Elections 2010 Mwandishi mwingine MCL apata misukosuko

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Saturday, 25 September 2010

MWANDISHI mwingine wa magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), amepata misukosuko kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwandishi huyo Kwirinius Mapunda alipata mkasa huo, baada ya kuwekwa kizuizini mjini Songea, na walinzi wa CCM wakati wa ziara ya Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana (UVCCM) Ridhiwani Kikwete.

Ridhiwani alifika Songea mjini akitokea Namtumbo akifanya kazi ya kuomba kura kwa wagombea wa CCM.

Waandishi wengine wa Mwananchi ambao walishakumbwa na misukosuko katika kampeni za CCM ni Frederick Katulanda na Ray Naluyaga, wote wa Mwanza.

Katika tukio hilo Mapunda aliwekwa chini ya ulinzi na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya CCM mkoani Ruvuma, ambaye alimzuia kutekeleza majukumu yake

Mbali na kujitambulisha kuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya mkoa, mtu huyo pia alidai kuwa ni mmoja wa mwanafamilia wa mgombea wa urais kupitia CCM, Jakaya Kikwete.

Mara baada ya kuwasili kwa mgeni huyo wa UVCCM, mtu huyo alianza kumhoji mwandishi wa Mwananchi akitaka kujua ataandika nini kwenye ziara hiyo.

Mwandishi alimjibu kwamba ataandika atakayoyasikia na kuona na kwamba baada ya maelezo hayo , ofisa huyo alimtaka mwandishi wa habari apande gari alilokuwa akiliongoza yeye.

Msafara ulianzia ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma na kwamba ulipofika ofisi ya CCM Wilaya ya Songea mjini, ofisa huyo alizidi kuwa karibu huku akimzonga wakati wa kupiga picha.

Ridhiwani Kikwete pamoja na wenyeji wake waliingia kwenye ukumbi ambapo, naye mwandishi aliingia.

Lakini ghafla baada ya muda mfupi kijana wa CCM aliyevalia mavazi yaliyoandikwa Green Guard, alifika na kumweleza mwandishi kwamba alikuwa akiitwa nje ya ukumbi.

Mwandishi alinyanyuka kwenda nje ambako hakumkuta mtu yeyote na kwamba alipochunguza zaidi aligundua kwamba gari alilopangiwa lilikuwa limeondoka likiwa na mfuko wake wa kamera na vifaa vingine.

Mapunda alianza kusaka namba ya simu ya ofisa wa CCM ambapo baadaye aliipata na kumpigia simu.

Ofisa wa CCM huyo alijibu kwamba gari analo na kwamba mzigo wake upo salama, lakini akasisitiza kwamba asubiri nje.

Mwandishi alipojaribu kuingia ndani , aliambiwa na vijana wa CCM kwamba haruhusiwi kuingia kwenye mkutano wa ndani jambo ambalo lilimshtua zaidi.

Lakini kibaya zaidi yule ofisa aliyetoweka na gari likiwa na mfuko wa mwandishi , naye hakurudi na baadaye alipiga simu kwamba mzigo wa mwandishi ulikuwa kwenye Hoteli Top In One iliyopo maeneo ya Msamala.

Kufuatia hali hiyo Mwandishi aligundua kwamba tukio lilikuwa la makusudi.

Katibu wa UVCCM wa Mkoa wa Ruvuma, Mwajuma Rashid, alipoulizwa kama anafahamu lolote juu ya tukiuo hilo alisema safari ya Ridhiwani Kikwete iliratibiwa na ofisi yake na kwamba aliyemsumbua mwandishi hakumuona.

http://joomladigger.com/
 
kama kawaida lazima wasema ukweli ubanwe kusudi wafanye ufisadi wao....

vile vile hao vibaraka wa familia ya JK na mafisadi wa CCM hawatazuia mabadiliko ya Watanzania,, tumechoka sana jamani na hawa watu wa CCM kwani kwa miaka 50 wameshindwa je miaka mitano watafanya nini... Jk mwenyewe kasema kuwa wameshindwa kujenga chuo cha VETA mara sasa leo ataweza nini?????
 
CCM inatamani kulifungia gazeti la mwananchi. Watalitafutia kila sababu maana limekuwa mwiba kwao. Yule fisadi wa habari Muhingo Rweyemamu alisikika siku moja kwenye kampeni akisema kuwa siku za mwananchi zinahesabika. Yangu macho.
 
Gazeti la Mwananchi linakuza mno mambo haya. Kwa maoni yangu tatizo liko kwenye gazeti la MWANANCHI lenyewe ambalo lina ajenda ya siri kama ilivyokuwa huko Kenya na Uganda. Kama linataka waandishi wake wasisumbuliwe ni vema iliwagharimie waandishi wake kwa kuwapa usafiri wao na kuwalipa posho. Sio waandishi wao wakinyimwa posho ndipo wanaandika kuwa eti wananyanyaswa.

Waandishi wa habari wa Tanzania ni ajabu kweli kweli. Waandishi wa habari wanalipwa posho na wagombea halafu wanadai eti wao wako huru na siyo mafisadi. Unalalamika nini wakati wewe mwandishi wa habari unajidhalilisha kwa kusotea posho? Waandishi wa habari wa tanzania pamoja na kazi nzuri wanayofanya lakini wana kasoro kubwa mno. Wanadhani wao ni kila kitu.
 
Hata kama wanalipiwa posho etc etc wanayo haki ya kuandika wanachokitaka kulingana na taaluma zao mradi hawakiuki maadili ya uandishi. Tatizo ni kwamba wagombea wawachukua na kuwalipa posho wakitarajia waandishi hao waandike in their favour badala ya kuandika wanachokiona wao waandishi, which is totally wrong.

Kutokana na maelezo ya mwandishi huyu ni dhahiri kwamba yote hayo yalitokea. Sasa alitakiwa aripoti vipi?
 
CCM inatamani kulifungia gazeti la mwananchi. Watalitafutia kila sababu maana limekuwa mwiba kwao. Yule fisadi wa habari Muhingo Rweyemamu alisikika siku moja kwenye kampeni akisema kuwa siku za mwananchi zinahesabika. Yangu macho.

Then hakutokuwa na uhuru wa vyombo vya habari kabisa kwani wao wanataka wafanyapo mambo yawe ya siri au??? wao sindio wanataka si ha sa iwe hivyoo si ndio kama wanajua wanachokifanya sicho why do they complain and if wanafanya mazuri wathibitishee kwa jamii so this game hit both ways hivyo wakubaliane na matokeo hakuna si ha sa wanayoitaka na wanyoipalilia iende hivyo

Hawa viongozi siwaelewi wao wataka sifiwa kwa mazuri tuu na kukosolewa kwa mabaya au kuteleza kwao wao hawatakii yasikike then sio uongozi basi wao ni maraika wa MUNGU??
 
Back
Top Bottom