Mwandishi Oscar Oscar achukua fomu kugombea nafasi ya Urais TFF

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,431
2,000
Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa michezo nchini wa kituo cha Radio EFM na TVE, Oscar Oscar leo Juni 9 2021 ameenda yalipo Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais katika Shirikisho hilo.

Mara baada ya kukabidhiwa fomu Oscar Oscar amesema baada ya kutoa maoni yake kwa muda mrefu ameona umefika wakati wa kuwania nafasi ya kuongoza Shirikisho la Mpira wa Miguu ili kuwa Mtendaji.

"Nimekuwa nikitoa maoni yangu kama Mwanahabari. Lakini sasa nimeona ni wakati mwafaka, kuwania nafasi hii ili kutekeleza mipango ambayo itaipeleka mbele soka letu la Tanzania, Afrika na Duniani kwa ujumla". amesema Oscar.

Oscar Oscar amekuwa mgombea wa nne kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi ya Urais katika Shirikisho hilo ambapo uchaguzi wa kikatiba unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Agosti mwaka huu 2021.
 

ngalanga

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,429
2,000
Kikubwa asiwe Simba basi
Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa michezo nchini Oscar Oscar leo Juni 9 2021 ameenda yalipo Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais katika Shirikisho hilo.
 

GEMBESON

JF-Expert Member
Apr 15, 2012
1,167
2,000
Hivi kosa kubwa la karia kupigwa vita kiasi hichi ni nini?
Shida ni itikadi za Simba na Yanga na ni vigumu kumpata Kiongozi ambae hana upande kwa hizi Timu mbili.

Ukiwa Kiongozi wa Michezo wa nchi hii huwezi kupendwa na kilamtu, hata Malinzi alivyokuwa madarakani wadau wa Simba waliona kama hawatendewi haki angalau uongozi wa Tenga kidogo haukuwa na hizi chuki.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
87,325
2,000
Mwandishi wa Habari na Mchambuzi wa michezo nchini wa kituo cha Radio EFM na TVE, Oscar Oscar leo Juni 9 2021 ameenda yalipo Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais katika Shirikisho hilo.
 

Poisonous

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,477
2,000
Kikubwa asiwe Simba basi
Namjua tokea akitoka Kufundisha Shule ya Msingi Wilayani Kinondoni huku akigombania 'DalaDala' na Musa Kawambwa ( sasa yupo Azam Media katika Redio yao ya Uhai FM ) kutokea pale zilipokuwa Ofisi za EFM Jengo la K-Net Kawe akiwa Hobela Hobela ( Choka Mbaya ) mno Kimaisha na Mdomo ukiwa umemkauka na Bahasha yake Kwapani.

Oscar Oscar ni mwana Simba SC ' lia lia ' kabisa japo kwa sasa nimeshangaa sana baada ya kupata Pesa kutokana na Kupigiwa pande Super Sports na Maulid Kitenge na Marehemu Ephraim Kibonde ( huku akianza kupata Exposure za Kusafiri nje ya nchi na kupanda Ndege mara ta Kwanza tena akiwa Ukubwani hivyo ) amebadilika na kuwa ni mwenye Dharau na Nyodo kiasi cha Kutushangaza wengi tunaomjua atokako na yaliyokuwa Maisha yake.

Nakataa na sijui kwanini mnamuita Oscar Oscar ni Mwandishi wa Habari wakati Kitaaluma si mwana Habari bali ni Mwalimu tu na Mchambuzi wa Soka na huu Uchambuzi ndiyo umemtambulisha mpaka Maulid Kitenge kumpigia pande EFM na akaachana na Ualimu wake uliokuwa ukimfanya avae Nguo zake za Kupauka 24/7 alipokuwa akianza Kuchambua Mpira EFM.

Hivi sasa Oscar Oscar anamalizia Shahada yake ya Mawasiliano ya Umma ( Mass Communication ) Tumaini University ya Mwenge akiwa ametanguliwa na akina Erick Shigongo ( sasa Mbunge ) na Florian Kaijage waliomaliza na Kuhitimu hapo hapo mwaka Jana Shahada zao za Kwanza.

Hata hivyo mlio karibu na Oscar Oscar mshaurini sana aachane na Anasa za dunia ( hasa Umalaya na Pombe ) kwani Pesa alizopata Ukubwani hivi na Kumiliki Gari lake la Harrier na Kupanga katika ' Appartment ' Kawe Beach zinamzuzua sana na kumpa Kiburi, Kujisikia na Kudharau kila Mtu kutokana na Ushamba ( Umbwiga ) wake aliokuwa nao kwa muda mrefu tokea Kijijini Kwao Kaliua Mkoani Tabora.

Kiuchambuzi hana ' Mpinzani ' Tanzania.

Cc: Ghazwat
 

mbwe

JF-Expert Member
Feb 23, 2018
508
1,000
Hivi kosa kubwa la karia kupigwa vita kiasi hichi ni nini?
Hao ni vilaza wa yanga ndio wanampiga vita Karia ,ila watanyoka tu maana sion wa kumtoa karia pale tff mpaka aje achoke mwenyewe ,kwanza yule faza ni smart upstairs kulinganisha na hao mbugilaz wanaosimama nae .

Karia kaleta mabadiriko mengi sana ambayo yanaonekana kwa watu smart tu ,wale vipofu ambao wanapaswa wanunuliwe miwani ili waone vzr ndio haters wa kalia kisa litimu lao halifanyi vzr na lawama zote wanapeleka kwa karia as if karia ndiye anacheza mpira uwanjan.

Yaan ulete akina fisiton ,srpong alafu utegemee ubingwa !!! Ukiona unaelekea kukosa lawama kwa karia ,shwain kabis hawa simbilisi wa jangwani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom