mwandishi huyu vp?

Shaycas

JF-Expert Member
Feb 13, 2009
906
110
Mkapa kalewa au kapotoka?
Na Mwandishi Maalum - Imechapwa
03 November 2010
Tafakuri
RAIS mstaafu Benjamin Mkapa si mtu
anayependa kusema au kuhojiwa,
lakini pale anapofanya hivyo huzua
kasheshe na kauli yake kulalamikiwa.
Katika mkutano wa mwisho wa
kampeni za Jakaya Kikwete, mgombea
urais kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Mkapa aliibuka na kushambulia
wapinzani wake wa kisiasa. Akiongea
kwa mbwembwe na tambo zilizozidi
mipaka, Mkapa alishambulia kila
mmoja.
Kwanza, Mkapa alisema vyama vya
upinzani havistahili kukabidhiwa
madaraka ya dola kwa sababu
vinahubiri udini. Pili, Mkapa alijitosa
kutetea Mwenge wa uhuru.
Kwa wanaomfahamu Mkapa wameona
kuwa tabia yake haijabadilika hata
baada ya kukaa nje ya ulingo wa
kisiasa kwa miaka mitano sasa.
Bado amebaki Mkapa yule yule
mwenye tabia na hulka zilezile. Baadhi
yao wanasema, Mkapa utampenda pale
anaposoma hotuba yake kwenye
karatasi, maana watu husikia kwa
masikio na kutafakari kwa mioyo.
Lakini akihutubia bila karatasi, watu
husikia kwa masikio na mikono
huiweka kifuani kama ishara ya
kuomba Mungu awaepushe na maneno
yatakayotoka katika mdomo wake.
Hivyo ndivyo ilivyotokea Jumamosi
iliyopita wakati CCM wanahitimisha
kampeini zao katika viwanja vya
Jangwani, Dar es Salaam.
Wahenga husema, tabia haina dawa.
Naye Mkapa kwa kuwa ni mzee, bila
shaka amejaliwa mengi na pia kuna
mengine mengi ambayo ameyakosa.
Kwanza, nguvu yake ndiyo udhaifu
wake. Pili, ni mwelewa wa mambo
mengi, mwenye uwezo mkubwa wa
kujenga hoja, lakini pia huitumia
karama hii vibaya. Wengi
wanaomfahamu vema wanamwona
mwenye kiburi na majivuno mbele ya
wananchi.
Binafsi, nilibahatika kuongea na Mkapa
huko nyuma na kumuuliza ikiwa
alikuwa na marafiki wa aina yake hapa
nchini. Alinijibu hana kabisa rafiki
nchini.
Nilishangaa, maana nilidhani kwa
uzalendo wake anaodai kuwa nao,
alipaswa kuwa na marafiki wengi
ndani ya taifa lake.
Katika mkutano ule wa Jangwani,
Mkapa alisema mengi, yasiyo na
mpangilio na yaliosheheni hasira. Kwa
mfano, alituhumu watu aliodai
wanasambaza udini katika kampeni za
uchaguzi mkuu.
Matokeo yake, alipotosha hata maana
halisi ya kuomba kura kwa mgombea
na kimsingi kwa jinsi alivyoporomosha
shutuma, aliwaudhi hata
waliohudhuria, wasikilizaji na
waliokuwa wanamtazama.
Bila kujali kuwa yeye ni mzee wa taifa,
mlezi wa maadili mema katika taifa na
mhimili wa amani na utulivu, Mkapa
alilaani vyama vya upinzani na
wagombea wake, kama ‘mzee asiye na
busara.”
Alianza kwa kujeli. Akatamba kuwa
hajali hata kama wanaoeneza udini
wanavaa majoho ya namna gani.
Udini alioulaani ukageuka majoho
aliyoyalaani badala ya wavaa majoho
aliodai wanaeneza udini.
Lisemwalo lipo, kama halipo laja. Udini
katika uchaguzi unaenezwa kwa
kulaaniwa kuliko ukweli halisi.
Wanaodai kuna udini kama ilivyo kwa
Mkapa, wanasali katika makanisa na
misikitini.
Lakini sidhani kama kuna siku waliona
udini huko, wakausema na kuonya
kuwa utaangamiza taifa. Badala yake,
wananchi walishuhudia Mkapa
anayejifanya muumini mzuri wa dini
ya kikirsto, akitua Jangwani kukemea
wale alioita, “Wanaoeneza udini.”
Ni kwa sababu, marafiki wa Mkapa,
wakiwamo wanaotuhumiwa wakuu
