Mwandishi wa Gazeti la Majira ajiapiza ailaani CHADEMA

Mchaka Mchaka

JF-Expert Member
Jul 20, 2010
4,517
1,399
Naheshimu sana siasa za ushindani...hasa ushindani wa hoja. Nilishtuka sana kusikia yale wana CHADEMA waliyoyafanya kwa Mkuu wa Wilaya. Ni kitendo kibaya sana, na hasa ni picha mbaya sana kwa wale wapenda demokrasia ya ushindani. Hili ni kosa la jinai na waliohusika wote wanapaswa kushitakiwa bila kujali ni wafuasi wa CHADEMA au la. Kiungwana nilitegemea viongozi wa CHADEMA kuomba radhi kwa yale yaliyofanywa na wafuasi wao lakini kwa kuendelea kuwatetea wanaudhilishia umma wa
Ulijiunga ili uwe unaandika uharo au? Hebu kuwa na adabu basi? Changia ktu inayoeleweka acha ushabiki wa kirambuza.

Mbopo

JF-Expert Member
Jan 29, 2008
2,532
410
Gladness umekata jongoo kwa meno kwa kusema ukweli wa mambo na jamaa wanatapatapa sasa na kurusha kila aina ya matusi. Imekula kwao.

Aug 15, 2011
39
3
ni vizuri mkasoma alama za nyakati usiangalie hivyo vijisenti ulivyopewa hapo igunga angalia na kesho nani atasoma gazeti lako watz wa sasa tumesha waelewa nyie waandishi mna njaa kali sana ndiyo maana mnatumiwa na ccm ya mafisadi

Mwamikili

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
417
136
Mwandishi kazungumza ukweli kabisa.Kama uko mpinzan ukikosea nawe ukubali kukosolewa.Watz hawapaswi kusamehe upuuzi wa CDM wa kujichukulia sheria mkononi hasa vijana wa kiume kumshambulia na kumkamata mama wa kike.Chama cha siasa tangu lini kikawa na makamanda?,hapo mwandishi ndio anasema CDM mnakoelekea ni kubaya.Kumvua mama hijabu mmedhihirisha kuwa padre anachuki na uislam na waislam hatutawasamehe kamwe labda mtuombe radhi.

hahaaaaa mlidhani ccm itawaletea mahaka ya kadhi bora padre atawaletea hiyo mahakama amia chadema!!

Apr 11, 2011
14
5
Chama cha Magamba yaani Chukua Chako Mapema yaani Chama cha Mafisadi yaani Chama cha Mapacha watatu yaani Chama cha Maraha yaani Chama cha Matanuzi hapa Tanzania kinajulikana kama CCM hakina jipya kwa kuboresha maisha ya mtanzania ila ni kuwatumia waandishi masaburi kuandika habari ya kuafurahisha viongozi wa Magamba. Tunaamini hata Libya, Misiri, Iraq walikuwepo waandishi wa aina hiyo lakini walishindwa na propaganda zinazoegemea vyama vinavyojiita tawala. Ubabe na uhuni uko kwa viongozi wa magamba ambao wanaleta usanii kwa mtaji wa umaskini. Kama CCM wangekuwa wamefanya mambo mazuri wasingehangaika kuwaita hata wafu wa siasa kwenda kuwasaidia kampeni Igunga kama vile Kangi Mbunge wa Mwibara na jirani yake Wassira, Lusinde amabaye ana mtindio wa ubongo, Komba mlafi na Mwiguru mpenda wake za watu. IGUNGA MFUNUENI KAFUMU ILI KASHINDYE ASHINDE.

Kwaroz

Member
Aug 30, 2009
55
10
CHADEMA kwa hili mmechemka

Na Gladness Mboma

ALHAMISI ya wiki iliyopita wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walimkamata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa

madai kuwa walimkuta akifanya kikao na viongozi wa vijiji na kata ndani ya ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Isakamaliwa.

Kwanza kabisa kwa mtazamo wangu CHADEMA walichofanya ni makosa lisha ya kwamba walimdhalilisha kiongozi wa wananchi kwa kumvuta huku na huko huku wakitambua wazi kwamba kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Kosa ambalo ama hakika bila ushabiki wowote wahusika wote wanapaswa kushtakiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.

Ni hoji kwanza, hivi hawa wahuni wanaojiita makomandoo wa CHADEMA wameenda Igunga kwa misingi ya kumnadi mgombea wao ama kumdhalilisha kiongozi aliyewekwa madarakani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Awali nilikuwa ninawakubali CHADEMA kutokana na sera zao za kuleta maendeleo lakini kwa uhuni huu uliofanywa na wanachama hao Igunga katu siwezi kusita kutamka kwamba wakipata nafasi ya kutawala nchi hii awachelewi kuwanyanyasa Watanzania kijinsia.

Tuzingatie kwamba, Bi. Kimario ni kiongozi wa nchi hawakustahili kumdhalilisha kiasi hicho, tena kibaya zaidi wanaume ndio waliohusika kumvuta mama huyo huku na huko kama mwizi.

Haiwezekani hizi ni vurugu ambazo zinatakiwa kupigwa vita na kukemewa kwa nguvu zote ina maana kiongozi ana mipaka ya kufanya mikutano?

Huyu ni kiongozi ana haki ya kufanya kikao mahali popote muda wowote na wananchi wake bila kubuguziwa ili mradi asivunje sheria.

Ina maana wakati huu kampeni za uchaguzi mdogo unaoendelea Igunga kiongozi yoyote wa serikali hatakiwa kufanya kikao na wananchi wake kwa kuhofia kuwa anapanga njama za ushindi wa chama fulani.

CHADEMA sasa mnakoelekea ni kubaya mlikuwa mnakwenda vizuri sasa vurugu zenu na ubabe wenu ndio utakaowakosesha kura na wala si vinginevyo.

Kwani mkifanya siasa na kampeni za ustaarabu hamtaonekana ndani ya jamii ama hadi kila siku muwe na jambo jipya linaloonesha udhalilishaji kwa ili nidhiriki kutamka kwamba wapumbavu siku zote huwa wanajitwalia makaa ya moto wenyewe hivyo siwafichi kwa stahili hii mnajiangusha wenyewe na mnajiua wenyewe.

Vurugu hazipendezi hata kidogo, huyu Mkuu wa Wilaya ana haki ya kufanya mkutano au kikao na viongozi wake kwa sababu kwa ni haki yake ya msingi ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Katika suala hili hakuna ubishi ni lazima mchukuliwe hatua, watu waliomkamata na kumdhalilisha ni lazima sheria ichukue mkondo wake huu ni ukosefu wa nidhamu.

Hii ni hatari kwa maana hiyo kiongozi yoyote wa serikali wa Wilaya ya Igunga asifanye chochote kwa kuhofia vyama vya upinzani, jamani tuacha mawazo mgando huu ni uhuni kama siyo ujinga katika vichwa vya watu walioelimika.

Hata kama huyo mama alikwenda kinyume, lakini hakustahili kufanyiwa kitendo hicho hata kidogo ni udhalilishaji.

nadhani mwandishi hana kumbukumbu vizuri siku za nyuma kuna mbunge wa CUF alikuwa anazungumza na wananchi wake katika jimbo la Tabora na aliwekwa mahabusu kwa siku nane sasa naona hapa ndugu mwandishi anaeleza mpaka povu kumtoka bila kuwa na kumbukumbu sawa. Au alichofanyiwa huyo mbunge ni sawa? Maana kwa mkuu wa wilaya ni sawa lakini kwa mbunge si sawa kwaninu? Mbunge kachaguliwa na wananchi na mkuu wa wilaya kachaguliwa na raisi. Nadhani kuna haja ya kuacha sheria ijitafsiri yenyewe na si kwa shinikizo la watu wachache.

Apr 11, 2011
14
5
Kabla mwandishi wa gazeti la majira hajailaani CDM sote wapinga Magamba Tanzania tumlaani huyu mwandishi masaburi kwani ana zero ya form four akapelekwa kusoma chuo fulani kwa ushawishi wa magamba leo analipa fadhila. Tumhurumie kesho yake itakuaje baada ya Chama cha Matanuzi aka Mwiguru na wake za watu Igunga aka Lusinde mtindio wa ubongo aka Wassira mwenye ugonjwa wa kusinzia hata chooni aka Kangi wa Mwibara kibaraka wa Wassira na wengineo wengi

