Mwandishi wa BBC akamatwa kwa kuhoji shule kukosa vyoo Mwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandishi wa BBC akamatwa kwa kuhoji shule kukosa vyoo Mwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by geek, Sep 17, 2010.

 1. g

  geek Member

  #1
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Eric Nampesya, leo Ijumaa asubuhi alikamatwa na kuwekwa mbaroni baada ya kukorofishana na mkurugenzi wa jiji la Mwanza - kisa alienda kufuata reaction kwanini shule nyingi hazina vyoo vya kutosha?

  Nampesya alifanya story iliyo-highlight watoto wa shule jijini Mwanza kujisaidia kwa shida kwasababu shule wanazosoma hazina mashimo ya kutosha ya vyoo. Story ya kwanza ilisikika Alhamisi na ya pili Ijumaa, lakini story hizo zenye kufichua uzembe, zimemponza.

  Baadhi ya matatizo aliyoyaona ni shule tatu zilizo pamoja kuwa na jumla ya wanafunzi 3,680, lakini kuna mashimo ya vyoo 20 tu, kiasi kwamba watoto wanajisaidia kwa kushindwa kusubiri foleni ya kuingia kujisaidia.

  Ingawa Nampesya ameachiwa jioni hii, ameshikiliwa na polisi kwa saa zaidi ya nne. Maelezo zaidi yatafuatia baadaye.
   
 2. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #2
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Duh, kumshika mwandishi sio ufumbuzi wa tatizo sana sana ndo wanajiongezea matatizo kwani mwandishi alikuwa anafanya kazi yake na kupata maelezo ya upande wa pili kwa nini hali iko hivyo, hivyo basi kumtia mbaroni haiwasaidii sana walichotakiwa ni kutoa sababu ya hali hiyo au kukiri uzembe wa viongozi hao kuwahamasisha wananchi kujijengea vyoo mashuleni
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hiyo ndo CCM bana na watendaji wake!!
   
 4. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Duh! Huyo Mkurugenzi wa jiji la Mwanza ndio huyohuyo aliyekuwa amemuengua Hezekia Wenje asigombee ubunge jimbo la Nyamagana (kupitia CHADEMA) kwa kumsingizia kuwa si raia wa Tz, hali iliyomuacha Masha wa CCM awe pekee, kabla ya Tume ya Uchaguzi kutengua maamuzi hayo ya Mkurugenzi huyo (anaitwa Kabwe).
  Na huyohuyo Kabwe kwa wadhifa wake ndiye msimamizi wa uchaguzi majimbo ya Nyamagana na Ilemela. Kazi ipo.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Talk about shooting the messenger!
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Kuna mijitu inaishi zama za mawe. Strategic thinking zero. Unaongezea tatizo la kutokuwa na vyoo tatizo lingine la censorship.

  BBC will have a field day on this dinosauric steam engine of a bureaucrat.
   
 7. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  haya nayo makubwa kweliiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 8. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Huyo Mkurugenzi ni wa ajabu sana,

  Mr. Kabwe that place is my home na nakuambia hivi wewe umekuja tu hapo kwa kuletwa huko Arusha ulishindwa na una scandle za kufa mtu,

  Let me tell u tena kwa machungu sana pale Mkurugenzi anapo taka kujionyesha hajuu umuhimi wa vyooo esp katika mashule esp eneo la mlimani bugando hebu angali mabatini inayo elekea bugando umeji tayarisha vipi kimiundombinu na kukabiliana na watu hao mlimani na kuwawezeshea kuweka mambomba ya maji taka au kuwahamisha hao watu na kutaftiwa viwanja huko kuelekiea Igombe au Igoma ??? Mji unakuwa tena kwa kasi na twahitaji wataaaramu wanaojua nini maana ya kuwa mkurugenzi yaani wewe hupendi kukosolewa na hili ndio tatizo la watanzania hatutaki kukubali weekness zetu na kujifunza yaani unataka kuliendesha jiji ki dectetor???

