Mwandishi wa Gazeti la Majira ajiapiza ailaani CHADEMA

Nampa hongera dc kwa kupata alichokitararajia, alifuata fedheha amefedheheshwa, heshima haiombwi au kulazimishwa usipojiheshimu utapata yaliyompata fatma kimario. mwandishi wa habari msameheni anachumia tumbo.
 
Unamaanisha kiongozi aliyewekwa na rais anayo haki ya kuvunja taratibu na asichukuliwe sheria, Kumkamata mhalifu ni wajibu wa mtu yeyote pale pasipo kuwa na askari. Mama huyo ameiuka taratibu za uchaguzi

Vurugu unazozisema ni wewe ni hizo za DC kufanya vikao kinyume na taratibu za uchaguzi amekiri kukutwa na barua za watu kuomba kazi za usimamizi wa uchaguzi anahusika vipi na uchaguzi? HIZO NDIO VURUGU AMBAZO WOTE TUNAPASWA KUZIKEMEA KWA NGUVU ZOTE!

Mama huyo alikiuka kanuni(MOA) ya uchaguzi na anapaswa kuwajibishwa kwa hilo

Yaani kwa tafsiri yako wewe kumkamata unayemuita mhalifu ni kumdhalilisha na hata kumvua nguo na kutishia kumbaka? Hiyo ni sheria kwa tafsiri ya nani? Kumbuka CUF ilipoteza umaarufu kutokana na vitendo vya wahuni wachache kama hao walioko ndani ya Chadema ambao kwa kukosa utashi na akili timamu, mnawapachika majina ya makamanda!
 
Mh. Magdalena Sakaya aliburutwa na polisi wa kiume na kulazwa chumba kimoja na wahalifu wakiume. Huyo kada wa ccm alikuwa na piga kampeni wakamwadabisha kidogo tu wanalalama. "MKUKI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU."
 
Yaani kwa tafsiri yako wewe kumkamata unayemuita mhalifu ni kumdhalilisha na hata kumvua nguo na kutishia kumbaka? Hiyo ni sheria kwa tafsiri ya nani? Kumbuka CUF ilipoteza umaarufu kutokana na vitendo vya wahuni wachache kama hao walioko ndani ya Chadema ambao kwa kukosa utashi na akili timamu, mnawapachika majina ya makamanda!

Hivi ukiwa mfanyakazi wa serikali ya bongo shurti ushabikie CCM?
 
Another simple crap...

Mkuu pamoja na simple crap lakini nchi haiwezi kuendeshwa na mabaunsa wanaoenda kuwadhalilisha watu. Suala la kuthubutu kumdhalilisha mkuu wa Wilaya ambaye ni mwakilishi wa Rais wilayani si suala la kushangilia hata kidogo. Watu wametukana weee wameona sasa haitoshi wameanza kuwadhalilisha viongozi. Katika hili kwa hakika serikali inatakiwa iwe kali manake kama wameanza na mkuu wa wilaya wakichekewa watasonga mbele kwa mkuu wa mkoa kisha kwa Rais!! Walioshiriki wanatakiwa wapewe adhabu kali ili iwe fundisho kwao wenyewe na wenzao wanaofikiria kufanya hivyo. Mabaunsa tumewazoe kuwaona wakilinda kwenye kumbe za starehe zinazohudhuriwa na walevi sasa kwenye mkutano wa mkuu wa wilaya wanatafuta nini kama si shari. Watu waliliona hili mapema ndio maana wakaandika kwamba "Vurugu zenu pelekeni huko Arusha"
 
Call a spade a spade and no mincing words. Chama hiki ambacho awali kilibeba matumaini ya sisi wote, ghafla kimeamua kujiua kama ilivyofanya CUF kwa kukumbatia vitendo vya kihuni na vya ukatili dhidi ya wananchi.
 
mh. Magdalena sakaya aliburutwa na polisi wa kiume na kulazwa chumba kimoja na wahalifu wakiume. Huyo kada wa ccm alikuwa na piga kampeni wakamwadabisha kidogo tu wanalalama. "mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu."
acha uongo
 
mwandishi huyu ni CCM so hakuna atakachoandika tofauti na mambo ya ccm mazuri na chadema mabaya....

ila ukweli ni ukweli CCM siku zao zimefika ukingoni....
 
Call a spade a spade and no mincing words. Chama hiki ambacho awali kilibeba matumaini ya sisi wote, ghafla kimeamua kujiua kama ilivyofanya CUF kwa kukumbatia vitendo vya kihuni na vya ukatili dhidi ya wananchi.
 
CHADEMA kwa hili mmechemka



Na Gladness Mboma


ALHAMISI ya wiki iliyopita wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walimkamata Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa
madai kuwa walimkuta akifanya kikao na viongozi wa vijiji na kata ndani ya ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Isakamaliwa.

Kwanza kabisa kwa mtazamo wangu CHADEMA walichofanya ni makosa lisha ya kwamba walimdhalilisha kiongozi wa wananchi kwa kumvuta huku na huko huku wakitambua wazi kwamba kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Kosa ambalo ama hakika bila ushabiki wowote wahusika wote wanapaswa kushtakiwa na kuchukuliwa hatua za kisheria haraka iwezekanavyo.

