Uchaguzi 2020 Mwandishi John Marwa wa Dar24 akamatwa kwa kumkashifu Naibu Waziri Mwita Waitara

nokwenumuya

Senior Member
Jun 29, 2019
107
250
Mwandishi John Marwa akamatwa na kunyimwa dhamana ya polisi kwa kumchafua naibu waziri Mwita Waitara

- Ni katika malumbano ya kisiasa katika kundi la whatsapp la jambo Tarime

- *Mpelelezi wake adai hawezi kumpa dhamana hadi amkamate mshitakiwa mwenzake ajulikanae kwa jina la David Gichogo
1591797417192.png

John Marwa ambaye ni mwandishi wa habari ameshikiliwa katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kilichopo Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni uliopo katika Jiji la Dar es Salaam kwa tuhuma za kumchafua Mbunge wa Jimbo la Ukonga na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mh. Mwita Mwikwabe Waitara katika malumbano ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 hususani katika Jimbo la Tarime Vijijini.

Malumbano hayo yaliyofanyika katika kundi la WhatsApp lijulikanalo kama Jambo Tarime lilipelekea Naibu Waziri Mwita Waitara kuwafungulia mashitaka Mtuhumiwa John Marwa na David Gichogo kwa makosa ya kumchafua kimtandao.

Juhudi za kumuwekea dhamana zimeshindikana baada ya mpelelezi wake kudai hawezi kumpa John Marwa dhamana hadi hapo atakapofanikiwa kumkamata David Gichogo ambaye bado hajapatikana, jambo ambalo sio sahihi kisheria.

Kando ya uandishi wa HABARI, John Marwa pia ni mwanachama wa ACT-Wazalendo hivyo huenda mabishano yalitokana na minyukano ya kisiasa kwa sababu wanatoka katika vyama tofauti vya kisasa.

Juhudi zinaendelea kufanyika kupitia kwa wakili wa John Marwa na kwa viongozi wa Jeshi la Polisi ili kuhakikisha haki ya dhamana inapatikana kwa John Marwa maana makosa anayotuhumiwa nayo yana dhaminika.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusu jambo hilo kadri linavyoendelea ila kwa sasa juhudi za kumuwekea dhamana bado zinaendelea kupitia Wakili wake.
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
15,604
2,000
Wewe unadhani waandishi wa habari nikama kundi lenu la chadema? Ukatukane kule hafu uje tukuchangie. Huo ujinga wa ngazi ya kulewa Faru John nakudai umetekwa upo chadema.

Waandishi tutakuwa na wewe penye haki, ila ukipewa vipesa ukatukana harafu useme tuwe pamoja hilo hatuko hivyo.

Wamsaidie walio mtuma, maana huwezi kusema huyu aliwahi kulala na mama yake ili apate ubunge, huo ni ujinga wa Faru John! Aende akathibitishe.
Acha ubwege wewe kama unajua huwa kuna vicent hutoka ina maana wewe ni kinara wa kupokea vicent ili kuitukana chadema, wewe mbona umepewa vicent kuitukana chadema nani yupo pamoja na wewe? hawezi kusema nini? Kama jambo ni la ukweli kwa nini asiseme kisa umekula vicent vya mwita waitara umeamua kujitoa fahamu zote ukazania watu hawajui Tabia zake
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
15,604
2,000
Mwita waitara hawezi kupata kura hata za shetani anachokwenda kufanya ni kupora jimbo kwa nguvu chini ya msaada wa Polisiccm Tumeccm mkurugenziccm, hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu atamchagua waitara
 

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
27,199
2,000
Ni Mheshimiwa mmoja kavimba macho maana anashindia ulabu
Huo ulabu ndio hatari kwani ndio ukimwangusha anageuka mgomba vijana hubaki kula ndizi. Yaliwatokea baadhi ya viongozi wawili wa CCM huku znz vijana wakajilia ndizi . Hivi sasa hao viongozi ni marehemu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom