Mwandishi makini ni Chukizo kwa Utawala Wenye Mashaka, tukutane Kisutu leo

IKUNGURU IJIRU CHUKU

JF-Expert Member
Feb 27, 2021
372
500
Leo mwandishi makini akianza kufuatilia uozo unaofanywa na watawala dhalimu basi kesho asubuhi usishangae kukuta amenyofolewa kucha, ameng’olewa meno kwa ‘magalo’, ametobolewa jicho kwa spoku ya baiskeli na kuchinjwa kama kitoweo cha mwaka mpya.

Ni ishara ya utawala wenye mashaka. Sun Tzu mnamo miaka ya 400 aliita kitu hii, "Kill one, terrify a thousand.” Ni utaratibu wa kawaida katika nchi zenye utawala wenye mashaka. Ngoja nikupe mifano miwili, mitatu hivi.

Tarehe 22 Novemba 2000 mwandishi wa habari makini, Carlos Cardo, alipigwa risasi huko mjini Maputo Msumbiji, akiwa katika harakati za kuchapisha kwenye gazeti lake la Metical ubadhirifu,
wa dola za Kimarekani milioni 14 kwa ajili ya maendeleo kutoka benki kuu, “Banco Comercial de Moçambique.”
 

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,266
2,000
Kutoweka kwa Sanane,Lissu,na yule mwandishi wa mwananchi kule kibiti,ilitosha kuwanyamazisha watu 50,000,000+ wakiwemo waandishi wa habari.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom