Mwandishi Francis Godwin atoweka Iringa kuhofia maisha yake

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
mm.jpg


Mwandishi wa habari kulia Francis Godwin akiwa na marehemu Daudi Mwangosi (katikati) Enzi za uhai wake.

Ikumbukwe Godwin alikuwepo siku ya mauaji ya Mwangosi baada ya tukio alitaka kupiga picha mapolisi yakamtishia na mtutu wa bunduki akakimbia anaeleza kuwa kuna gari ilikuwa inamfuatilia nyuma ikiwa haina plate number. Ameamua kutoweka kusiko julikana kuhofia maisha yake kwani ana windwa na watu wasio taka kuambiwa ukweli mjini humo Iringa.
Ameandika kwenye mtandao wake Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima

Kabla ya kutoweka alipata tetesi kuwa anatafutwa na Polisi Iringa akaenda kujisalimisha


6
Kwa sababu za kiusalama ilikua picha yake isiwekwe hapa lakini yeye mwenyewe ameidhinisha iwekwe kwa sababu haogopi, Francis Godwin ni huyo mwenye nguo nyeusi.



Siku mbili baada ya kifo cha mwandishi mwenzao wa habari (Daudi Mwangosi) aliefariki kutokana na kulipukiwa na bomu akiwa mikononi mwa polisi waliokuwa wanatawanya wafuasi wa Chadema huko Iringa, mwandishi wa habari Francis Godwin ambae alikua rafiki wa marehemu amejisalimisha polisi kufata masharti ya taarifa iliyotolewa kwa yeye na wenzake wawili kusakwa na polisi.
Exclusive na millardayo.com namkariri Godwin akisema "kutokana na hali halisi ya kushuhudia tukio la mauaji ya Mwangosi, nilifukuziwa kwa nyuma na gari lisilokua na namba pia nilipofika nyumbani niliambiwa kuna watu walikuja kuniulizia lakini hawafahamiki, na taarifa zikatoka kwamba tunasakwa"
Kuhusu kujisalimisha, Godwin amesema aliamua kufanya huo uamuzi baada ya kusikia taarifa za kusakwa kwake pamoja na waandishi wengine wawili, jana (september 5) aliamua kujisalimisha mwenyewe Polisi akiwa amesindikizwa na waandishi wa habari kama hamsini ambapo baada ya kufika pale walikutana na kamishna wa makosa ya jinai Tanzania Robert Manumba ambae ilibidi ahoji polisi Iringa kama ni kweli wanamtafuta Godwin na wenzake.
.

Namkariri Godwin akisema "baada ya kumuuliza mmoja kati ya maofisa wake kama ni kweli wanamtafuta Godwin ofisa huyo alijiumauma na baadae akasema hatumtafuti, baada ya hapo waandishi wa habari tulisimama tukaondoka kwa sababu ya kutokubaliana na kilichotaka kuendelea kuhusu taarifa ya uchunguzi ya Manumba"
Kingine kilichoendelea baada ya hapo ni Club ya waandishi wa habari Iringa kuziomba redio mbalimbali za iringa ambazo zimekua zikirusha matangazo ya polisi jamii kusimamisha matangazo hayo ambapo wamiliki wa vyombo hivyo wamekubali ombi.
Francis Godwin ambae alikua karibu na marehemu Daudi Mwangosi muda mfupi kabla ya kuuwawa kwa bomu amesema "Nilijua kwamba mimi ni miongoni mwa waandishi watatu wanaotafutwa kwa sababu marehemu kabla ya kifo akiwa amekamatwa nilitaka kwenda kumuokoa pale lakini nilipokua namsogelea Daudi akaniambia Godwin mdogo wangu kimbia… wakati nakimbia kama hatua 20 mbele nyuma nageuka nasikia mlipuko mkubwa, kuangalia ni Wangosi amekufa na nilibahatika kupiga baadhi ya picha ambapo askari waliokuwepo walipoona narudi kwenye eneo hilo walinionyeshea bunduki ikabidi ninyooshe mikono juu kwamba jamani mimi nakuja kwa heri wakaniambia potea"

Godwin amesema baada ya kugeuka na kuanza kukimbia walianza kumfukuzia ila bahati nzuri gari yake ilikua mbali, baada ya kutishwa na polisi walipokwenda hospitali ulipopelekwa mwili wa marehemu ilibidi waanze kutoa mabango ya wanahabari yaliyobandikwa kwenye gari yao pamoja na kutoa namba za gari, alianza safari ya kuondoka lakini kuna gari zilikua zinamfukuzia kwa nyuma mpaka alipofika nje kidogo ya mji wa Iringa na kuingia mitaani ndio akafanikiwa kukimbia.
Kwenye sentensi ya mwisho Godwin anasema ameibiwa siri na askari mmoja ambae alimwambia kuhusu kutafutwa kwake yeye na waandishi wa habari awengine mbapo alimuonya kwamba msimamo na kauli aliokua ameutoa pamoja na ushahidi wa tukio la mauaji ndio vimefanya atafutwe.
 