  JIJI la mwanza lakusanya mapato mengi sana na wingi wa watu unaongezeka kwa kasi na kama huwezi kazi resign wapewe wengine, yaani sielewi kwanini tumekuwa na sela za kuwa na mikoa tungelikuwa na majimbo yani tungekuwajibisha Jana hiyo hiyo maana kinaniuma sana wanafunzi wanajisaidia kwa zamu kweli wewe sijui unakaa Capri-Point au Isamilo na watoto wako wanasoma huko St. Patric Arusha, Ivi unajisikia vipi watoto wa maskini wa kipato cha chini wanawasomesha watoto wao kwa shida ivi Mr. Kabwe ulitembelea hizo shule huko mlimani bugando au unakaa unakula upepo mzuri wa Tilapia-Hotel na samaki satoo tuu.

  Mwandishi wa habari akisema ukweli ni anakuwa adui kabisa wa viongozi ingalikuwa mie sijakulia au kusomea hapo mwanza sawa ila napajua A - Z, mashule yako vile vile kama Nyanza Primary, Nyakabungo,Mirongo,Nyamagana,Makongoro-Mwenge,Kirumba,Kitangiri,Lake Primary,Mabatini hizi shule zote hazina mabadiliko since 1980's upto date kuan alama mmoja niliwahi iweka Nyanza Primary mpaka mwaka jana nikaikuta na dirisha liko vile vile khaaaaa???

  Naomba wano ona maovu wayafunue na ndio maaana hata Mbg. L.Masha alishuku kurudi kugombea Nyamagana kwani fiki walikuwa hawamtaki na ashukuru Ridhwana alienda kubeba jahazi.
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Yaani mpaka leo twaongela matundu ya choo!kumbuka tuko kwa karne ya 21
  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI NA SERIKALI YAKE
   
 10. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Helikopta 3 + ndege 1 = matundu 20 ya choo
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Unashangaa mkuu? Kuna shule moja huko Tanga inaitwa (Bombo Primary), wazazi wataka kuandamana kumfukuza mwalimu mkuu eti anawalazimisha watoto wao kutumia vyoo vya maji badala ya vyoo vya shimo. Kwa kuwa watoto walikuwa wanabanwa kuhakikisha ni visafi.

  Yaani kwenye suala la vyoo nadhani tuko karne ya 10 hivi!
   
 12. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,214
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Yaani watoto 3,680 wanakuwa na matundu 20 tu ya choo? Hiyo ni watoto 184 per tundu. Hayo sasa ndio matokeo ya kutawaliwa na watu wale wale wasioweza kwa miaka 50.

  Fedha alizopokea mzee "Vijisenti" kama hongo wakati wa kununua rada hazingetosha matundu mengi sana? Na zile bilioni 700 ambazo CAG amegundua zimechotwa hazingejenga vyoo shule zote?

  Ndugu zangu: Kama mkiendelea na watu hawa wa CCM mwakani hali haitabadilika. Chagueni viongozi wapya. Kwa vingine tutaendelea kuwa kichekesho duniani.
   
 13. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #13
  Sep 18, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kumkamata, kumweka ndani na kumhoji mwandishi wa BBC, bila ya sababu ya msingi, kwa kuwa tu amefuatilia kukosekana kwa vyoo kwenye shule za msingi - MAHALI POPOTE DUNIANI - ni kutaka ugomvi na vyombo vya habari vya kimataifa. Nadhani DC wa Mwanza hakutumia busara. BBC ina mtandao mkubwa wa mawasiliano duniani. Habari hii itaenea DUNIA NZIMA. Sasa kama tulikuwa hatutaki ijulikane kwamba shule za msingi Tanzania zina tatizo la vyoo, sasa imekuwa wazi kama mchana, jua kali, saa sita! Dunia nzima sasa inajua.

  Lakini kibaya zaidi Tanzania sasa itawekewa nembo mpya; nchi ambayo haipendi uwazi, yenye kuendekeza ukandamizaji kwa vyombo vya habari na wanahabari. Hii ni mbaya, ukifikiria kwamba bado tunawahitaji wafadhili - kutupa misaada? - ambao tumekuwa tukiwadanganya kwamba Tanzania ni nchi inayoheshimu utawala wa sheria, uhuru wa vyombo vya habari na utawala bora.

