Mwandishi Katabazi analipwa na Liyumba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandishi Katabazi analipwa na Liyumba?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanda2, Apr 24, 2010.

 1. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nimekuwa nikisoma habari za kesi ya Bwana Liyumba kupitia magazeti mbali mbali,likiwemo Tanzania Daima ambako mwandishi Happyness Katabazi ndiye anayeripoti masuala ya mahakamani.

  Uandishi wake ni wa kishabiki sana.naona kama haufuati kanuni za fani ya habari.nikitizama Gazeti la Nipashe linavyoripoti au Mwananchi kuna tofauti kubwa sana.mnaweza kupitia Blog yake Katabazi na kuona maandishi yake.

  kwenye kuripoti kwake anawasifu mawakili wa Liyumba mara kwa mara utasikia kulikuwa na kicheko.
  mnaweza kutizama habari yake www.freemedia.co.tz halafu tizama www.ippmedia.com tizama hata huko nyuma alivyokuwa akiripoti. anaandika kishabiki sana.soma maandishi yake hapa.
  http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=15158
   
 2. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  1. Mwango
  2. 23rd April 2010

  3. [​IMG]
   B-pepe

  4. [​IMG]
   Chapa

  5. [​IMG]
   Maoni

  6. [​IMG]
   Aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Amatus Liyumba.   Aliyekua Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, anayekabiliwa na shitaka la matumizi mabaya ya ofisi, amedai mahakamani kuwa mradi wa majengo pacha ulisimamiwa na Meneja mradi, Deogratius Kweka, na kwamba (Kweka) aliwajibika moja kwa moja kwa Gavana (wakati huo marehemu Daud Balalli).  Kadhalika, Liyumba alidai kuwa mradi huo ulikuwa chini ya kurugenzi yake ambapo alipewa mamlaka ya kusaini barua zilizofanyiwa mapendekezo na gavana kutoka kwa meneja mradi.
  Liyumba alitoa madai hayo wakati akitoa utetezi wake mbele ya jopo la mahakimu watatu, Edson Mkasimongwa, Lameck Mlacha na Benedict Muingwe wanaosikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
  Akiongozwa na Wakili wa utetezi, Majura Mgafu, mshtakiwa huyo alidai kuwa mradi wa majengo hayo ulianza mwaka 2002 ukiwa chini ya Kurugenzi ya Utumishi na Utawala.

  Alidai kuwa katika mradi huo, BoT ilimuajiri mtaalam wa ujenzi kwa mkataba maalum, yaani Kweka ambaye alikuwa anawasiliana moja kwa moja na gavana.

  "Mradi wote ulisimamiwa na Kweka na ulikuwa katika kitengo kinachojitegemea, lakini chini ya kurugenzi yangu… Kweka alikuwa akiwasiliana na makampuni yote yaliyokuwa na majukumu tofauti katika mradi huo na mabadiliko au mapendekezo yote yaliyohusu mradi aliwasiliana na gavana," alidai.

  Aliiambia mahakama kuwa aliteuliwa kusaini nyaraka na barua za mradi huo, kwa sababu Kweka hakuwa na ajira ya kudumu BoT. Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano kati ya Liyumba na wakili wake, Magafu:
  Wakili: Shahidi wewe unafanya shughuli gani?

  Liyumba: Mimi ni mfanyabiashara, nina kampuni ya kukopesha fedha kwa wajasiliamali wadogo wadogo na ninamiliki hoteli.
  Wakili: Mwaka 2006, ulikuwa unafanyakazi gani?

  Liyumba: Nilikuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala BoT ambapo nilistaafu kwa mujibu wa sheria Desemba, mwaka 2008. Kabla ya kustaafu nilikuwa na majukumu ya kusimamia uendeshaji wa shughuli zote za benki hiyo na nilikuwa chini ya Naibu Gavana na Gavana.
  Wakili: Unaufahamu mradi wa ujenzi wa majengo pacha?

  Liyumba: Ndiyo, naufahamu. Ulikuwa chini ya kurugenzi yangu, lakini ulikuwa una kitengo kinachojitegemea.
  Wakili: Una maana gani hapo?

  Liyumba: Mradi ulikuwa chini ya Kweka na aliwajibika moja kwa moja kwa Gavana.
  Wakili: Je, Kweka ni mwajiriwa wa BoT?

  Liyumba: Hapana, alikuwa na mkataba maalum kwa ajili ya mradi huo.
  Wakili: Ulihusika vipi katika mradi huo?
  Liyumba: Nilihusika kushughulikia masuala mbalimbali na kwa kuwa meneja hakuwa mwajiriwa, niliteuliwa kusaini barua zilizohusu mradi huo.

  Wakili: Uliteuliwa na nani?
  Liyumba: Na Gavana wa BoT. Nilikuwa nasaini barua ambazo zilifanyiwa mapendekezo na meneja mradi na kukubaliwa au kukataliwa na gavana kuhusu mradi huo.
  Wakili: Nani alitoa maelekezo?

  Liyumba: Meneja alitoa ushauri wote kwa gavana.
  Wakili: Hapa mahakamani kuna tuhuma dhidi yako kwamba ulikiuka taratibu bila kibali cha bodi. Je, unasemaje?
  Liyumba: Mimi na bodi tulikuwa mbali kwani haikuniteua wala hainihusu kabisa.
  Wakili: Nani aliandaa nyaraka zinazohusu mradi huo?

  Liyumba: Meneja mradi alitayarisha nyaraka zote za kupeleka katika bodi, lakini gavana na naibu gavana ndiyo walikuwa na mamlaka ya kuwasilisha mbele ya bodi.
  Wakili: Nani alihusika na mabadiliko ya mradi?

  Liyumba: Mapendekezo yote yalifanywa na meneja mradi. Mimi ni mchumi, masuala ya ujenzi hayanihusu kabisa.
  Wakili: Je, Unaiambia nini mahakama kuhusu tuhuma hizi?
  Liyumba: Mimi naomba mahakama ielewe ukweli, sio kweli kwamba mimi nilitumia madaraka vibaya na wala sioni shitaka lolote dhidi yangu hapa. Naye Wakili wa Serikali Juma Ramadhani, alimhoji shahidi huyo wa utetezi kama ifuatavyo:

  Wakili: Shahidi, sheria za BoT unazijua?

  Liyumba: Ndiyo nazijua.
  Wakili: Nani ana mamlaka ya kufanya mabadiliko?

  Liyumba: Bodi ya BoT.
  Wakili: Mradi huo nani alitakiwa kufanya mabadiliko?
  Liyumba: Ni Bodi.
  Wakili: Mamlaka ya kusaini barua ulipewa kwa njia gani?
  Liyumba: Gavana alinipa mamlaka kwa njia ya maneno.

  Naye shahidi wa pili wa utetezi ambaye pia ni mshitakiwa katika kesi hiyo, Bosco Kimela (55) alidai kuwa kati ya mwaka 2001 na 2006 alikuwa Kaimu Katibu wa BoT.

  Kimela alidai kuwa anaufahamu mradi wa majengo pacha na kwamba ulikuwa chini ya kurugenzi ya utumishi ambapo gavana aliweka kitengo kilichokuwa kinasimamiwa na meneja mradi ambaye alikuwa mtaalamu wa masuala ya ujenzi.

  Upande wa utetezi ulifunga ushahidi na mahakama ilisema itatoa hukumu ya kesi hiyo Mei 24, mwaka huu.  1. CHANZO
   
 3. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Pekua Tovuti
  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  • LIYUMBA AINANGA SERIKALI.
  • Amtupia mzigo marehemu Ballali

  na Happiness Katabazi


  [​IMG]
  ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu, Amatus Liyumba (62), ambaye sasa anakabiliwa na shtaka moja la matumuzi mabaya ya ofisi ya umma, amedai serikali haijui itendalo dhidi ya kesi iliyomfungulia.


  Liyumba ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, izingatie ukweli wakati wa kutoa hukumu dhidi yake Mei 24 badala ya kuwasikiliza watu wasiojua watendalo.  Maneno hayo mawili ‘hawajui watendalo’ yanafanana na yale aliyotumia Yesu Kristo, anayeaminika kuwa ni Mwokozi wa waumini wa Kikristo wakati akieleza kitendo cha Wayahudi waliokuwa wakimsulubisha (Luka 23:34).  Mshtakiwa huyo jana alipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kutoa utetezi wake mbele ya Kiongozi wa Jopo la Mahakimu Wakazi, Edson Mkasimongwa, aliyekuwa akisaidiwa na Lameck Mlacha na Benedict Mwingwa.  Kesi hiyo ambayo imevuta hisia za watu wengi ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam ilifikishwa mahakamani hapo Januari 26 mwaka jana ambapo Liyumba alikuwa akikabiliwa na makosa mawili ambayo ni matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia hasara serikali ya sh bilioni 221.


  Hata hivyo Aprili 9 mwaka huu, mahakama hiyo ilimfutia shtaka la kuisababishia hasara serikali baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha hasara kwa namba kama ilivyokuwa ikitakiwa.
  Liyumba, aliongozwa kutoa ushahidi wake na wakili mahiri wa kujitegemea Majura Magafu aliyekuwa akisaidiwa na Jaji Mstaafu Hillary Mkate, Onesmo Kyauke na Hudson Ndusyepo huku upande wa mashitaka ulikuwa ukiongozwa na mawakili waandamizi Juma Mzarau, Ben Lincoln na Tabu Mzee.  Mstahakiwa huyo, alianza kujitetea saa tano asubuhi hadi saa saba mchana mbele ya umati wa watu uliofurika ndani ya mahakama hiyo na kusababisha watu wengine kusimama nje ya ukumbi wa mahakama, alidai kuwa anaiomba mahakama kuzingatia ukweli katika kuandika hukumu yake.
  Amedai kuwa ameamua kutoa tahadhari hiyo kwa sababu upande wa mashitaka umewasilisha vielelezo ambavyo baadhi yake ni barua alizozisaini zilikuwa zinatoa maelekezo kwa kampuni ya ujenzi wa mradi wa Ten Mirambo Extention “Minara Pacha” ya Design&Service wakati kuna barua nyingine zilisainiwa na wasaidizi kwa niaba yake, na barua za kampuni ya Design&Service zilizokuwa zikiandikia BoT, hazikuletwa mahakamani hapo kwa makusudi.  “Waheshimiwa naomba sana mzingatie ukweli kabla ya kufikia kutoa hukumu dhidi yangu, kwani upande wa mashitaka umeleta barua hizo tu kwa sababu zimesainiwa na Liyumba, kama upande wa mashitaka unatenda haki ni kwa nini ulishindwa kuleta barua zilizosainiwa na wasaidizi wangu kwa niaba yangu ambao nao walikuwa wakitoa maelekezo mazito tu kuhusu mradi huo?


  “Na kama kweli walikuwa wanatenda haki ni kwa nini wameshindwa kuleta zile barua ambazo kampuni ya ujenzi ilikuwa ikiiandikia BoT na mimi kwa kuwa niliteuliwa na Gavana (Marehemu Balali) kushughulika na masuala ya uongozi katika mradi huo, nilikuwa nazijibu baada ya kupata idhini ya gavana.

  “Kwa faida ya waendesha mashitaka mimi nilikuwa nikijibu barua za Design&Service na barua hizo nilizosaini zimeonyesha wazi nilikuwa najibu barua hizo kwa kutumia kumbukumbu mbalimbali za barua zilizokuwa zinatoka nje kuja BoT...narudia tena kama hawa waendesha mashitaka walikuwa wanatenda haki wangeleta nyaraka hizo zote nilizozitaja.  Kwa sababu wanazozijua wao walipoona tu barua hizo zinasaini yangu wakazichomoa kwenye jalada ambalo linahifadhiwa kwenye ofisi ya Meneja wa Mradi na kuzileta mahakamani,” alidai Liyumba na kusababisha watu kuangua vicheko na wakili mwandamizi wa serikali Juma Mzarau ambaye alikuwa akimhoji kujiinamia na kisha kucheka.


