Mwandishi Kanichakachua na kuneemekea Mgongoni kwangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandishi Kanichakachua na kuneemekea Mgongoni kwangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Derimto, Dec 3, 2010.

 1. D

  Derimto JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama ni kuibiwa na kutapeliwa na Baadhiya wana habari walikosa maadili yatakuwa yamewapata wengi ila hawana pa kusemea maana hata wakisema nani ataandika maana wengi wao wako kundi moja.

  Nilikuwa na habari ambayo nilishawaitoa kwenye ngazi husika na hawakuifanyia kazi nikaona hapa dawa ni kumpa mwandishi wa habari aitoe kwa umma ili umma uujue ukweli na waamue wao.

  Nikasafiri kwenda mkoani Arusha mapumziko nikiwa bar na rafiki yangu wa siku nyingi tunapata kilaji akatokea dada mmoja ambaye yule bwana alinitambulisha kuwa huyo ni kama mdogo wake kwa jinsi wanavyo heshimiana na yule dada alionyesha kunifahamu na alishawahi kuniona waziri fulani na baadhi ya watu akiwemo mtu ambaye yeye anamtafuta sana aongee naye lakini anashindwa kumpata kutokana huyo bwana kumkwepa mara kwa mara nami nikamuuliza kuwa yeye anafanya kazi gani akaniambia yeye ni mwandishi wa habari wa MCL. Nikaona ile habari niliyotamani kuitoa kwa jamii imepata mahali pake nikamwuliza nikimpa habari anaweza kuipeleka kwa usahihi bila kupotosha akaniambia hilo kwake halina shida yoyote na hasa ukizngatia niko na kaka yake.

  Nilikusanya ushahidi wote kutoka kwenye laptop yangu na kumpa kwenye flash na kumwomba azingatie maadili kabla hajaitoa aende akapate uhakika kwa kuwauliza wahusika na wakikanusha awambie anao ushahidi alifurahia sana na kuniahidi habari hiyo atawapa na mwana halisi,raia mwema na baadhi ya magazeti ya kiingereza ili ujumbe uwafikie walengwa kiurahisi.

  Baada ya kuachana alienda kufanya kazi yake kama kawaida lakini baadaye nikaona kimya na nilipompigia simu akaanza longolongo nyingi sana zisizo na mwelekeo ndipo nikagundua alipewa hela ndefu na baadhi na kigogo mmoja wa kampuni ambaye ni mkenya ili afunge mdomo na pia alinitaja mimi kuwa ndiyo niliyempa habari ile na hivyo iliniletea uhasama na baadhi ya wenzangu kwenye Management kwamba sijatunza siri kwa masilahi ya Kampuni.

  Na habari hiyo haijawahi kutoka mpaka leo.

  Nilitumia uzoefu wangu na kumchunguza kwa kina maana sikuamini kuwa anaweza kufanya kitu kama kile kwa kuzingatia nilitambulishwa kwake na mtu anayemfahamu na kumheshimu sana ndipo nilingua mambo kadhaa ikiwemo elimu yake alikuwa amefoji na hata kubadili jina ili liendane na vyeti alivyotumia na ni mtu wa kujipendekeza kwa watu wenye madaraka mbalimbali na fedha na kwa muda mrefu alitumika na aliyekua mgombea ubunge kupitia ccm aliyeshindwa Batilda Buriani na alikula hela ya kutosha na hasa kipindi cha kura za maoni alitumika sana kumuunganisha Burian na watu ambao walimpiga vita Felex Mrema atupwe kwenye kura za maoni na ana ushawishi mkubwa sana kwa wenzake.

  Kuanzia hapo nikakaa kimya na kunifanya niwaogope sana waandishi wa habari na kutowaamini 75% yao kuwa ni waganga njaa na hawana muda wa kuwaelimisha wananchi na badala yake wanatumiwa na mafisadi kulinda masilahi ya wachache.
   
 2. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Du pole ndivyo walivyo. Lakini ingependeza kama ungemtaja na jina ili nasi tumfanyie uchakachuaji. Si wajua tena ukipenda kuchakachua, nawe kubali kuchakachuliwa japo kidogo.
   
 3. D

  Derimto JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nashukuru ndg. Yangu ila sidhani kama ni njia bora ya kumfanya aache hiyo tabia sanasana tutamvurugia ajira yake ambaye ndiyo kisu chake cha kukutana na watu wengi wanajijua na hata wengine huenda wako humu ndani wanafahamu hivi vimchezo vyao na njaa yetu wabongo imetuzidi sana kaka ndiyo maana tunafanya mambo ya aibu hivyo.
   
 4. birungi

  birungi JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kweli hajakutendea haki.
  kama umeshagundua kweli alifoji vyeti vyake hebu fanya mpango umchakachue.kwa sababu ye mwenyewe hana wema.
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Yeah, corruption has metastasized through all sectors of society in Tz! Basi tupe hiyo habari humu kwenye jf nobody atakuchakachua tena!
   
 6. D

  Derimto JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni kitu ninachokifikiria mara mbili ila natamani sana kama nitakipeleka kwa wabunge likafumuliwa huko maana kuna vitu vinafanyika nchi hii vinawasha masikio na huwezi kuamini kama vinatokea kwenye jamii yetu na serikali inajua inavikalia kimya kwa walinda wachache.
   
Loading...