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Sep 8, 2010
1,017
256
''To every action there is an equal and opposite reaction'' Makamanda wa Chadema wanafikia hapo baada ya CCM kutuimia watumishi wa Serikali kwa maanufaa yao. Mkuu wa Wilaya halipwi na chama cha CCM, anlipwa na serikali anapaswa kuhudumia wananchi wote kwa haki bila kificho. Mkuu wa wilaya anapo fanya shughuli za kificho kikisaidia chama kimoja kupata ushindi ni uwizi wa rasilimali za wote kwa manufaa ya wachache. Mkuu wa wilaya kuondoka mwenyewe bila hata msaidizi na kujichimbia na watendaji wengine wakati Chama kingine kinafanya mkutano wa kampeni sehemu hiyo ni hujuma. CCM iache kuhodhi vyombo vya dola ili vifanye kazi kwa manufaa ya watanzania wote Hapo ndipo AMANI itatamalaki.

Lakini huyu mwandihi alipaswa kuandika makala hiii mwakajana, wakati Robert Kisena alimpiga mtama na kumwangusha chini OCD akiwa kituoni ndani ya sare za Polisi. Mbona hatukusikia mkiaandika mtemi Kisena afunguliwe mashitaka. Na hata RPC aliposema hilo ni swala binafsi hakuana aliona hilo ni tendo la udhililishaji si tu wa OCD bali hata kwa dola nzima.Au kwa kuwa OCD ni mwanume hivyo hadhaliliki? Kwa hiyo mwandishi yoyote kama huyu wa Majira anaye bwatuka kwa sababu tukio limefanywa na Chadema na likifanywa na CCM ananyamaza ni KABURU tu, yaani ni Mbaguzi hafai kuwa katika mhumili wa nne wa nchi hii.

matungusha

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
594
126
me
CHADEMA kwa hili mmechemkaNa Gladness Mboma

ALHAMISI ya wiki iliyopita wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walimkamata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa
madai kuwa walimkuta akifanya kikao na viongozi wa vijiji na kata ndani ya ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Isakamaliwa.

Kwanza kabisa kwa mtazamo wangu CHADEMA walichofanya ni makosa lisha ya kwamba walimdhalilisha kiongozi wa wananchi kwa kumvuta huku na huko huku wakitambua wazi kwamba kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Kosa ambalo ama hakika bila ushabiki wowote wahusika wote wanapaswa kushtakiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.

Ni hoji kwanza, hivi hawa wahuni wanaojiita makomandoo wa CHADEMA wameenda Igunga kwa misingi ya kumnadi mgombea wao ama kumdhalilisha kiongozi aliyewekwa madarakani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Awali nilikuwa ninawakubali CHADEMA kutokana na sera zao za kuleta maendeleo lakini kwa uhuni huu uliofanywa na wanachama hao Igunga katu siwezi kusita kutamka kwamba wakipata nafasi ya kutawala nchi hii awachelewi kuwanyanyasa Watanzania kijinsia.

Tuzingatie kwamba, Bi. Kimario ni kiongozi wa nchi hawakustahili kumdhalilisha kiasi hicho, tena kibaya zaidi wanaume ndio waliohusika kumvuta mama huyo huku na huko kama mwizi.

Haiwezekani hizi ni vurugu ambazo zinatakiwa kupigwa vita na kukemewa kwa nguvu zote ina maana kiongozi ana mipaka ya kufanya mikutano?

Huyu ni kiongozi ana haki ya kufanya kikao mahali popote muda wowote na wananchi wake bila kubuguziwa ili mradi asivunje sheria.

Ina maana wakati huu kampeni za uchaguzi mdogo unaoendelea Igunga kiongozi yoyote wa serikali hatakiwa kufanya kikao na wananchi wake kwa kuhofia kuwa anapanga njama za ushindi wa chama fulani.

CHADEMA sasa mnakoelekea ni kubaya mlikuwa mnakwenda vizuri sasa vurugu zenu na ubabe wenu ndio utakaowakosesha kura na wala si vinginevyo.

Kwani mkifanya siasa na kampeni za ustaarabu hamtaonekana ndani ya jamii ama hadi kila siku muwe na jambo jipya linaloonesha udhalilishaji kwa ili nidhiriki kutamka kwamba wapumbavu siku zote huwa wanajitwalia makaa ya moto wenyewe hivyo siwafichi kwa stahili hii mnajiangusha wenyewe na mnajiua wenyewe.

