Mwandishi wa Hayati Karume: Karume aliamuru watoto wote wa shule walale kufikia saa 1:00 jioni

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,386
Nasikiliza hapa simulizi za maisha ya watu wa Zanzibar enzi za utawala wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kupitia Star TV...

Wanaongea watu wengi lakini aliyenivutia zaidi ni aliyekuwa Mwandishi wake enzi zile Bw. Enzi Taalib...anasema Sheikh Karume alitawala kwa "decrees" na moja ya decree hizo ni ile iliyowataka WATOTO WOTE WA SHULE KULALA IFIKAPO SAA 1:00 JIONI/USIKU...funny!

Anasema pia kulikuwa na majaribio zaidi ya 12 ya kumpindua Sheikh Karume.

Mtoto wake Ali Karume anasema kuna kijana mmoja mwanajeshi anaitwa 'Mahfoudh' alipata kumtamkia yeye Ali kuwa kuwa maisha yanapita tu na iko siku ambayo haikuwa mbali sana yeye 'Mahfoudh' angewatawala akina Karume kama ambavyo wao walikuwa wakimtawala yeye na Wazanzibar wengine kwa wakati huo... Ali anasema kauli hii ilimsumbua sana nafsini mwake na hivyo wakati mmoja wakiwa wameketi mezani wanakula chakula na baba yake alimwambia baba yake kuhusu jambo hilo lakini Sheikh Karume alionekana hakujali sana inshu hiyo na hivyo akamtaka mtoto ale chakula akalale na kwamba wao walikuwa salama...Ali anasema haukumalizika mwezi kweli Mzee Karume akauawa...

Zanzibar ina simulizi tamu!
 
Back
Top Bottom