  Liyumba ambaye ni mchumi kitaaluma, aliiambia mahakama kuwa katika kipindi cha mwaka 2001-2006 alikuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa BoT na alistaafu kwa mujibu wa sheria Desemba 2008. Majukumu yake akiwa na wadhifa huo alikuwa akishughulika na shughuli zote zinazohusu uendeshaji wa benki.


  Alieleza kuwa kiongozi wake wa kazi alikuwa Naibu Gavana huku nafasi ya Gavana ilikuwa ikishikiliwa na Daudi Balali na alikuwa akiwajibika kwake lakini kama hakuwepo alikuwa akiwajibika kwa naibu wake.


  Alidai anaufahamu mradi wa ujenzi wa Minara Pacha kwani wakati anahamishiwa Makao Makuu ya BoT Dar es Salaaam, akitokea mkoani Mwanza alikuta mradi huo upo kwenye mchakato na ilikuwa mwaka 2000 na ujenzi wa mradi huo ulianza rasmi mwaka 2002.


  Liyumba ambaye anamiliki hoteli moja na kampuni moja ya kutoa mikopo midogo midogo , alidai kuwa kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na benki hiyo, mradi ulikuwa chini ya kurugenzi aliyokuwa akiiongoza yeye ila kulikuwa na kitengo kinachojitegemea chini ya Meneja Mradi Deogratius Kweka na meneja huyo alikuwa anapeleka taarifa za mradi huo moja kwa moja kwa gavana.


  “Huyo meneja mradi hakuwa mwajiriwa wa kudumu wa BoT bali alikuwa na ajira ya mkataba ambayo aliipata kutokana na kuanzishwa kwa mradi huo.


  Mimi nilikuwa nahusika kiutendaji kwa sababu Kweka hakuwa mwajiriwa wa kudumu wa BoT, na kwa kuwa hakuwa na ajira ya kudumu meneja huyo hakuwa na mamlaka ya kusaini barua za BoT kwenda kwa kampuni ya Design&Service.
  “Mimi ndiye niliyeteuliwa na Gavana kuwa nasaini barua mbalimbali kwa niaba ya BoT zilizokuwa zikihusu mradi huo na kama mimi sipo alikuwa akizisaini msaidizi wangu na kumbukumbu zipo...kama Kweka angekuwa amepewa dhamana ya saini barua hizo za mradi wala mimi nisingeweza kusaini,” alidai Liyumba.


  Huku akionyesha kujiamini, Liyumba alieleza utaratibu wa barua zilizokuwa zikienda BoT na zile zilizokuwa zikielekezwa kwake, barua zote zilizokuwa zikihusu mradi, zilifikia kwa gavana na yeye huzipeleka kwa Meneja Mradi na meneja huyo anatoa ushauri wa kitaaluma.  “Gavana, alikuwa akitoa maelekezo kwangu ya jinsi ya kuzijibu barua hizo ambazo mimi nilikuwa naweka saini yangu, ushauri wote wa ujenzi wa mradi ule Meneja Mradi alikuwa anautoa kwa gavana kwa sababu wafanyakazi wa Benki hawakuwa mainjinia,” alieleza.


  Alifafanua kwamba watu wanapoizungumzia Menejimenti ya Benki Kuu, watambue kwamba menejimenti hiyo ni Gavana; hayo yametamkwa wazi kwenye Sheria ya Benki Kuu na kuongeza kuwa Jamhuri kudai yeye aliidhinisha mabadiliko ya ujenzi wa mradi huo bila idhini ya bodi ‘haijui itendalo’.


  Alidai kwamba yeye na bodi ya wakurugenzi hawafanyi kazi kama inavyodaiwa kwa sababu haimhusu na wala haikumteua kuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala huku akisisitiza kuwa yeye alihusika katika mradi huo kwa shughuli za kiutawala tu.


  “Aliyekuwa na jukumu la kupeleka chochote kilichohitajika kwenye mradi ni Meneja Mradi kwani ndiye aliyekuwa anaandaa taarifa za mradi kwa gavana, ndiye alikuwa anazipeleka taarifa hizo kwenye bodi.