Vurugu hazipendezi hata kidogo, huyu Mkuu wa Wilaya ana haki ya kufanya mkutano au kikao na viongozi wake kwa sababu kwa ni haki yake ya msingi ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Katika suala hili hakuna ubishi ni lazima mchukuliwe hatua, watu waliomkamata na kumdhalilisha ni lazima sheria ichukue mkondo wake huu ni ukosefu wa nidhamu.

Hii ni hatari kwa maana hiyo kiongozi yoyote wa serikali wa Wilaya ya Igunga asifanye chochote kwa kuhofia vyama vya upinzani, jamani tuacha mawazo mgando huu ni uhuni kama siyo ujinga katika vichwa vya watu walioelimika.

Hata kama huyo mama alikwenda kinyume, lakini hakustahili kufanyiwa kitendo hicho hata kidogo ni udhalilishaji.

Hapo kwenye red je mkuu wa wilaya ni kiongozi wa wananchi au kada wa ccm? to me huyu ni mteule wa Jk na ccm yake na wala sio kiongozi wa wananchi!!! viongozi wa wananchi ni hao wabunge walokamatwa coz wamechaguliwa na wananchi ni sio chaguo la raisi na marafikim zake...

Ulimakafu

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
26,926
7,980
Waandishi wengi walishaonwa na Nape kana miezi 2 iliyopita wakati akitembelea vyombo vya habari ikiwemo Majira.Mie binafsi sishangai.

wakuwaza

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
316
79
Masahihisho kwa wino mwekundu

CHADEMA kwa hili mmechemkaNa Gladness Mboma

ALHAMISI ya wiki iliyopita wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walimkamata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa madai kuwa walimkuta akifanya kikao na viongozi wa vijiji na kata ndani ya ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Isakamaliwa.

Sina maneno na utangulizi wake, lakini ni kweli Fatma Kimario alikutwa akifanya vikao, na yeye mwenyewe alikiri.

Kwanza kabisa kwa mtazamo wangu CHADEMA walichofanya ni makosa lisha ya kwamba walimdhalilisha kiongozi wa wananchi kwa kumvuta huku na huko huku wakitambua wazi kwamba kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Hukukosea kutanguliza "kwa mtazamo" wako. Lakini ulijuaje walichofanya ni kosa la jinai? Tupe kifungu cha sheria. Haitoshi tu kusema kosa la jinai, fafanua na utupe marejeo. Hata hivyo, wewe siyo mahakama na unajua kesi iko mahakamani. Hata kama ungekuwa mahakama, kwanini usingewasikiliza kwanza watuhumiwa kabla ya kuwahukumu? Unahukumuje kesi ambayo hujaisikiliza?

Kosa ambalo ama hakika bila ushabiki wowote wahusika wote wanapaswa kushtakiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.

"Wahusika wote wanapaswa kushtakiwa." Hapo umenena. Lakini kwanini ulihukumu kwanza kabla ya kushitaki? Unamhukumuje mtu ndipo baadaye umshitaki?

Ni hoji kwanza, hivi hawa wahuni wanaojiita makomandoo wa CHADEMA wameenda Igunga kwa misingi ya kumnadi mgombea wao ama kumdhalilisha kiongozi aliyewekwa madarakani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Wahuni wanaojiita makomandoo wa CHADEMA." Kwanza una ushahidi gani kuwa ni wahuni? Uliwasikiaje wakijiita 'makomandoo wa CHADEMA'? Unawezaje ukathibitisha madai yako? Kama mahakama isipowatia hatiani wakati wewe umeshawatia uko tayari kubeba mzigo wa lawama? Wakija wakilidai gazeti lako fidia ya kuchafuliwa majina yao kwa gazeti kukuruhusu kuwaita wahuni mhalifu atakuwa nani? Kuna nguzo za uandishi wa habari. Hapa hukutumia hata moja, hususan ile ya msingi inayowataka waandishi waandike pande zote, siyo upande mmoja au pande mbili tu, bali pande zote, yaani balanced news story. Kama wewe ni mwandishi makini kwanini hukufanya hivyo? Mwandishi wa kweli hawezi kufanya dhambi kubwa namna hiyo kiuandishi.

Awali nilikuwa ninawakubali CHADEMA kutokana na sera zao za kuleta maendeleo lakini kwa uhuni huu uliofanywa na wanachama hao Igunga katu siwezi kusita kutamka kwamba wakipata nafasi ya kutawala nchi hii awachelewi kuwanyanyasa Watanzania kijinsia.

Kwanza ulikuwa unawakubali CHADEMA, halafu ikawaje? Uhuni wao ukabadili itikadi yako? Una ushahidi gani unaoweza kuufikisha mahakamani kuwa waliofanya hivyo ni CHADEMA? Unawezaje kuithibitishia mahakama kuwa CHADEMA kama chama ndiyo iliyofanya hivyo? Umejuaje wakipewa nafasi ya kutawala nchi watawanyanyasa Watanzania kijinsia? Kilichotokea Igunga, kama kweli ni hivyo ndivyo, kilikuwa ni unyanyasaji wa kijinsia? Alikamatwa akiendesha mkutano wakati CHADEMA ikifanya mkutano wa kampeni, jambo ambalo ni kosa kisheria, je, DC huyo angekuwa mwanamume yasingemfika yaliyomfika Fatma? Huo ndio unaouita unyanyasaji wa kijinsia?

Tuzingatie kwamba, Bi. Kimario ni kiongozi wa nchi hawakustahili kumdhalilisha kiasi hicho, tena kibaya zaidi wanaume ndio waliohusika kumvuta mama huyo huku na huko kama mwizi.

Hapa nakubaliana na wewe. Kiongozi wa wananchi anapaswa kuheshimiwa. Hapaswi kudhalilishwa. Lakini namna gani akikutwa anatenda kosa? Asikamatwe? Uhalifu ni uhalifu tu. Namna gani ingekuwa aliingia kibaka mwanamke kupora ofisi za DC na kisha hao unaowaita wahuni wanaojiita makomandoo wa CHADEMA wakaingia kumkamata? Hapo ungeuita unyanyasaji wa kijinsia?

Haiwezekani hizi ni vurugu ambazo zinatakiwa kupigwa vita na kukemewa kwa nguvu zote ina maana kiongozi ana mipaka ya kufanya mikutano?

Swali hili ulipaswa kuanza kuliuliza kabla hujakimbilia kumtetea DC. Pengine ungepata jibu lake na maelezo yake hungeandika uliyoandika hapa. Ungeanza kuuliza swali hilo ndipo tungeona umakini wa uandishi wako.

Huyu ni kiongozi ana haki ya kufanya kikao mahali popote muda wowote na wananchi wake bila kubuguziwa (kubughudhiwa) ili mradi asivunje sheria.

Hii inanipa wasiwasi zaidi. Kiongozi ana haki ya kufanya mkutano popote na muda wowote? Hicho ni kifungu gani cha katiba? Labda wasaidie wengine wakuelewe. Hilo unalosema limeandikwa wapi? Au tuambie ulikolipata. Hili lingine ulilosema "bila kubuguziwa (nadhani ulitaka kumaanisha kubughudhiwa) hujasema nalo umelipata wapi. Kwa hiyo kama anaweza "kufanya mkutano popote na muda wowote" unataka kumaanisha hata msikitini, kanisani na usiku wa manane au hata wakati CHADEMA nao wanafanya mkutano? Lakini lile ulilosema "ili mradi asivunje sheria" ndipo ulipochanganya mambo. Ulijuaje hakuvunja sheria hata kama anayo haki ya kufanya mkutano popote na muda wowote?

Ina maana wakati huu kampeni za uchaguzi mdogo unaoendelea Igunga kiongozi yoyote wa serikali hatakiwa kufanya kikao na wananchi wake kwa kuhofia kuwa anapanga njama za ushindi wa chama fulani.

Hili nalo halipaswi kuulizwa na mwandishi makini. Mwandishi yeyote alipaswa alijue hilo. Kazi kubwa ya mwandishi ni kuchunguza. Kama hujachunguza huna haki ya kuandika.

CHADEMA sasa mnakoelekea ni kubaya mlikuwa mnakwenda vizuri sasa vurugu zenu na ubabe wenu ndio utakaowakosesha kura na wala si vinginevyo.

Kubaya ni wapi? Tufafanulie. Lakini kama "vurugu" na "ubabe" vitawanyima kura CHADEMA ni suala la kusubiri na kutazama.

Kwani mkifanya siasa na kampeni za ustaarabu hamtaonekana ndani ya jamii ama hadi kila siku muwe na jambo jipya linaloonesha udhalilishaji kwa ili nidhiriki kutamka kwamba wapumbavu siku zote huwa wanajitwalia makaa ya moto wenyewe hivyo siwafichi kwa stahili hii mnajiangusha wenyewe na mnajiua wenyewe.

"Siasa na kampeni za ustaarabu" ni zipi? Kufanya vikao vya kula njama ya kuiba kura ndizo kampeni za ustaarabu? Kukiuka taratibu kama alivyofanya DC ndio ustaarabu? CCM kuandikisha shahada za wapiga kura ndizo unazoziita kampeni za ustaarabu? Au kuna jambo ulilisahau wakati ukiandika?

Vurugu hazipendezi hata kidogo, huyu Mkuu wa Wilaya ana haki ya kufanya mkutano au kikao na viongozi wake kwa sababu kwa ni haki yake ya msingi ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Ni kweli vurugu hazipendezi, nakubaliana na wewe. Lakini kama walifanya vurugu ulichunguza ukajua sababu ya vurugu yao?

Katika suala hili hakuna ubishi ni lazima mchukuliwe hatua, watu waliomkamata na kumdhalilisha ni lazima sheria ichukue mkondo wake huu ni ukosefu wa nidhamu.

Hii ni hatari kwa maana hiyo kiongozi yoyote (yeyote) wa serikali wa Wilaya ya Igunga asifanye chochote kwa kuhofia vyama vya upinzani, jamani tuacha mawazo mgando huu ni uhuni kama siyo ujinga katika vichwa vya watu walioelimika.

Natahadharisha maneno hayo (huu ni uhuni kama siyo ujinga). Itakapothibitika mahakamani kuwa siyo wahuni, huenda wakalijia gazeti lenu na kuwataka muwathibitishie. Hapo ndipo mtakaposafisha 'ujinga' wao na kuwaona ni wenye akili. Mhariri wa gazeti hilo naye hawezi kuepuka hilo ikiwa litajitokeza.

Hata kama huyo mama alikwenda kinyume, lakini hakustahili kufanyiwa kitendo hicho hata kidogo ni udhalilishaji.

Hapa nakubaliana na wewe kabisaaaaa. Bora sentensi hiyo ungeiweka mwanzoni kabisa. Kwa upande mwingine, yeyote aliyehusika kumkamata mama DC alifanya makosa, hata kama alikuwa mhalifu. Tunajua kazi hiyo inafanywa na polisi. Lakini kama uhalifu unafanyika wakati polisi haipo uachwe tu uendelee? Si ndiyo maana vibaka wanachomwa moto? Tunawaheshimu sana waandishi kwa sababu wanatupasha habari, lakini chonde chonde tuandikieni yanayopaswa kuandikwa, siyo yale yaliyojaza mioyo yenu. Huo sio uandishi. Inavyoelekea ni ama makala hiyo haikupita kwa mhariri, au mhariri huyo anamwamini sana mwandishi wake.

kweleakwelea

JF-Expert Member
Nov 29, 2010
3,064
1,528
chadema kwa hili mmechemkana gladness mboma

alhamisi ya wiki iliyopita wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) walimkamata mkuu wa wilaya ya igunga, bi. Fatma kimario kwa
madai kuwa walimkuta akifanya kikao na viongozi wa vijiji na kata ndani ya ofisi ya mtendaji wa kata ya isakamaliwa.

Kwanza kabisa kwa mtazamo wangu chadema walichofanya ni makosa lisha ya kwamba walimdhalilisha kiongozi wa wananchi kwa kumvuta huku na huko huku wakitambua wazi kwamba kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Kosa ambalo ama hakika bila ushabiki wowote wahusika wote wanapaswa kushtakiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.

Ni hoji kwanza, hivi hawa wahuni wanaojiita makomandoo wa chadema wameenda igunga kwa misingi ya kumnadi mgombea wao ama kumdhalilisha kiongozi aliyewekwa madarakani na rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania.

Awali nilikuwa ninawakubali chadema kutokana na sera zao za kuleta maendeleo lakini kwa uhuni huu uliofanywa na wanachama hao igunga katu siwezi kusita kutamka kwamba wakipata nafasi ya kutawala nchi hii awachelewi kuwanyanyasa watanzania kijinsia.

