Mwandishi Tanzania Daima atangaza kumng'oa Mramba

Tambara Bovu

Tambara Bovu

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2007
Messages
586
Likes
6
Points
0
Tambara Bovu

Tambara Bovu

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2007
586 6 0
na Grace Macha, Rombo

MWANDISHI wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima, Edward Kinabo (29), ametangaza kuwania ubunge katika Jimbo la Rombo linaloshikiliwa na Basil Mramba.

Kinabo ambaye ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa, anawania kiti hicho kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Alitangaza azma hiyo jana alipokuwa akifanya mikutano ya hadhara kwenye tarafa za Tarakea, Useri na Mengwe akilenga kukiimarisha chama chake kuelekea uchaguzi mkuu.

Kinabo alisema amefikia uamuzi huo kuitikia wito wa wakazi wa kata mbalimbali za jimbo hilo waliomwomba agombee ubunge wakati akiwanadi wagombea wa CHADEMA walioshiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

Mwanasiasa huyo kijana ambaye katika uchaguzi mkuu uliopita alikuwa meneja wa kampeni za mgombea ubunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, John Mnyika, alisema ameamua kulikubali ombi hilo ili kutoa fursa kwa wananchi wa Rombo kupata mbunge kijana mwenye uwezo, unyenyekevu na usikivu wa kutosha kushughulikia matatizo na kero mbalimbali zinazowakabili vijana, wanawake na wazee wa jimbo hilo.

Akitangaza uamuzi wake huo aliouita kuwa ni zawadi ya mwaka mpya kwa wakazi wa Rombo, Kinabo alisema atatumia uzoefu wake wa kuwa mwanaharakati na kiongozi katika asasi zisizo za kiserikali (NGO’s), kushughulikia matatizo ya kijamii na kiuchumi likiwemo tatizo kubwa la umaskini wa kipato linalowakabili wakazi wengi wa jimbo hilo.

“Wazee wangu wa Mamsera, vijana wenzangu na mama zangu wa Mamsera, mimi Edward Edmund Kinabo leo natangaza rasmi kuwania ubunge wa Jimbo la Rombo, nimekubali kuwatumikia, uwezo huo ninao, msihofu nitawatumikia, endeleeni kuniunga mkono. Kwa pamoja tunaweza, kwa pamoja tutashinda,” alisema Kinabo huku akishangiliwa.

Aliyataja baadhi ya matatizo yaliyomsukuma kukubali ombi la kuwania kiti hicho kuwa ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana, uhaba wa huduma za maji, kudorora kwa kilimo cha kahawa, migogoro ya ardhi, uhaba wa shule bora na vifaa vya ufundishaji pamoja na tatizo la Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kushindwa kutambua vipaumbele muhimu kwa maendeleo ya wananchi.

Aidha, alisema ameamua kugombea ubunge kupitia CHADEMA ili kuongeza nguvu ya wabunge makini wa kambi ya upinzani katika kuwatetea wananchi wa Rombo na Watanzania wote kwa ujumla.

“Nimekuwa mwanachama wa CHADEMA kwa miaka sita sasa, nimelelewa na kujengwa kisiasa na chama hiki. Nimeiva kuwatumikia.

“Lakini wapo watu wanaojipitishapitisha wakisema Kinabo hafai ni mdogo. Hao ni washamba wa kisiasa, siasa za dunia zimebadilika…ni wakati wa Rombo kubadilisha historia na kujipatia mbunge kijana mwenye uwezo wa kuwatumikia. Kwa pamoja tutashinda,” alisema.

Katika mikutano hiyo, Kinabo alipokea wanachama wapya 150 na kuanzisha matawi mapya sita, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kukiimarisha chama hicho. ...

Kazi ipo kwa Mramba
 
Kinyambiss

Kinyambiss

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2007
Messages
1,372
Likes
7
Points
135
Kinyambiss

Kinyambiss

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2007
1,372 7 135
Hehe.. Hamwajui warombo nyie.
 
Kimbweka

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2009
Messages
8,609
Likes
58
Points
145
Kimbweka

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2009
8,609 58 145
Warombo wakae chonjo sasa!
 
I

Irizar

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2009
Messages
217
Likes
4
Points
0
I

Irizar

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2009
217 4 0
Mhhhhh namtakia mafanikio mema kijana. Kweli ni wakati sasa watanzania tuangalie kushoto na kulia pia mbele na nyumaaaaaa.
Tumechoshwaaaaaaaa na MAFISADI!!!!!!!!!!
 
Shapu

Shapu

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2008
Messages
2,016
Likes
360
Points
180
Shapu

Shapu

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2008
2,016 360 180
Kaka karibu...leta sera tusikie sie kule no longo longo. We are results oriented. Muulize mramba tulicho mfanya moja ya hizi chaguzi. Mwenyewe alikoma ndo maana akatoa machozi alipotetea hii lami tunayowekewa sasa.

Anyways karibu tuone utafanya nini!
 
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2008
Messages
3,158
Likes
22
Points
135
Next Level

Next Level

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2008
3,158 22 135
Kaka karibu...leta sera tusikie sie kule no longo longo. We are results oriented. Muulize mramba tulicho mfanya moja ya hizi chaguzi. Mwenyewe alikoma ndo maana akatoa machozi alipotetea hii lami tunayowekewa sasa.

Anyways karibu tuone utafanya nini!
He!he!he!he!he!.....atawahakishia upatikanaji wa ndafu, mbege na kisusio....!
 
Tambara Bovu

Tambara Bovu

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2007
Messages
586
Likes
6
Points
0
Tambara Bovu

Tambara Bovu

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2007
586 6 0
Mhhhhh namtakia mafanikio mema kijana. Kweli ni wakati sasa watanzania tuangalie kushoto na kulia pia mbele na nyumaaaaaa.
Tumechoshwaaaaaaaa na MAFISADI!!!!!!!!!!

Kwa kweli tumechoshwa na mafisadi.
 
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Messages
2,974
Likes
32
Points
0
Regia Mtema

Regia Mtema

R I P
Joined Nov 21, 2009
2,974 32 0
Huyu jamaa namkubali sana.
 
Kinyambiss

Kinyambiss

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2007
Messages
1,372
Likes
7
Points
135
Kinyambiss

Kinyambiss

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2007
1,372 7 135
Rombo CCM wataweka mtu atakewaletea uwaziri maendeleo yaje fasta, wafanyabiashara wao washamiri fasta.. Hakuna swala la CHADEMA rombo. They dont want to waste time alafu serikali ya JK iwawekee ngumu. CCM is the only thing in Rombo that can win. They operate in concert, wanakubaliana na mtu then wanampa kura. Mramba mwenyewe kidogo wamwage sema walijua ataleta uwaziri. CHADEMA no chance..sorry
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,744
Likes
2,035
Points
280
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,744 2,035 280
mmh..ngoja tuyaoner ila where there is a will, the only limit is the sky!
 
Jayfour_King

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2009
Messages
1,141
Likes
12
Points
0
Jayfour_King

Jayfour_King

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2009
1,141 12 0
Rombo CCM wataweka mtu atakewaletea uwaziri maendeleo yaje fasta, wafanyabiashara wao washamiri fasta.. Hakuna swala la CHADEMA rombo. They dont want to waste time alafu serikali ya JK iwawekee ngumu. CCM is the only thing in Rombo that can win. They operate in concert, wanakubaliana na mtu then wanampa kura. Mramba mwenyewe kidogo wamwage sema walijua ataleta uwaziri. CHADEMA no chance..sorry
Kwa mawazo haya kazi ya kuikomboa Tanzania safari bado ndefu, lakini ni kawaida kwenye vita no one to trust. Ukombozi wa kweli unahitaji kujituma na kuwa na mbinu mbalimbali na wanajeshi shupavu.
Pamoja tunaweza.
 
Spear

Spear

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2008
Messages
510
Likes
7
Points
0
Spear

Spear

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2008
510 7 0
na Grace Macha, Rombo

MWANDISHI wa habari wa Gazeti la Tanzania Daima, Edward Kinabo (29), ametangaza kuwania ubunge katika Jimbo la Rombo linaloshikiliwa na Basil Mramba.

Kinabo ambaye ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa, anawania kiti hicho kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Alitangaza azma hiyo jana alipokuwa akifanya mikutano ya hadhara kwenye tarafa za Tarakea, Useri na Mengwe akilenga kukiimarisha chama chake kuelekea uchaguzi mkuu.

Kinabo alisema amefikia uamuzi huo kuitikia wito wa wakazi wa kata mbalimbali za jimbo hilo waliomwomba agombee ubunge wakati akiwanadi wagombea wa CHADEMA walioshiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

Mwanasiasa huyo kijana ambaye katika uchaguzi mkuu uliopita alikuwa meneja wa kampeni za mgombea ubunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, John Mnyika, alisema ameamua kulikubali ombi hilo ili kutoa fursa kwa wananchi wa Rombo kupata mbunge kijana mwenye uwezo, unyenyekevu na usikivu wa kutosha kushughulikia matatizo na kero mbalimbali zinazowakabili vijana, wanawake na wazee wa jimbo hilo.

