Mwandishi wa habari huwezi kuwa vuguvugu:Dk. Azavaeli Lwaitama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandishi wa habari huwezi kuwa vuguvugu:Dk. Azavaeli Lwaitama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by gabatha, Sep 17, 2012.

 1. g

  gabatha Senior Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kufuatia kifo cha Mwangosi dk. Lwaitama amesema haiwezakani mwandishi wa habari ukawa in btn . ni either unakuwa kny kusimamia haki au kwny ukandamizaji na si vinginevyo.Amedai kuwa waandishi wa wa kweli ni ktk Mwanahalisi na marehemu Mwangosi ambao wameonekana kutaka kusimamia ukweli tofauti na wanafiki wengine km akina Neville, Msacky na wengine.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Kila mtu - hata waandishi wanaopokea vibahasha- anasema anasimamia haki. Na wengine wanasema haki inataka mtu mwenye balance, asiye activist journalist wala government stooge, kwa hiyo anatakiwa kuwa vuguvugu kwa maana hiyo.

  Kusema mwandishi anatakiwa asimamie haki ni rahisi, tatizo haki ni nini?

  Ni kususia kuandika habari za polisi na kumnyima mwananchi habari muhimu? Ni kuchagua upande wa kuutetea hata kabla ya kupata habari kamili ili tu usiitwe "vuguvugu"?
   
 3. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  unajua wakati mwingine mtu akiwa mfupi, hata akili zake huwa ni fupi, kila kitu kwenye maisha yake ni kifupi tu, mikono yake nayo mifupi, miguu mifupi, vidole vifupiii kila kitu kifupii na akil ivilevile....hata usome ufike wapi ni mfupi tu....akili za mbayuwayu changanya na za kwako.
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Kazi yao ya kwanza ni ku ripoti habari bila kutupa maoni au misimamo yao
  je wanaifanya hiyo?
   
 5. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Toka nilivyomsikia maneno ya Neville pale jangwani nikajua Tanzania waandishi kwishney,kila mmoja anaangalia
  maslahi.Oh pole Kubenea bila shaka umepata jibu uko na nani kusimamia kweli.wengi ni wanafiki heri Mwangosi
  angebaki.
   
 6. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Si kweli. Mwandishi siku zote ni kama hakimu. Anapaswa kuwa neutral kwani tuna-assume kuwa ukweli hauna upande mmoja. Kwa mfano, unapoongelea ufisadi wa mtu fulani, lazima ujiridhishe kwa kusikiliza pande mbili. Lwaitama ametolea mfano waandishi wawili anaowaona wa maana kuliko wengine ambao ni marehemu Mwangosi kutokana na kufikwa na mauti akiwa kazini na Kubenea kutokana na kumwagiwa tindikali. Hivi si vigezo vya kisomi. Kwanini hataki kuangalia upande wa pili kwa mfano kuhusiana na Kubenea kuwa kulikuwa na tuhuma ambazo hakukanusha kuwa alimwagiwa tindikali na mtu aliyekuwa akimchukulia mke? Uandishi una misingi yake na misingi hii haitegemei welewa au mawazo ya Lwaitama. Naona anaitwa mhadhiri mstaafu na si profesa. Heri angejiendeleza angalau akafikia sifa ya kuwa prof. Kimsingi, Lwaitama anataka kuogelea kwenye bahari asiyoijua kwa kutumia usomi na umaarufu wake. Mambo hayaendi hivyo. Anachosema ni kinyume na ethics za uandishi. Kwa vile amestaafu, basi angechukua muda lau kusoma hata cheti cha uandishi agundue alipochemsha kwa kulaani waandishi wote bila kujua ethics za taaluma yao.
   
 7. Root

  Root JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,243
  Likes Received: 12,964
  Trophy Points: 280
  wana familia zao
   
Loading...