  Haya yote sasa yatatupwa, kwa tukio moja tu, KUKAMATWA KWA MWANDISHI WA HABARI WA BBC!

  Mola, tuepushie viongozi wapumbavu kama hawa, wenye kutujulisha nyuma kimaendeleo. Alishindwa nini kuwasiliana naye, kumsikiliza, mpaka ampeleke polisi? Polisi wanapelekwa wahalifu, SI waandishi wa habari!

  -> Mwana wa Haki

  Hii ni sababu nyingine inayotutaka tufanye mabadiliko kwenye mfumo wa utawala wa nchi yetu tunayoipenda. Kama unaipenda na kuijali Tanzania, ifikapo 31 Oktoba 2010, CHAGUA CHADEMA!
   
 14. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Shame on JK.

  Anazungumzia kuwa katika miaka mitano ijayo shule zitakuwa zikifundisha kwa njia ya electronic kwa kutumia computer badala ya kusema katika miaka mitano ijayo nitahikikisha kila shule ina vyoo vya kutosha kujisaidia. Hapo tungemwelewa kuwa yupo genuine. au angezungumzia kutengeneza madawati ili wanafunzi wasikae chini.

  Tarifa yenyewe ni kuwa shule tatu za msingi katika jiji la mwanza zenye zaidi ya wanafunzi 3600 wanajisaidia kwa kutumia matundu 10 ya choo. matundu mengine 10 yametengwa kwa ajili ya waalimu wa shule hizo
   
 15. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Waache tu, hii itawasaidia watu waelewe kuwa Chama gani kinastahili kuingia madarakani sasa
   
 16. p

  pierre JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duuuuuuuuuh hii kali sana.Zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama.TUMEAHIDI TUMETIMIZA.
   
 17. U

  Umsolopogaas Member

  #17
  Sep 18, 2010
  Joined: Jul 18, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna mchangiaji wa JF alisema hapa kuwa watu wenye utamaduni wa kujisaidia vichakani hawafai kuwa viongozi kwani hawataona ukosefu wa vyoo kuwa ni tatizo. Kwa hiyo wanafunzi 3,680 kutokuwa na vyoo kwao siyo ishu na kama wana matundu ya vyoo 20 basi wameendelea! Kama kiongozi yuko nyuma kuliko anaowaongoza, uongozi wake hauwezi kuwa wa kuwapeleka mbele anaowaongoza bali utakuwa ni wa kuwarudisha nyuma.
   
 18. m

  matambo JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  yale yale ya sauper na mapanki na the darwins nightmare, sijui kwa nini sisi waafrika na hasa watanzania hatupendi kuambiwa ukweli, mi nilidhani ukiwa kiongozi mzuri hizi ndizo changamoto unazozihitaji kuzisikia ili uweze kuzifanyia kazi kwani kwa kuwa wewe upo ofisini ni ngumu kujua matatizo yaliyoko kwenye jamii
  bahati mbaya viongozi wetu wana hekima ya mbuni ya kuficha kichwa kwenye mchanga akidhani ndio kajificha mwili mzima, sasa huyo CED badala ya kumshukuru mwandishi yeye anamkamata

  hukohuko mwanza tuliambiwa hakuna mapanki wala watu wa mwanza hawali mapanki na rais akaongoza zile kelele, lakini jana kwa walioangalia taarifa ya habari ITV nadhani waliona wananchi wakinunua mapanki na wakisema hawana uwezo wa kununua samaki wazima, sasa sijui kikwete taarifa ya habari ile aliangalia na kama aliangalia aliichukuliaje? si ajabu mwandishi yule nae akakamatwa akiambiwa anaweka stori za kutunga,

  hii ndiyo tanzania usioyoijua na isiyoisha vibweka
   
 19. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #19
  Sep 18, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Huyo D.C achunguzwe kwanza kama kwake kwenyewe kuna choo!, msimlaumu bure. "HARI ZAIDI, NGUVU ZAIDI, KASI ZAID" YA mwanzo haitoshi?!.
   
 20. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #20
  Sep 23, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani hii story imeishia wapi?
   
Loading...