wa ufisadi nchini wamekataliwa katika
uchaguzi wa mwaka huu. Ndiyo msingi
wa yeye na wenzake kujificha ndani
ya kwapa la tuhuma za udini.
Laana ya Mkapa kwa wanaoeneza
udini, haina uzito wowote kuliko laana
ya wananchi kwa ufisadi uliofanywa
katika kipindi cha utawala wake na
mwingine kwa mikono yake
mwenyewe.
Kwa mfano, nani asiyefahamu kuwa
katika ukwapuaji wa fedha uliofanywa
na kampuni ya Kagoda, Mkapa alikuwa
miongoni mwao?
Kila mmoja anajua kuwa mafisadi
wamelaaniwa katika misahafu yote ya
dini, na Mkapa kwa kuwa hajawahi
kukana kuhusika na ufisadi, anaweza
kuwa anakumbwa na laana hiyo.
Mkapa akawaita wale wanaopingana
na sera za CCM kuwa ni “kokoto.” Hulka
ya udikteta ni kuwageuza watu kuwa
vitu badala ya viumbe hai.
Kama kupingana na CCM ni kugeuka
kokoto, basi Mkapa ni zaidi ya kokoto,
maana ni yeye aliyeasisi upinzani wa
kweli wa sera za CCM pale alipozama
katika lindi la fikra za kibeberu na
kifisadi.
Mkapa amekuwa akilia anaonewa na
kudiriki hata kuomba huruma za
wenye majoho aliowalani pale
Jangwani. Ushahidi wa hili upo wazi.
Akiongea kana kwamba hana
kumbukumbu, Mkapa alisahau hata
alichowahi kukisema na hata
kukitenda huko nyuma.
Kwamba ni chini ya uongozi wake
ambapo sera ya udini ilianzishwa
ndani ya chama chake pale chama
hicho kilipoingiza Mahakama ya Kadhi
katika ilani yake ya uchaguzi.
Ilipodaiwa kuwa ni Mkapa alilalamika
pembeni akidai watesi wake hawajui
nini maana ya “dola.” Ni kiburi hicho
hicho kinachomfanya sasa,
kuwadharau wapinzani kwa kuwaita
wambea, waongo na kokoto.
Mmbeya ni yule anayeshindwa kueleza
fikra zake wazi na badala yake akaisha
kupika majungu pembeni.
Matokeo ya uchaguzi yanayoendelea
kutangazwa nchi nzima yanamsuta
Mkapa kwa sababu ni yeye aliyefunga
kampeni kwa matusi badala ya
kuwanyenyekea wapiga kura.
Si ajabu ni yeye aliye nyuma ya Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) sasa
kushinikiza kubadili matokeo ili laana
ya kukosa kura isimrudie maana wana
mtandao tayari wanadai
aliyewaharibia kampeini zao ni Mkapa.
Wanadai walianza peke yao na
walikuwa wanaenda vizuri bila
msaada wake, lakini kwa kitendo
chake cha kuwatukana wapiga kura
alitia dosari kubwa katika kampeini za
CCM.
Mkapa anapaswa kuelewa kuwa
wananchi wamebadilika, na kwamba
mtindo wa kiimla anaoutumia,
umepitwa na wakati. Hata utetezi
wake kwa Mwenge wa Uhuru hauna
nguvu kwa sababu, kazi ya Mwenge
wa Uhuru aliouasisi Baba wa taifa
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
ilikuwa ni kuleta nuru palipo na giza,
na matumaini mahali watu walipokata
tamaa.
Sambamba na jukumu hilo, Mwenge
ukachoma mabepari na wanyonyaji wa
raslimali za taifa. Lakini wakati huu,
mwenge unatumika kuzalisha mafisadi
na kuwalea.
Ni muhimu Mkapa akafahamu kuwa
Mwenge tunaoutaka ni ule wenye
uwezo wa kuchoma mafisadi
waliokwapua mabilioni yetu ya
shilingi, viwanda vya umma,
waliojiuzia nyumba za serikali na
wanaotumia raslimali za taifa
kuanzisha vitega uchumi vyao.
Mwenye wa aina hiyo, hautufai na
Mkapa anatakiwa kuelewa hivyo.
Gazeti toleo na. 213
0
 
Nitaimalizia kesho hiyo thread!!ila Mkapa yeye kama yeye anajua tabia zakiuandishi hivyo bado hutumia nguvu nyingi kujilinda na vyombo vya habari!kumbuka Rizi khan wakati yupo CNN.
 
Back
Top Bottom