Tambara Bovu
JF-Expert Member
- Dec 19, 2007
- 585
- 140
na Grace Macha, Rombo
MWANDISHI wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima, Edward Kinabo (29), ametangaza kuwania ubunge katika Jimbo la Rombo linaloshikiliwa na Basil Mramba.
Kinabo ambaye ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa, anawania kiti hicho kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Alitangaza azma hiyo jana alipokuwa akifanya mikutano ya hadhara kwenye tarafa za Tarakea, Useri na Mengwe akilenga kukiimarisha chama chake kuelekea uchaguzi mkuu.
Kinabo alisema amefikia uamuzi huo kuitikia wito wa wakazi wa kata mbalimbali za jimbo hilo waliomwomba agombee ubunge wakati akiwanadi wagombea wa CHADEMA walioshiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.
Mwanasiasa huyo kijana ambaye katika uchaguzi mkuu uliopita alikuwa meneja wa kampeni za mgombea ubunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, John Mnyika, alisema ameamua kulikubali ombi hilo ili kutoa fursa kwa wananchi wa Rombo kupata mbunge kijana mwenye uwezo, unyenyekevu na usikivu wa kutosha kushughulikia matatizo na kero mbalimbali zinazowakabili vijana, wanawake na wazee wa jimbo hilo.
Akitangaza uamuzi wake huo aliouita kuwa ni zawadi ya mwaka mpya kwa wakazi wa Rombo, Kinabo alisema atatumia uzoefu wake wa kuwa mwanaharakati na kiongozi katika asasi zisizo za kiserikali (NGOs), kushughulikia matatizo ya kijamii na kiuchumi likiwemo tatizo kubwa la umaskini wa kipato linalowakabili wakazi wengi wa jimbo hilo.
Wazee wangu wa Mamsera, vijana wenzangu na mama zangu wa Mamsera, mimi Edward Edmund Kinabo leo natangaza rasmi kuwania ubunge wa Jimbo la Rombo, nimekubali kuwatumikia, uwezo huo ninao, msihofu nitawatumikia, endeleeni kuniunga mkono. Kwa pamoja tunaweza, kwa pamoja tutashinda, alisema Kinabo huku akishangiliwa.
Aliyataja baadhi ya matatizo yaliyomsukuma kukubali ombi la kuwania kiti hicho kuwa ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana, uhaba wa huduma za maji, kudorora kwa kilimo cha kahawa, migogoro ya ardhi, uhaba wa shule bora na vifaa vya ufundishaji pamoja na tatizo la Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kushindwa kutambua vipaumbele muhimu kwa maendeleo ya wananchi.
Aidha, alisema ameamua kugombea ubunge kupitia CHADEMA ili kuongeza nguvu ya wabunge makini wa kambi ya upinzani katika kuwatetea wananchi wa Rombo na Watanzania wote kwa ujumla.
Nimekuwa mwanachama wa CHADEMA kwa miaka sita sasa, nimelelewa na kujengwa kisiasa na chama hiki. Nimeiva kuwatumikia.
Lakini wapo watu wanaojipitishapitisha wakisema Kinabo hafai ni mdogo. Hao ni washamba wa kisiasa, siasa za dunia zimebadilika ni wakati wa Rombo kubadilisha historia na kujipatia mbunge kijana mwenye uwezo wa kuwatumikia. Kwa pamoja tutashinda, alisema.
Katika mikutano hiyo, Kinabo alipokea wanachama wapya 150 na kuanzisha matawi mapya sita, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kukiimarisha chama hicho. ...
Kazi ipo kwa Mramba