtilie mashaka, iweje huyu mtalii aongozane na wafuasi wa Chadema?” alihoji Kamanda Massawe.

  Kwa mujibu wa Kamanda Massawe, Joyceline ambaye baada ya kuhojiwa, alidai kuwa yeye ni mwandishi wa habari anayefanya kazi nchini Uganda na Marekani, alipiga picha hizo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Wilaya ya Tarime.

  Marehemu hao ni Chacha Ngoka wa Kewanja, Nyamongo, Emmanuel Magige wa Nyakunguru, Mwikwabe Marwa na Chawali Bhoke; wote wa Mugumu Serengeti.

  Mbali na picha za maiti hao, Joyceline pia anadaiwa kufika katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime juzi na kupiga picha watuhumiwa wa uchochezi akiwemo Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) na watuhumiwa wenzake saba.

  Washitakiwa wengine katika kesi hiyo iliyofikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Mei 24 ni Mwita Waitara (36), Mwita Maswi (48), Abdalah Suleman ‘Sauti’ (31), Stanslaus Nyembea (33) na Underson Chacha (35) ambao ni wakazi wa Tarime.

  Wengine ni Andrew Andalunyandu (63) na Irahim Juma (27) ambao ni wakazi wa Singida. Baadaye Joyceline anadaiwa alipiga picha baadhi ya majengo ya Serikali ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Tarime na kutuma baadhi ya picha hizo nje ya nchi.

  Kamanda Massawe alisema Joyceline mwenye hati ya kusafiria ya Marekani iliyoandikishwa Aprili mwaka huu, anaendelea kuhojiwa na polisi pamoja na maofisa uhamiaji wilayani hapa kutokana na ujio wake huo wenye utata.

  Kamanda Massawe alisema hati ya kusafiria ya Joyceline namba 7100566100, inaonesha aliingia nchini Mei mosi mwaka huu 2011 na kuondoka na baadaye akarudi tena Mei 22 na kuanza kupiga picha za matukio hayo ya vurugu na maiti.

  Ofisa Uhamiaji wa Wilaya ya Tarime, Isack Mayeka amethibitisha kukamatwa na kuhojiwa kwa Joyceline na kuongeza kuwa hata kama ni Mwandishi wa Habari, hakupaswa kufanya kazi ya uandishi katika nchi nyingine kabla hajajulisha vyombo vya usalama.

  Mayeka alisema Joyceline pia alitakiwa kutoa taarifa kwa Idara ya Habari (MAELEZO) au Baraza la Habari Tanzania (MCT) na kufuata utaratibu wa nchi husika.

  Alisema kwa kitendo hicho cha Joyceline kuingia nchini na kuanza kupiga picha za matukio hayo bila kutaarifu idara na mamlaka husika, kinatia shaka ujio wake hapa nchini.

  Mayeka alisema yeye na maofisa wengine wa Polisi wanaendelea kumhoji zaidi mwanamke huyo kuhusu ujio wake nchini kwa kuwa anatia shaka huenda anatumiwa na vyama vya upinzani na wafadhili wa baadhi ya vyama hivyo.

  Wakati huo huo, Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine (CCM) amewapiga marufuku wanasiasa wachochezi kufika jimboni humo kwa sababu wanazorotesha kasi ya maendeleo.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Nyangwine alisema hawezi kuwavumilia wanasiasa wa aina hiyo na kuwataka wakae kwenye maeneo yao ili walete maendeleo.

  Alisema, muda wa kampeni na ushindani wa kisiasa umekwisha hivyo kila mmoja aelekeze nguvu zake kwenye shughuli za maendeleo na kutekeleza ahadi walizotoa.

  “Wilaya ya Tarime inayo mamlaka kamili ya kujitegemea kama serikali, sasa nawataka wanasiasa na wabunge wa upinzani watuache, matatizo ya Tarime tunayatatua wenyewe hatutaki kuingiliwa.

  “…Naomba wananchi wa Tarime waniunge mkono katika hili nataka tukae tushikamane kuleta maendeleo na kutekeleza ahadi nilizotoa wakati naomba ridhaa yenu.

  “Sitakubali kuwaona watu wanakuja kutuvuruga… kama wanataka kuja kwetu waje kwa shughuli za maendeleo na sio vinginevyo,” alisema Mbunge huyo ambaye hivi karibuni msafara wake ulishambuliwa kwa mawe na wanachi aliodai kwamba wameshawishiwa na wanasiasa wengine.

  Kwa upande wake, Mwakilishi wa wazee wa mila wilayani humo, Enock Chambiri alisema wanalaani kitendo cha baadhi ya wananchi kuushambulia kwa mawe msafara wa mbunge wao.

  Alisema wananchi wa Tarime hawana desturi ya kuwapiga viongozi wao na kubainisha kwamba kilichotokea ni ushawishi na msukumo wa kisiasa.

  “Kwa niaba ya wazee 26 wanaowakilisha koo 13 kule Tarime na serikali kwa upande mwingine, tunalaani kitendo cha baadhi ya wanasiasa kutumia muda wao kulivuruga jimbo letu,” alisema Chambiri.

  Katika hatua nyingine, CCM imeitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina wa vifo na mazingira ya vifo hivyo vya Tarime na pia itafute ufumbuzi wa kudumu wa migogoro inayotokea mara kwa mara kati ya wananchi wanaozunguka migodi na wawekezaji.

