Mwandishi atishiwa maisha kwa kuandika ukweli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandishi atishiwa maisha kwa kuandika ukweli!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rugemeleza, Oct 1, 2010.

 1. R

  Rugemeleza Verified User

  #1
  Oct 1, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Naomba niwajuze yale yanayoendelea na kuwasibu wenzetu wanaoitakia mema nchi yetu.
  Habari hii nimeisoma kwenye mtungo wa Francis Godwin
  September 30, 2010

  SITAZIBWA MDOMO KWA VITISHO ,NIPO TAYARI KUFA KWA KUSEMA KWELI DAIMA........


  [​IMG] Mmiliki wa mtandao huu Bw Francis Godwin
  [​IMG]
  UPO usemi kuwa ukitaka kazi ya jeshi usiogope kufa na siku zote mkweli hutengwa wa waongo kama hivyo ndivyo basi kwa mara ya kwanza leo kwanza ninapenda kuanza kumshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ambaye amepata kunileta duniani na kuniongoza kwa kila jambo na kunilinda na maadui wangu kwa kuwapa roho ya upendo na huruma mwingi.

  Pia napenda kuwapongeza wanahabari wenzangu wote wa Tanzania ambao tumekuwa nao bega kwa bega katika kuipasha habari jamii ya kitanzania kulingana na uwezo wetu kweli nawapongeza wote bila kuwasahau wakurungezi wenzangu ambao tunamiliki vyombo vyetu yaani Blog na Website .

  mimi Francis Godwin kama mmiliki wa mtandao huu na mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima napenda kutumia uwanja wangu huu wa kujidai kueleza masikitiko yangu kwa wale wote ambao wameendelea kunipigia simu za vitisho kuhusiana na habari hii chini ya japo sijapokea simu ya wahusika wenyewe ila wapambe wa nje wameendelea kuwa na nguvu hata kutoa vitisho dhidi yangu kuwa iwapo nitaendelea kujifanya mkweli siku zangu zinahesabika .

  Napenda kupingana na wote walionipigia simu nakutoa vitisho kama hivyo huku nikiamini kuwa kifo kwangu ni mipango ya Mungu na sitoogopa wala kuingia katika dhambi ya kusema uongo kwa jambo la ukweli hivyo ni heri kuteswa hata kufa kwa kusema ukweli kuliko kuliangamiza taifa langu kwa kuendekeza rushwa na kusema uongo kwa faida ya wachache .


  Pia ninapenda utambue kuwa habari hii iliyopewa nafasi ya mbele katika gazeti la Tanzania Daima la leo na katika mtandao huu ndiyo ambayo imeonekana watu hata wale ambao ni rafiki zangu wakubwa na viongozi wangu ninao waheshimu zaidi kuninyoshea vidole na bila uchunguzi wakinituhumu kuwa mimi ni Chadema japo si dhambi kuwa chadema wala chama chochote cha siasa kwa mtanzania ila ni vema watambue kuwa mimi ni kada wa CCM na nimepata kugombea ubunge kupitia CCM na hapa nilipo ni mjumbe wa halmashauri ya CCM wilaya ya Iringa vijijini japo taaluma yangu haina chama ,dini wala kabila.

  HII NI CHANZO
  MTOTO wa mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Jakaya mrisho Kikwete ,Ridhiwan Kikwete jana ameonja joto la jiwe katika ziara zake za kampeni ndani ya CCM baada ya kutimuliwa mbio zaidi ya mara moja wakati akitaka kufanya kampeni za CCM katika taasisi za umma.

  Ridhiwani ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la umoja wa vijana wa chama cha mapindunzi (UVCCM) Taifa akiwa na viongozi akiwemo aliyekuwa mshindi wa kura za maoni jimbo la Iringa mjini Frederick Mwakalebela na washiriki wengine wa kura za maoni kama Jescar Msambatavangu walifika katika shule ya msingi Ipogolo wakitaka kukutana na vijana wa eneo hilo ili mjumbe huyo aweze kumuunganisha mgombea ubunge wa jimbo hilo Monica Mbega na Mwakalebela japo mkakati huo uligonga ukuta.

  Kabla ya msafara wa Ridhiwan kufika shuleni hapo kwa ajili ya kikao chake cha ndani ya vijana wa CCM kwa lengo la kuvunja makundi ndani ya chama hicho ,aliyekuwa mmoja kati ya wana CCM 12 walioingia katika kinyang'anyiro cha ubunge jimbo hilo Msambatavangu alipita mitaani kujaribu kuwaomba vijana kwenda kumsikiliza mtoto huyo wa Rais Kikwete japo waligoma kwa madai kuwa hawadanganyiki na ujio wake.

  Hata hivyo baada ya vijana hao wa vijiweni kugoma kwenda katika shule hiyo kwa ajili ya kutana na mjumbe huyo kwenye chumba cha darasa la pili katika shule hiyo ya msingi Ipogolo bado msafara huo uliweza kufika katika eneo hilo kwa ajili ya mkutano japo idadi ya vijana waliokuwa wamefika ilikuwa ni kama vijana 10 pekee.

  Mwandishi wa habari hizi alishuhudia mvutano mkubwa ndani ya ofisi ya mkuu wa shule hiyo Amani Mkeremi kati ya viongozi wa UVCCM mkoa walioongozwa na katibu wao mkoa Rhoda George na wale wa vyama vya upinzani walioongozwa na katibu kata ya Kitwiru Baraka Kimata (Chadema) wakivutana juu ya CCM kuzuia wanafunzi kuendelea na masomo kwa ajili ya kampeni za uchaguzi.

