Mwandishi wa Habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera aomba msamaha kwa Rais Magufuli

alexelias

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
2,032
3,198
Kupitia kwa Wakili wake Jebra Kambole ameomba pengine katika kazi yake ya Uandishi wa habari kama aliteleza na kuandika habari ya kukwaza, anaomba asamehewe

'Kwa niaba yake tunamwombea radhi kwa Mheshimiwa Rais amsamehe na yupo tayari kufanya lolote ili tu awe huru na akaungane na familia yake' amesema Jebra.

My take;Unapofanya ujinga na kwa chuki binafsi tena kwa kuisaliti Nchi yako kwa tamaa ya pesa na madaraka mwisho wake ni mbaya.
******

Mwandishi wa habari nchini Tanzania, Erick Kabendera amemwomba radhi Rais na Serikali ya nchi hiyo akiomba kusamehewa kama kuna makosa ameyafanya.
Kabendera amesema hayo leo Jumanne Oktoba 1, 2019 jijini Dar es Salaam kupitia kwa wakili wake, Jebra Kambole.

Kambole amesema hayo muda mfupi baada ya kesi inayomkabili mwandishi huyo ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha Sh173.24 bilioni kuahirishwa hadi Oktoba 11, 2019 kutokana na upelelezi kutokamilika.

“Sisi kama mawakili tunatoa ombi kwa Rais, kama Erick katika utendaji kazi wake kama kuna mahali alimkosea Rais au Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa niaba yake, familia yake, ndugu zake tumwombe radhi,” amesema Kambole

Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anadaiwa katika siku tofauti kati ya Januari 2015 na Julai 2019 jijini Dar es Salaam, alitoa msaada katika genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Katika shtaka la pili, inadaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa bila kuwa na sababu za msingi kisheria alishindwa kulipa kodi ya Sh173.24 milioni ambayo ilitakiwa ilipwe kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la utakatishaji fedha, kati ya Januari 2015 na Julai 2019 ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam mshtakiwa alijipatia kiasi hicho cha Sh173.2 milioni wakati akizipokea alijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kukwepa kodi na kujihusisha na genge la uhalifu.

Soma: Breaking News: - Erick Kabendera aachiwa huru baada ya kukiri makosa na kufutiwa shtaka
 
Back
Top Bottom