'Mwandishi' wa Daily News ambaye pia mtetezi wa mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Mwandishi' wa Daily News ambaye pia mtetezi wa mafisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Aug 31, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,874
  Likes Received: 83,352
  Trophy Points: 280
  Wanaotaka Rais Kikwete akamate mafisadi hawamtakii mema
  Neophitius Kyaruzi
  Daily News; Sunday,August 31, 2008 @09:29

  MAPEMA wiki hii, Rais Jakaya Kikwete alitumia muda mrefu kuhutubia Bunge tofauti kabisa na hotuba zake nyingine tulizozizoea. Urefu wa hotuba hiyo ambayo ilidumu kwa zaidi ya saa tatu, ulitokana na hotuba hiyo kusheheni mada nyingi zilizohitajika kutolewa ufafanuzi na rais mwenyewe.

  Licha ya urefu wa hotuba hiyo, watu wengi waliokuwa wakimsikiliza moja kwa moja kutoka bungeni kupitia luninga au redio hawakuthubutu kuondoka katika vifaa hivyo vya mawasiliano. Hiyo inatokana na ukweli kwamba, wengi wao walikuwa na shauku ya kutaka rais aseme yale waliyokuwa wanataka kuyasikia na si kusikiliza mambo mengine yenye maslahi ya taifa.

  Kwa maana hiyo basi, walisikiliza hotuba hiyo kwa makini wakidhani kuwa muda wa kusikia kile walichokuwa wanahitaji lakini mambo yalikuwa kinyume na matarajio yao. Watu wa aina hii ni wale wanaosikiliza hotuba bila ya kuwa na ‘sober mind.'

  Kwanza kabisa napenda nimpongeze Rais kwa kuweka mada ya EPA mwishoni mwa hotuba yake, kwani kama angeitanguliza, watu wa aina hiyo wasingesikiliza mambo mengine aliyoyazungumza ambayo yanagusa maslahi ya taifa kwa kiasi kikubwa.

  Nasema hivyo kutokana na ukweli kwamba badala ya watu kusikiliza Rais anasema nini kuhusu mikakati ya taifa ya kujikwamua kiuchumi ili kufikia hatua ya maendeleo endelevu, masikio yao yalielekezwa kusika angesema nini kuhusu mafisadi wa EPA.


  Hata hivyo, napenda kuwatahadharisha wale wote wanaodhani kwamba naunga mkono ufisadi kwa kuandika uchambuzi huu, kutokana na ukweli kwamba jinsi walivyomwelewa vibaya rais na mimi wanaweza kunielewa vibaya.

  Kinachoonekana kwa baadhi yetu, ni kupinga usemi usemao ‘subira huvuta heri' na kukumbatia usemi usemao ‘ngoja ngoja huumiza matumbo'. Ni dhahiri kwamba watu wa aina hii hawakufurahishwa na hatua zilizofikiwa na serikali katika kupambana na mafisadi wa EPA.

  Hiyo inatokana na ukweli kwamba baada ya rais kuhitimisha hotuba yake, baadhi ya watu walionekana kuiponda waziwazi kwamba walitarajia kusikia akitaja majina ya mafisadi waliohusika kuhujumu uchumi wa nchi kupitia EPA, pia walitaka kusikia kutoka kwake hatua ambazo angechukua akiwa kama kiongozi mkuu wa nchi.


  Kama tutakumbuka, katika hotuba yake Rais alisema kwamba ingawa anayo mamlaka makubwa kama kiongozi wa nchi hawezi kumchukulia mtu hatua kwa kumuonea, hivyo wale wote wanaodaiwa kuhusika katika ufisadi huo wanapaswa kuchunguzwa na kuhojiwa na ikibainika kwamba walihusika wafikishwe mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

  Kwa upande wangu, nadhani kwamba huo ni uamuzi wa busara kwani kama isingekuwa taarifa tunazozipata kupitia vyombo vya habari, ingetuwia vigumu kujua, japo kwa tetesi, watuhumiwa wa ufisadi wa EPA. Tatizo ni kwamba, baada ya kupata taarifa hizo ambazo wakati mwingine zikiwa zimeandikwa kwa uchochezi, baadhi yetu tumekuwa tukitaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.

  Naamini kwamba kiongozi yeyote mwenye busara hawezi kuendeshwa na utashi wa wananchi wachache, bali atafanya kazi yake kwa kufuata sheria za nchi ili kila mwananchi atendewe haki. Tunapaswa kutambua kwamba hakuna chombo kingine kinachosimamia haki zaidi mahakama, hivyo Rais Kikwete ameiachia mahakama ifanye kazi yake. Huo ndio msingi wa utawala bora! Utawala unaojali mgawanyiko wa kazi za Bunge, Mahakama na Serikali.

  Natambua kwamba wengi hawakufurahishwa na uamuzi huo, lakini tunapaswa kujiuliza kwamba tutakuwa tunalipeleka wapi taifa letu kama Rais akisikia jambo baya kwa mtu fulani na kuamuru akamatwe kesho yake? Huu utakuwa utawala wa sheria au udikteta wa kupindukia?

  Tunapaswa kutambua kuwa ingawa tupo katika mapambano makubwa dhidi ya ufisadi, mapambano hayo tunapaswa kuyaendesha kwa umakini mkubwa, kwani tusipoangalia tunaweza kujikuta tukiliingiza taifa katika hasara mara mbili. Kama alivyosema Rais Kikwete, hakuna si kiongozi wala mwananchi aliye juu ya sheria, hivyo kila uamuzi unapaswa kuchukuliwa kwa kufuata misingi ya sheria.

  Nasema hivyo kutokana na ukweli kwamba baadhi ya watu walishangazwa na kauli za rais pale aliposema kwamba inawezekana kabisa mtu akakurupuka kuwachukulia hatua watuhumiwa wa EPA, halafu mwisho wa siku ikibainika kwamba watu walionewa wakaifungulia mashtaka serikali, jambo ambalo linaweza kuiingizia hasara nyingine serikali.

  Kutokana na ukweli huo, tunapaswa kurejea katika misingi mitatu ya kisosholojia inayofutwa na jamii yeyote iliyostaarabika. Misingi hiyo ni: ‘self control', ambapo mtu anapaswa kujizuia kitu kibaya kutoka rohoni mwake mwenyewe kwa mfano, ya kuuchukia ufisadi kutoka moyoni; ‘formal control', kwa mfano kuuchukia ufisadi kwa kuhofia jamii itamwonaje; ‘Informal control' kwa mfano, kuwachukulia hatua mafisadi kwa kufuata misingi ya sheria, kama alivyofanya Rais Kikwete!
   
Loading...