Tuzingatie kwamba, bi. Kimario ni kiongozi wa nchi hawakustahili kumdhalilisha kiasi hicho, tena kibaya zaidi wanaume ndio waliohusika kumvuta mama huyo huku na huko kama mwizi.

Haiwezekani hizi ni vurugu ambazo zinatakiwa kupigwa vita na kukemewa kwa nguvu zote ina maana kiongozi ana mipaka ya kufanya mikutano?

Huyu ni kiongozi ana haki ya kufanya kikao mahali popote muda wowote na wananchi wake bila kubuguziwa ili mradi asivunje sheria.

Ina maana wakati huu kampeni za uchaguzi mdogo unaoendelea igunga kiongozi yoyote wa serikali hatakiwa kufanya kikao na wananchi wake kwa kuhofia kuwa anapanga njama za ushindi wa chama fulani.

Chadema sasa mnakoelekea ni kubaya mlikuwa mnakwenda vizuri sasa vurugu zenu na ubabe wenu ndio utakaowakosesha kura na wala si vinginevyo.

Kwani mkifanya siasa na kampeni za ustaarabu hamtaonekana ndani ya jamii ama hadi kila siku muwe na jambo jipya linaloonesha udhalilishaji kwa ili nidhiriki kutamka kwamba wapumbavu siku zote huwa wanajitwalia makaa ya moto wenyewe hivyo siwafichi kwa stahili hii mnajiangusha wenyewe na mnajiua wenyewe.

Vurugu hazipendezi hata kidogo, huyu mkuu wa wilaya ana haki ya kufanya mkutano au kikao na viongozi wake kwa sababu kwa ni haki yake ya msingi ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Katika suala hili hakuna ubishi ni lazima mchukuliwe hatua, watu waliomkamata na kumdhalilisha ni lazima sheria ichukue mkondo wake huu ni ukosefu wa nidhamu.

Hii ni hatari kwa maana hiyo kiongozi yoyote wa serikali wa wilaya ya igunga asifanye chochote kwa kuhofia vyama vya upinzani, jamani tuacha mawazo mgando huu ni uhuni kama siyo ujinga katika vichwa vya watu walioelimika.

Hata kama huyo mama alikwenda kinyume, lakini hakustahili kufanyiwa kitendo hicho hata kidogo ni udhalilishaji.

ungalijua tuko mbioni kufuta cheo cha mkuu wa wilaya na mkoa!!! Hakina chochote zaidi ya kuwaumiza wananchi!

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,185
2,300
Huyu mama anadhalilisha taaluma yake kwani anaandika mambo ambayo hajafanyia utafiti kabisa. nasema hivi kwa sababu habari hii imeihukumu CDM right away kana kwamba huyo mama alikuwa tu amejikalia akavamiwa. Mwandishi ana lengo la kuichafua CDM ili anufaike na vijipesa vya Nape ila ajue baada ya uchaguzi atabaki tu kuwa gunia la kujifutia miguu la CCM.

shaluu

Member
Jul 17, 2011
11
1
Msibabaishwe na gazeti la Majira kwani hata Igunga halifiki na wapiga kura wa Igunga kamwe hawatashawishiwa na Majira wanona wenyewe madudu ya CCM ambayo hata Rost Ham aliyaona, wasaliti wapo wengi.....aluta continyuuu

Tilu

Member
Sep 20, 2011
5
1
Jamani tuache upuuzi kwenye mambo ya msingi! Nchi inaendeshwa kwa mjibu wa sheria. Mkuu wa wilaya au kiongozi yeyote hayuko juu ya sheria. Yule mama alikosea ndo maana hata yeye alikubali kutii alipokamatwa. Rais wa Wilaya anaendesha kikao bila hata ulinzi? Mbona vyombo vingine vya Wilaya havikuwa na taarifa ya kikao chake? Hebu tuache siasa za umaamuma ambazo ndo zimetufikisha hapa tulipo miaka 50 ya Uhuru watoto wetu wanasomea mchangani halafu sisi tunazungumza habari ya hijabu? Hijabu tunaiona bora kuliko future ya maisha yetu? Jamani tutafakari mambo haya! Tumelishwa mawazo na fikra mbovu sana na watawala wetu ili waendelee kujinufaisha kupitia ujinga wetu!

4 Reactions
Reply
Top Bottom