  Mapendekezo ya ushauri mabadiliko ya mradi yalikuwa kamati ya mradi na ilijadili na kuwahusisha washauri kutoka kampuni tatu ambazo zilikuwa zinatoa ushauri wa ujenzi huku malipo ya kazi yao yalikuwa yakilipwa na BoT.


  “Baada ya gavana kupelekewa ushauri huo, kama akitaka kufanya mabadiliko ya ujenzi alikuwa anamuelekeza Meneja Mradi ambayo hurudi kuiarifu kamati na hatimaye hufikisha kile kilichoamuliwa kwa gavana.  “Mwisho kabisa naiomba mahakama hii tukufu wakati inaandaa hukumu dhidi yangu izingatie ukweli na iniachilie huru kwani hilo shitaka ambalo Jamhuri inadai nimetenda ...sioni kama linanihusu mimi kwani sijatenda kosa hilo na kwa kunishitaki Jamhuri imeonyesha haijui ilitendalo,” alidai Liyumba na kusababisha watu kuangua vicheko.


  Naye aliyekuwa Kaimu Katibu wa Benki Kuu na Katibu wa Bodi ya Benki hiyo ambaye ni mwanasheria kitaaluma, Bosco Kimela (52), aliieleza mahakama kuwa shitaka linalomkabili Liyumba hastahili kushtakiwa nalo kwani hajalitenda.


  Kimela ambaye anakabiliwa na kesi moja ya matumuzi mabaya ya ofisi ya umma na mbili za EPA na anaendelea kusota rumande kwa ajili ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, aliiambia mahakama pamoja na aliyekuwa na wadhifa huo pia alikuwa na wadhifa wa kuandaa vikao mbalimbali vya benki ambavyo gavana alikuwa anaviitisha.


  Alidai taarifa za kitaalamu za mradi huo zilikuwa zinaandaliwa na Meneja Mradi na kuhusu mradi huo Liyumba hakuhusika kwa namna yoyote kutoa maamuzi yake binafsi kwani gavana alikuwa akimpatia orodha ya majina kabla ya kikao kufanyika na yeye alikuwa akiiandaa barua za mialiko na ya kuwaita wajumbe.

  ‘Kwenye vikao Gavana alikuwa akiwasilisha taarifa mbalimbali zinazohusu benki na Meneja Mradi, Deogratius Kweka, aliyekuwa akiwasilisha taarifa zinazohusu mradi huo na tangu mwaka 1992 hadi 2008 nikiwa na nyadhifa hizo sijawahi kushuhudia Liyumba akifanya maamuzi bila idhini ya Gavana, hilo halijawahi kutokea...mimi ndiye nilikuwa naandaa taarifa za vikao, ajenda, yatokanayo na mkutano, utekelezaji wa yaliyoamuliwa na kikao na nikishaandaa napeleka kwa Gavana na si vinginevyo.”


  Baada ya kutoa maelezo hayo Wakili wa serikali Juma Mzarau aliiomba mahakama ipokee maelezo ya onyo ya Bosco kama kielelezo lakini ombi hilo lilipingwa vikali na wakili wa utetezi kwa madai kwamba shahidi huyo si wa upande wa mashitaka na kama jamhuri ilimuona shahidi huyo ni muhimu kwao isingemuondoa kwenye orodha yake ya ushahidi na kwamba upande wa mashitaka haujatoa sababu za kutaka mahakama hiyo ifute ushahidi ulitolewa jana na Bosco.

  Akitoa uamuzi kuhusu ombi hilo la upande wa mashtaka, Hakimu Mkazi Mwandamizi Benedict Mwingwa alisema jopo hilo linatupilia mbali kwa sababu upande huo umeshindwa kutaja sababu za kukutaka ushahidi wa Bosco mahakama hiyo ikatae na kuamuru Bosco apande tena kizimbani kwa mara nyingine ili aendelee kutoa ushahidi wake.

  Baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake, wakili Magafu aliiambia mahakama kuwa walikuwa wamekusudia kuleta mashahidi wanne, lakini kutokana na mashahidi hao wawili waliomaliza kutoa ushahidi wao jana, wameona ushahidi huo unakidhi haja hivyo wamefikia uamuzi wa kufunga kesi yao.  Aidha, Hakimu Mkazi Edson Mkasimongwa alisema mahakama imekubali ombi hilo la kufunga kesi kwa upande wa utetezi, na akazitaka pande zote katika kesi hiyo kuwa Mei saba , zilete majumuisho ya mchanganuo wa ushahidi ulitolewa jana, Mei 21 kesi hiyo itakuja kwa ajili ya kutajwa na Mei 24, mahakama hiyo ndiyo itatoa hukumu ya kesi hiyo.  Januari 26, mwaka jana, Liyumba na Meneja Mradi wa Benki Kuu, Deogratius Kweka, walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza na kusomewa mashitaka hayo ya kuidhinisha mradi wa majengo ya minara pacha bila idhini ya bodi ya wakurugenzi na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 221. Mei 27 mwaka jana, mahakama hiyo iliwafutia kesi, lakini muda mfupi baada ya kuachiliwa walikamatwa tena mahakamani hapo na Mei 28 mwaka jana, Liyumba peke yake ndiye aliyerudishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka hayo na Kweka akawa ameachiliwa huru. Tangu kipindi hicho hadi sasa Liyumba anaendelea kusota rumande, baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, ambapo mahakama ilimtaka atoe fedha taslimu au hati ya mali yenye thamani ya sh bilioni 110.
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nenda ukalalamike baraza la habari kanda2 au ukiona article zake usizisome. Au lalamikia waandishi wa Uhuru na mzalendo ambao pia huwa wanaandika kama huyo unayemlalamikia!
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kanda2 kwani kunatatizo gani hapo?
  Sasa kama watu walicheka mahakamani karipoti kama ilivyo kuwa kuna tatizo gani hapo Kanda2.?
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Huyo Katabazi anaweza kuwa na interest zake lakini na IPP media nao wana interest zao kuhusiana na kesi hiyo. Si ajabu mrengo wa reportage yao inakinzana
   
 7. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe unalipwa na nani? Na waliomshtaki? Just Thinking out silent
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Apr 24, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Katabazi yuko hatua nyingi sana katika uandishi wa habari za mahakamani kuliko waandishi wa vyombo vingi vya habari.
  Katabazi unaweza kudhani anashabikia jambo lakini mwisho wa siku kile anachooandika huwa ndivyo.
  Nilifuatilia kwa makini habari za mahakamani wakati wa sakata la marehemu Ditopile, kisha nikamfuatilia katika kesi ya Zombe na sasa kesi hii, huyu dada ni mjuzi sana wa kazi yake, maana hutoa yale ambayo yameeongelewa mahakamani kama yalivyo......hapa nazungumzia anavyoripoti.
  sasa huwa anaandika makala kuelezea maoni yake juu ya mienendo mbalimbali yya kesi kwa uzoefu wake wa kushinda kwenye mahakama zetu, mara nyingi amekua akionya namna DPP na serikali kwa ujumla inavyokurupuka kufungua kesi bila maandalizi kwa kuangalia upepi na ujiko wa kisiasa.
  aliwahi kutabiri kushindwa kwa serikali ktk kesi ya Zombe na sasa ukisoma makala zake utagundua kuna aina ya utabiri kuwa kesi za kina Liyumba zitaiingizia serikali hasara nyingi , kwamaana nafasi ya kushinda ni ndogo, ni maoni yake ambayo kwa wenye akili ndio hung'amua anaandika nini.
  ...mimi naamini Katabazi anaelekea kuwa Gwiji wa kuandika habari katika sekta ya sheria hapa Tanzania.
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Apr 24, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Umemaliza kila kitu Mkuu.
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Apr 24, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  GS ukisoma vyema hayo maelezo kwenye taarifa/ripoti ya mwandishi Katabazi kutoka mahakamani sioni ushabiki wa dhahiri.....ila utakachogundua ni aina ya uandishi wa mtu mwenye uelewa wakutosha wa masuala ya uendshaji kesi.....
  huyu mama amejitoa sana katika jukumu hili la kuandika habari za mahakamani....
  huyu ndie mwandishi pekee alie fanikiwa kumuhoji Ditopile baada ya kuachiwa kwa dhamana, huyu alikua na taarifa nyingi kuhusu hali ya Dito kule mahabusu , ni hivyo hivyo kwa kina Liyumba na Zombe.
  huyu dada haishii kisutu ama mahakama kuu , anakwenda hatua moja mbele, habari zake hunukuu vifungu vya sheria, taratibu za mahakama , miongozo ya mahakama, yeye anakuwepo mahakamani wakati kesi hizi zinaendeshwa hadi dakika mtuhumiwa anarudiishwa mahabusu ...tofauti na waandishi wengi, huingia na kutoka kwenye zile chamber za kuendeshea mashitaka.
  Katabazi nitashangaa kama free media hawajakuongeza mshahara hadi leo.
  huyu niana ya Waandishi kama Nevile Meena, kama Vick Mtetema, nawengineo.
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  ndiyo analipwa na liyumba..................usione liyumba anasota hivyo mahabusu ni kwa sababu zingine tu za wakubwa km jk ila jamaa anaweza hata kununua mikoa mitatu ta tz jinsi alivyo njema...................................WE unafikiri kwa njaa za waandishi wetu na tu tujisenti twa liyumba ataacha kumfagilia??????????????????????
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  Apr 24, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwahiyo kumnunua Katabazi ndio anaetoa hukumu ? hiyo si siasa kuwa ukinunua Waandishi utapata kura maana watakupigia kampeni
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Apr 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Bw. Kanda2 kule kwenu mzalendo hakukaliki?..peleka huko huu UDAKU.
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Apr 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Katabazi ni sahihi kwali Liyumba ana kosa gani? Si ameshitakiwa kumagrini tu, kafanywa (scape goat) kwani alikula hela hizo na vigogo wengine?
   
 15. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #15
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nimekusikia Dada yangu. nilikuwa natoa ushauri tu kwa mujibu wa uelewa wangu,unasema kuwa utabiri wa kushindwa serikali. hilo halihitaji uchambuzi. wanasheria wa serikali hawana uwezo wengi ndio kama wanajifunza kushindana na mawakili wa kujitegemea sio rahisi kwao.pia hawana mishahara mizuri,mawakili wa kujitegemea wanauza kesi itakuwa na hawa wanasheria wa serikali wanaolipwa laki nne?


  ili mtu uwe Gwiji wa Habari unatakiwa usiwe biased.kuna watu kama Jenerali Ulimwengu au Mbwambo ni mifano ya watu wanaolinda fani ya habari.Nimefuatilia habari karibu zote za Liyumba nimeona zinaandikwa kishabiki kama kuna INTEREST.

  Mwisho nisamehe kama kutoa maoni yangu ni kosa ila nimeweka habari zote mbili ili watu wapime.
   
 16. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  waandishi wananunuliwa sana sio na wanasiasa tu sekta karibu zote.muulize irine mark aliandika makala ya mshiko kwa waandishi hasa makanjanja.
   
 17. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #17
  Apr 24, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  [QUOTE]Liyumba: Nilihusika kushughulikia masuala mbalimbali na kwa kuwa meneja hakuwa mwajiriwa, niliteuliwa kusaini barua zilizohusu mradi huo.[/QUOTE]

  Haya sijaenda shule lakini ndiyo kwanza kusikia kuwa mtu anateuliwa kusaini vitu asivyohusika navyo! Mimi nilidhani saini inaendana na dhamana? Utasaini vipi kitu ambacho hauna habari nacho? Au ignorance siku hizi is an ACCEPTED excuse!

  Amandla...........
   
 18. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #18
  Apr 24, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mwanamama Katabazi is one of the most balanced court reporters this country has ever produced!! Hongera mama kwa kazi nzuri ya kutuhabarisha.
   
 19. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huu sasa wivu tu sasa kama vipi sema tu manake huyu mseminari hatoi pesa yeye anakupa mambo tu
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe mkuu. Utendaji wake kazi katika mahakama kwa muda mrefu umempatia huyu binti uzoefu wa kutosha katika masuala haya. Kwa hakika, katika fani ya uandishi na yeye ni 'authority' kwa masuala ya mahakamani
   
Loading...