Ni hoji kwanza, hivi hawa wahuni wanaojiita makomandoo wa CHADEMA wameenda Igunga kwa misingi ya kumnadi mgombea wao ama kumdhalilisha kiongozi aliyewekwa madarakani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Awali nilikuwa ninawakubali CHADEMA kutokana na sera zao za kuleta maendeleo lakini kwa uhuni huu uliofanywa na wanachama hao Igunga katu siwezi kusita kutamka kwamba wakipata nafasi ya kutawala nchi hii awachelewi kuwanyanyasa Watanzania kijinsia.

Tuzingatie kwamba, Bi. Kimario ni kiongozi wa nchi hawakustahili kumdhalilisha kiasi hicho, tena kibaya zaidi wanaume ndio waliohusika kumvuta mama huyo huku na huko kama mwizi.

Haiwezekani hizi ni vurugu ambazo zinatakiwa kupigwa vita na kukemewa kwa nguvu zote ina maana kiongozi ana mipaka ya kufanya mikutano?

Huyu ni kiongozi ana haki ya kufanya kikao mahali popote muda wowote na wananchi wake bila kubuguziwa ili mradi asivunje sheria.

Ina maana wakati huu kampeni za uchaguzi mdogo unaoendelea Igunga kiongozi yoyote wa serikali hatakiwa kufanya kikao na wananchi wake kwa kuhofia kuwa anapanga njama za ushindi wa chama fulani.

CHADEMA sasa mnakoelekea ni kubaya mlikuwa mnakwenda vizuri sasa vurugu zenu na ubabe wenu ndio utakaowakosesha kura na wala si vinginevyo.

Kwani mkifanya siasa na kampeni za ustaarabu hamtaonekana ndani ya jamii ama hadi kila siku muwe na jambo jipya linaloonesha udhalilishaji kwa ili nidhiriki kutamka kwamba wapumbavu siku zote huwa wanajitwalia makaa ya moto wenyewe hivyo siwafichi kwa stahili hii mnajiangusha wenyewe na mnajiua wenyewe.

Vurugu hazipendezi hata kidogo, huyu Mkuu wa Wilaya ana haki ya kufanya mkutano au kikao na viongozi wake kwa sababu kwa ni haki yake ya msingi ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Katika suala hili hakuna ubishi ni lazima mchukuliwe hatua, watu waliomkamata na kumdhalilisha ni lazima sheria ichukue mkondo wake huu ni ukosefu wa nidhamu.

Hii ni hatari kwa maana hiyo kiongozi yoyote wa serikali wa Wilaya ya Igunga asifanye chochote kwa kuhofia vyama vya upinzani, jamani tuacha mawazo mgando huu ni uhuni kama siyo ujinga katika vichwa vya watu walioelimika.

Hata kama huyo mama alikwenda kinyume, lakini hakustahili kufanyiwa kitendo hicho hata kidogo ni udhalilishaji.
Hapana hayo ndio matatizo ya kuwa mkuu wa wilaya huku ukiwa kiongozi wa CCM,sasa huyo mkuu anatumia wdhifa wake wa kiserikali kwa kufanya mambo ya kisiasa ,nia ni kutaka kukipendelea chama chake cha Magamba.Inabidi ufike wakati tutenganishe mfumo wa kuwa kiongozi wa serikali na wakati huo huo kiongozi wa chama tawala
 
Nalipa pongezi gazeti la Majira kwa kuandika habari za ukweli na uhakika.
Ni kweli wahuni wa CDM wanataka kuleta machafuko nchini wananchi wapenda amani hatuwezi kukubaliana na huo upuuzi

Ritz' hv hauoni kuwa Gazeti limefanya mambo ya kipumbafu kwa kujadili jambo lilipo Mahakamani? Hv kama mahakama itathibisha kuwa chadema hawana kesi ya kujibu juu ya huyo mkuu wa wilaya? Gazeti litaiomba msamaha Chadema au? Shenzi zao majira!
 
A man of one book is very dangerous! Tuzisome hata hizi 'hadithi za Kitchen Party'! Then tutaweza kujua ukweli na uongo ni upi!
 
Ukweli nimepitia maoni yenu baadhi na mi naomba niseme kitu kimoja kwanza.Hivi huyu mama ratiba yake ya vikao kwanini iangukie siku ile? na kama alikua na ratiba ya kikao kwa nini asingepewa ulinzi wa kutosha?Kwa mimi nijuavyo Mkuu wa Wilaya anapokuwa na kikao lazima awe na ulinzi kama kikao kipo katika ratiba yake.Lakini sidhani kama alikuwa na wajibu kufanya kikao siku ile kweli kabisa ujue kuna watu kupigwa huwa wanajitakia wenyewe jamani.CCM wamefanya mangapi hatuongei kabisa?Huyu muandishi wa Majira anataka nini?anataka kutuonyesha interest yake hapa au?Kaa fikiria gazeti lako linauza Copy ngapi kwa siku alafu sidhani kama utakuwa unaingilia mjadala kama huu tena.

Tufanye mambo ya msingi na sio kuongelea Chadema tafuta story andika kwa Gazeti lako na sio kuandika vitu vusivyo na msingi hapa ya kule Arusha umesahau?Nani alianzisha utasema ni Chadema au?Fikiria mara mbili.CCM yenyewe ndo inakandamiza wananchi wake.Mhariri kwa kifupi hata uongee vipi hunishwi Ng'oo Cha msingi jua kwamba Chadema inasera nzuri na endelevu.

Huyo mama aendelee kufanya vikao tena bila taratibu aonee cha motoooo.....
 
Back
Top Bottom