bila sha hata sisi wanaJF tutatafutwa tu. NAJUA KUNA POLISI MKO HUMU NAWAAMBIA HATUWAOGOPI HATA KIDOGO. BORA KUFA UMESIMAMA KULIKO KUFA UMEPIGA MAGOTI MBELE YA ADUI
 
akija dar asijifiche pori la mabwepande..polisi wanapeleka watu kuwaua huko watambamba...
 
Hii ni sawa na kuwa mkimbizi ndani ya nchi yako...the best way ni kwenda ubalozi wa Uingereza, Marekani au ubalozi wa nchi yoyote inayozingatia demokrasia na kuomba hifadhi
 
Hana lolote huyu, yeye nae ni walewale tu, atakuwa kuna visiri anavimiliki, sasa wakuu wameamua kumficha tu, mengine visingizio tu, nae anasubiri ukuu wa wilaya huyu
 
Akome kutumika kisiasa Akimbilie kwenye ofisi za Chadema aliokuwa anawafanyia kazi zao.
 
godwin yuko njiani kuelekea Dar kwenye mkutano wa utpc hawezi kukimbia wakati yeye mwanaccm safi ambaye alikuwa akisubiri udc
 
ki ukweli hii taarifa inasikitisha sana tu kwani ukijaribu kuangalia yote haya ni dhahili shahili kuwa hawa polisi walikuwa na nia ya kuua then wafiche ukweli kutokana na kuwa walishaambiwa ya kuwa wahakikishe chama cha chadema ndo hakipati nafasi haata kidogo na wahakikishe pia kuwa chama hiki hakifanyi mambo ambayo yanawapendeza wananchi yap tuko pamoja kupinga udhalimu huu wa jeshi dhalimu la polisi hope one day things will be okey then hao polisi ndo watajua mbivu ni zipi na mbichi ni zipi forever and fo always is my greeting to u all
 
WATANZANIA TUMESHAAMUA KUWA MABADILIKO YA KWELI NI LEO LEO NA WALA HAYASUBIRI KESHO HIVYO HAPA HAKUNA BREKI TENA KUHUSU MABADILIKO NCHINI!!!

Hata siku moja hakuna mtu au mamlaka anaye / inyoweza KUZUIA JAMBO AMBALO WAKATI WAKE UMEWADIA katika fikra za Umma; ni swala la muda tu.

Na hili la kuanza kukimbizana na baadhi ya waandishi wa habari gizani nakuambieni Mzee Manumba, kwa heshima na taadhima yote, jambo hili huenda ikaleta taabu kidogo endapo jamii nasi kwa upande wetu tutakapoanza kuchagua 'wale tunaowafahamu fika' nao wakaanza kukimbizwa zaidi tena zaidi.

Vifo zaidi kamwe havitovumilika tena.


Haijawahi kutokea mtutu wa Bunduki ukazuia mabadiliko yanayotafutwa kwa nguvu ya Umma. Historia inakataa. Labda Tanzania iwe ya kwanza.
 
Anakimbia kivuli chake.
NGOROMIKO,Upo mwanachama mtiifu kwa CCM. Wewe na chama chako na wanaokitetea sala za watanzania na zitawalaani na vizazi vyenu ,nina hasira na nyie hadi nasikia kupasuka!
 
bila sha hata sisi wanaJF tutatafutwa tu. NAJUA KUNA POLISI MKO HUMU NAWAAMBIA HATUWAOGOPI HATA KIDOGO. BORA KUFA UMESIMAMA KULIKO KUFA UMEPIGA MAGOTI MBELE YA ADUI

me ndio siwaogopi kabisa hao vilaza.
 
Jifiche kamanda Godwin hawachelewi kukumaliza kwa sababu wanafahamu wewe ndio utakuwa shahidi kwenye tume yoyote itakayotaka kutafuta ukweli.
 
Riwaya ya Tuwa Saidi "Mkimbizi"...kumbe fiction huwa reality. Sikuamini kama haya yaweza tokea Tz miaka ile.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Haijawahi kutokea mtutu wa Bunduki ukazuia mabadiliko yanayotafutwa kwa nguvu ya Umma. Historia inakataa. Labda Tanzania iwe ya kwanza.

Na haitatotekea kamwe Kamanda, labda huo mtutu uwe unatumika kuung'oa udhalimu. Ila mtutu uzuie haki? No way!
 
Back
Top Bottom