Mwandishi Mayage S Mayage na kazi ya umamluki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandishi Mayage S Mayage na kazi ya umamluki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngalikivembu, Apr 14, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Nimesoma makala ya mwandishi wa muda mrefu Mayage S Mayage katika gazeti la Raia Mwema wiki hii.Nitangulie kusema nilimjua ndugu huyu kupitia maandishi yake katika magazeti ya Habari Corporation wakti huo.Ndo kwanza nilianza kumsoma nikiwa kidato cha tano pale mwanza magazeti yaliyokuwa yananunuliwa na shule.Nilimpenda kwa wakati huo,kwa namna alivyokuwa anajenga hoja zake.Na nilikuwa kipenzi cha magazet hayo kabla ya kusitisha rasmi kuyasoma mara baada ya kuingia mwekezaji mpya aliyekuwa na sera mpya za kupamba chama.

  Baadae kidogo nilikuja kumjua kumbe alikuwa kada wa ccm ambaye alitaka kujaribu bahati ya ubunge kule Muhambwe Kigoma.Akatupwa nje.Nilikuwepo huko wakati huo.Sikubahatika kumsoma tena kutokana na kisa cha hapo juu.Leo nimemsoma tena katika gazeti la Raia mwema.Nimelazimika kuandika baada ya kile alichoeleza katika makala yake,"CCM imejivua gamba,lakini...."

  Kwa waliosoma makala hiyo watabaini kuwa kumbe pale Newhabari wanaandika kuchumia tumbo tu na kusubiri makombo ya wanasiasa wanaomiliki magazeti hayo.Kushuku kwetu kuwa magazet hayo yanaandika kuwahadaa watanzania kumbe ni kweli.Msome Mayage uone anaeleza nini.Eti kumbe kazi ya uhariri ina siri nzito sana.Nilivyobaini ni kuwa wahariri hao ni symbol tu lakini wahariri rasmi ni wanasiasa wenyewe wenye kumiliki magazet hayo.Ushauri alioutoa kwa CCM ni kuwatosa wanajidai wanaipamba ccm na kuipenda kumbe wapo kwa ajili ya maslahi yao.Anashauri kwa sasa inabidi isitumie tena vyombo vya mafisadi kama inataka kurudisha heshima yake.

  Hakika kama ameamua kuhama huko na kubain wanalishwa "sumu" hilo ni wazo la busara sana.Kina Muhingo na Balile bado hawajabaini kama wanawatendea watanzania isivyo ipo siku watakuja jutia kazi yao hiyo.
   
 2. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Amejivua gamba.
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Labda kama Balile naye ajivue Gamba, Muhingo alishaondoka long time New Habari mara baada ya Uchaguzi Mkuu, Yupo Quality Media Group inayomilikiwa na Yusuph Manji. Coming soon in Tanzania Media Industry!!!!!!!!
   
 4. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 180
  Hata mimi nilisoma makala ya Mayage S, Mayage nikabaki mdomo wazi, kumbe ndio yanayofanyiak. Kweli naye amejivua gamba
   
 5. M

  Maimai Senior Member

  #5
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  stupid balile na muhingo. Wanajifanya nchi yao, wamesomeshwa na lowasa
   
 6. h

  hoyce JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ndo hivyo. Hata uhuru kuna waandishi wazuri sana, lakini hadi watoke ndo utawajua. Ndio maana ya kusema waandishi wanafuata sera za vyombo vyao. Kila mtu anaona ukweli kulingana na sera zake. Mfano ukiweka maji yakafika katikati ya glasi, kuna atakayesema GLASI IMEJAA NUSU na wapo watakaosema GLASI HAIKUJAA NUSU.na wote watakuwa sahihi, na ukweli huo utapokewa na watu kila mtu anavyotaka
   
 7. I

  Innocent Munyuku R I P

  #7
  Apr 24, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waandishi hawatakuwa huru Tanzania hadi siku watakapoamua kuwa huru. Hoyce kasema jambo la msingi sana, kila Media House ina policy zake. Ukienda IPP, Mwananchi, Uhuru etc kuna miiko yake. So ukikubaliana na sera unasaini mkataba kama vp acha saka kazi nyingine. Full stop!
   
 8. m

  matongo manawa JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani kaachia ngazi habari cop?
   
 9. b

  banyimwa Senior Member

  #9
  Apr 24, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tena ujiuliza kama kweli watu hawa wameelimika baada ya kupelekwa huko shule maana graduate hawezi kuwa anatumiwa hivi mpaka anageuka kuwa laughing stock. Watu wanatembea na njaa yao kwenye mfuko wa rambo na kila mtu anaiona wazi. Watu hawa ni kichefuchefu kikubwa na hatari kwa amani na utulivu wa nchi hii!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...