Mwandishi 'Msomaji raia' wa Raia Mwema

Kwa wale wanaofuatilia makala za Mtu anayejiita Msomaji Raia , kwenye gazeti la Raia Mwema, atakubaliana nami kuwa mtu huyu atakuwa ana nafasi nyeti ndani ya CCM.

Kuna mambo mengi amekuwa akiandika ambayo mengine ni ya ndani, kiasi ambacho si rahisi kwa mwanachama wa kawaida kuyajua. Na amekuwa akiikosoa CCM kwa uwazi , japokuwa kwa bahati mbaya na kwa sababu anazozijua yeye hajitambulishi kwa jina rasmi. Kwenye gazeti la leo la Raia Mwema ameandika makala inayosema ,NANI ADUI WA CCM? CHADEMA AU UFISADI?

Katika makala hiyo ameleza wazi kuwa wanaCCM wengi na viongozi wa serikali wameaminishwa kuwa adui wa CCM ni Chadema na wanaacha ukweli kuwa adui mkubwa wa CCM na taifa kwa ujumla ni UFISADI na ndiyo maana kila kukicha wanaindama CDM na wanamapinduzi wote wa nchi hii. Na pia ndio maana hata mageuzi wanayojaribu kuyabuni ili kujinasua kutoka kwenye tope la ufisadi, kama kujivua gamba yanashindwa kufanikiwa, kwa kuwa mawazo yao yako kwa CDM. Nyaraka nyingi za siri za CCM zinahusu jinsi ya kuishughulikia CDM, badala ya matatizo ya msingi yanayokera wananchi ambayo yamesababishwa na wao.

Kwako Msomaji Raia: Kama kweli una uchungu na nchi hii na kama kweli una nia ya dhati ya kupambana na ufisadi basi Toka kati yao na Ujitenge nao hao Mafisadi. Ukweli ni kwamba CCM imeshindwa kuongoza nchi, wananchi walio wengi wamepoteza matumaini na viongozi wengi wanaotokana na hiki chama. Jiunge na wanamageuzi wasaidie Watanzania wenzako wanaoendelea kukandamizwa na watawala waliolewa madaraka
 
Back
Top Bottom