Akitangaza uamuzi wake huo aliouita kuwa ni zawadi ya mwaka mpya kwa wakazi wa Rombo, Kinabo alisema atatumia uzoefu wake wa kuwa mwanaharakati na kiongozi katika asasi zisizo za kiserikali (NGO’s), kushughulikia matatizo ya kijamii na kiuchumi likiwemo tatizo kubwa la umaskini wa kipato linalowakabili wakazi wengi wa jimbo hilo.

“Wazee wangu wa Mamsera, vijana wenzangu na mama zangu wa Mamsera, mimi Edward Edmund Kinabo leo natangaza rasmi kuwania ubunge wa Jimbo la Rombo, nimekubali kuwatumikia, uwezo huo ninao, msihofu nitawatumikia, endeleeni kuniunga mkono. Kwa pamoja tunaweza, kwa pamoja tutashinda,” alisema Kinabo huku akishangiliwa.

Aliyataja baadhi ya matatizo yaliyomsukuma kukubali ombi la kuwania kiti hicho kuwa ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana, uhaba wa huduma za maji, kudorora kwa kilimo cha kahawa, migogoro ya ardhi, uhaba wa shule bora na vifaa vya ufundishaji pamoja na tatizo la Halmashauri ya Wilaya ya Rombo kushindwa kutambua vipaumbele muhimu kwa maendeleo ya wananchi.

Aidha, alisema ameamua kugombea ubunge kupitia CHADEMA ili kuongeza nguvu ya wabunge makini wa kambi ya upinzani katika kuwatetea wananchi wa Rombo na Watanzania wote kwa ujumla.

“Nimekuwa mwanachama wa CHADEMA kwa miaka sita sasa, nimelelewa na kujengwa kisiasa na chama hiki. Nimeiva kuwatumikia.

“Lakini wapo watu wanaojipitishapitisha wakisema Kinabo hafai ni mdogo. Hao ni washamba wa kisiasa, siasa za dunia zimebadilika…ni wakati wa Rombo kubadilisha historia na kujipatia mbunge kijana mwenye uwezo wa kuwatumikia. Kwa pamoja tutashinda,” alisema.

Katika mikutano hiyo, Kinabo alipokea wanachama wapya 150 na kuanzisha matawi mapya sita, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kukiimarisha chama hicho. ...

Kazi ipo kwa Mramba
Huyo kijana amesha choka kuishi maisha ya Duniyani ,let wait and see I don`t want to cross the bridge before I get there .
 
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Likes
94
Points
0
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 94 0
- That is what we are talking about, ni vijana kujitokeza na kuingia in the game, saafi sana jamani mlio karibu naye tupeni kinachoendelea huyu kijana tumpe japo chochote katika kusaidia his dream, saafi sana Kinabo!

Respect.

FMEs!
 
Tambara Bovu

Tambara Bovu

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2007
Messages
586
Likes
6
Points
0
Tambara Bovu

Tambara Bovu

JF-Expert Member
Joined Dec 19, 2007
586 6 0
Huyo kijana amesha choka kuishi maisha ya Duniyani ,let wait and see I don`t want to cross the bridge before I get there .

Una wasiwasi gani?why are you saying so?
 
D

Dommy

Member
Joined
Jun 30, 2008
Messages
17
Likes
0
Points
3
D

Dommy

Member
Joined Jun 30, 2008
17 0 3
Bwana Kinabo

Kila la kheri, lakini una mtihani mkubwa mbele yako. Pamoja na shutuma za Mramba yeye bado ana nafasi kule maana ana network ya watu wengi wakiwemo wa Dar ambao ndio huwa wanasupport wagombea. Pia una wakati mgumu wa kuwahamasisha wanarombo hasa ukuzingatia Mramba alivyokomaa mpaka barabara ikajengwa.

Kila la kheri ila utambue uzito wa kazi yako.
 
G

Gangi Longa

Senior Member
Joined
Feb 5, 2010
Messages
195
Likes
30
Points
45
G

Gangi Longa

Senior Member
Joined Feb 5, 2010
195 30 45
Bwana Kinabo

Kila la kheri, lakini una mtihani mkubwa mbele yako. Pamoja na shutuma za Mramba yeye bado ana nafasi kule maana ana network ya watu wengi wakiwemo wa Dar ambao ndio huwa wanasupport wagombea. Pia una wakati mgumu wa kuwahamasisha wanarombo hasa ukuzingatia Mramba alivyokomaa mpaka barabara ikajengwa.

Kila la kheri ila utambue uzito wa kazi yako.
Kha na kupulula kote kule bado ana nafasi? wajameni????
 
Forum statistics

Threads 1,250,869
Members 481,514
Posts 29,748,902