  “Hata hivyo, Chama Cha Mapinduzi kilaani vikali tabia iliyojionyesha dhahiri kwa baadhi ya wanasiasa nchini kuvifanya vifo vya Watanzania wenzetu kuwa mtaji wa kisiasa,” ilieleza taarifa ya Idara ya Itikadi na Uenezi Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM jana.

  SOURCE: HABARI LEO 27/05/2011
   
 2. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Una matatizo sana ww! Soma title na content yako,kipi title na kipi content? Na ile Darwin's nightmare ilikuwa ya cdm? Acha izo !
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  siku hizi kila kitu chadema sio......mlevi akilewa mnasema kapewa hela n chadema.....
   
 4. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,176
  Trophy Points: 280
  Sasa hapo JK Atakuwa kachoka Wamarekani huwa hawasingiziwi Shauri yao Kitatumwa Kikosi kile kilichomuua Osama Kiende kumtoa huko Lupango na kiwauwe makamanda wote Hao Wasio hata na chembe ya Ubinadamu Masawe! Wacha wawachokoze kwa kusingizia wamarekani ni Chadema Utamu hapo.

  Marekani hafurahishwi na Serikali Dharimu kama hii Ataiondoa tu.. na kama Haki za Binadamu zinavunjwa Wazi na wavunjaji hawaovuliwi Gamba yaani Tunahitaji Msaada wa Marekani.
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Source habari leo na habari za kupikwa
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  hii habari imeandikwa na gazeti habari leo.

  lakini imekula kwao maana picha zilishatumwa tayari.
   
 7. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Utakuwa na matatizo wewe! Kwani hapo ni nini hakieleweki?
   
 8. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mbona kuna picha kabisa anapelekwa rumande? Au na picha wameiedit?
   
 9. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  habari ya kutengenezwa wanazuka mtaan wanakuta mzungu anatembea wanamnyaka wanasema eti yuko kwnye furugu za tarime

  kama wan uhakika na wanataka kuleta nuksi wafikishe issue hii US embassy watawatokea puani
   
 10. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  kosa lake nini? kupiga picha? sio yeye tu, wapiga picha wote walikamatwa na kunyang'anywa camera zao na picha kuharibiwa so ishu sio mmarekani ishu ni wapiga picha wote wamefanyiwa kama huyo mmarekani. Moja ya vitu vibaya sana kwa wamarekani ni kuwanyima habari....sasa sikia moto wake....mwaka huu...halina cha ubani wala udi...lishavunda harufu lazima itoke tuu!!
   
 11. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  inanikumbusa zile za bush bush...bundi akilia tu-fulani huyo...paka akilia tu-fulani huyo....mtoto akikohoa tu-fulani huyo.....sasa kila kitu ni CDM!!!! Tukio la Nyamongo (State assasination) ni media attention so watu wa media tofauti lazima wangeenda tu kuripoti....mbona hamsemi na yule jamaa ya NTV wa Kenya aliyekamatwa huko? nae pia ni CDM? mnalo mwaka huu!!
   
 12. Rayz of Diamond

  Rayz of Diamond Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda tumesikia tofauti!!
  Sikio langu limesikia kuwa yule ni Mwanahabari, alikuwa kazini na hajaenda kwa Mgongo wa CHADEMA.
  Na kama anavyosema Ng'wanangwa ni kuwa wamemkamata wakati tayari ameshatuma hizo Picha za vurugu ya Tarime.
   
 13. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
 14. h

  hans79 JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  kaz ipo tz,hao vipolis wanaogopa nn walisema cdm ndo wahusika wa yote yaliyotokea Tarime?tz kaz kwel kwe kwa viaskar vyake na biashara ya madin,mayai ya kuku,ujambaz,kes bandia,kuua raia,kuiba kura etc,jk aliwaambia dom uwongo ukinenwa sana huaminiwa,pana shaka na kaul ya vipolis tz.yana mwisho
   
 15. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  kaaaaah na wewe andika kama mtu aliyeenda SHULE
   
 16. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Yale yale ya Sophia Simba kwamba CHADEMA wanafadhilia na EU kuleta vurugu.
  Mabalozi wa EU walipomwambia athibitisha madai hayo akaingia mitini.

  Sasa kama kweli CCM wanadai huyo mwanahabari wa Marekani ametumwa
  na CDM naona hawajipendi, tofati na EU, Marekani haitishiwi nyau, CCM itakuwa
  imemuweka pabaya JK in international arena. Niliwahi kusema CCM IS A MENTAL
  DISEASE once you're in CCM then you can't think and reason normally because
  of the VIRUS that causes mental illness!
   
 17. g

  gambatoto Senior Member

  #17
  May 27, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata, sijamwelewa, :pound:
   
 18. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hahahahaha :biggrin1::biggrin1:
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Tuwekee basi hiyo picha
   
 20. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kila mti watakimbilia na kung'ang'ania.....! lakini kwa kuwa siku ya kufa nyani mti yote huteleza, basi na kila watakapokimbilia na kujaribu kung'ang'ania patateleza tu, na hivyo watadondoka tu.......! Walipekua kila kona ya nchi na dunia wakitafuta walau ukweli wowote wa kutungia wimbo, lakini wamekwama...... Na sasa wanaendelea kupekua kila kona ya dunia kutafuata walau uwongo wa kuwapumbaza Watanzania ili wapate kujinusuru na anguko lao siku za usoni...... Lakini kwa kuwa uwongo siku zote haujengi, basi watazidi kujimalizia wenyewe bila kujua....!
   
Loading...