  Tukio hilo ambalo lilitokea majira ya saa 7 mchana lilipelekea mkuu wa shule kupata wakati mgumu kulitolea ufafanuzi huku walimu wake wakijifungia ofisini kukwepa vurugu iwapo vingejitokeza kati ya wafuasi hao.

  Akielezea juu ya tukio hilo kiongozi wa vijana hao wa upinzani Kimata alisema kuwa walilazimika kuweka mtego katika shule hiyo baada ya kuona heka heka za makada wa CCM hazipungui shuleni hapo na wanafunzi wakirudishwa nyumbani kwa madai kuwa shuleni kuna ugeni wa kitaifa yaani mtoto wa Rais anatembelea shule hiyo.

  "Kweli sheria ya tume ya uchaguzi inakataza taasisi za umma kuingia katika kampeni ....sasa tulipatwa na wakati mgumu kuona CCM inatumia shule ya msingi kufanya kampeni ndio sababu ya kuweka ulinzi ili kuhakikisha sheria haivunjwe ....tunashukuru tumefanikiwa baada ya viongozi hao wa CCM kumkimbiza mgeni wao mtoto wa Rais Kikwete" alisema kada huyo wa upinzani.

  Hata hivyo alisema kuwa kabla ya msafara wa Ridhiwan kukimbizwa shuleni hapo kulikuwa kumetokea mvutano ndani ya ofisi ya mkuu wa shule huku akitaka watu wa CCM wabaki ndani na wale wa upinzani watoke nje kwanza ila baada ya kuonekana kuwa wale wa upinzani ndio walifika mapema CCM waliamua kutoka na kutoonekana kabisa eneo hilo.

  Hata hivyo alisema kuwa wao wameelekeza tuhuma zao kwa mkuu wa shule hiyo ambaye amekuwa akionyesha ukada wake wazi wazi dhidi ya CCM hata kuruhusu shule hiyo kugeuzwa jukwaa la siasa kwa CCM.

  Kwa upande wake mkuu huyo wa shule alikiri kuwa yeye ni kada mzuri wa CCM na kuwa taarifa ambazo CCM walikuwa wamefikisha shuleni hapo ni kuomba eneo la kufanya kikao na mgeni wao sio kufanya kampeni na kukusanya vijana kama ilivyokuwa.

  Hata hivyo alisema kuwa hana barua yeyote ya CCM kuomba darasa na eneo hilo la shule kwa ajili ya kufanya kampeni wala juu ya ugeni huo.

  Katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Rhoda ambaye ndiye alikuwa mwenyeji wa Kikwete katika shule hiyo alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi hakuweza kupokea zaidi ya kukata .

  Hata hivyo mmoja kati ya makada waliopo katika msafara huo wa mtoto wa Kikwete alisema kuwa kikao hicho kilikuwa maalum kwa ajili ya kampeni za wagombea wa CCM kupitia vijana hao pia kuweza kumuunganisha Mbega na Mwakalebela kwa vijana hao ambao wameendelea kupinga CCM kumsimamisha Mbega .

  Kada huyo alisema kuwa pamoja na kufukuzwa na vijana hao wa Chadema katika shule hiyo ya msingi pia uongozi wa chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha ulizuia majengo yake kutumiwa na CCM kwa kampeni hizo.

  NINI KINAENDELEA CCM
  MVUTANO wajitokeza sakata la msafara wa mtoto wa mgombea urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Kikwete kuzuiwa na vijana wa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) kufanya kampeni katika shule ya msingi Ipogolo kinyume na sheria za tume ya taifa ya Uchaguzi .
  Mvutano huo umekuja siku moja baada ya mtoto huyo wa Kikwete ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya baraza kuu la umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) Taifa Ridhiwan Kikwete na msafara wake kukwama kufanya kampeni katika shule hiyo pamoja na uongozi wa shule hiyo kupitia mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Ipogolo Aman Mkeremi kueleza wazi kuwa UVCCM ngazi ya kata waliomba darasa moja katika shule hiyo kwa ajili ya kukutana na vijana kwa ajili ya mambo yao.
  Ufafanuzi wa Mjumbe huyo mbele ya waandishi wa habari leo ofisi ya CCM Iringa mjini ni kuhusiana na tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na mwandishi wa habari hizi jana na wanahabari wengine ,unaonyesha wazi kuwa UVCCM imemgeuka mkuu huyu wa shule baada ya kudai kuwa hakuna aliyeomba kufanya kampeni katika shule hiyo zaidi ya msafara huo kusimama kwa muda shuleni hapo kwa ajili ya kuuliza eneo lilolokuwa limeandaliwa kwa ajili ya mkutano huo.
  “ Ni ukweli sisi kati ya vikao vyetu tulikuwa na kikao chetu ndani ya kata ya Ruaha …tulifanya kama wenzetu walivyotuambia na kuelekea katika eneo la mkutano ila tulipofika eneo hilo ipo shule moja ya msingi na ndipo tulipokutana na wenzetu ndani ya kata ya ruaha wakiwa katika eneo hilo la shule huku wakiwa na wanafunzi wamevalia vizuri masweta ya kijana ishara ya chama chetu …na kama mnavyojua kuwa chame chetu sisi ndio wasimamizi wakubwa wa amani hivyo ingekuwa si busara kwetu sisi kama tungeshuka kwenda kufanya mkutano katika shule hiyo”alisema
  Kuwa kutokana na hali hiyo yeye na viongozi wenzake walikaa ndani ya gari huku wale wa mkoa wakiongozwa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa ndio walioshuka kwenda katika shule hiyo kuuliza na baada ya hapo waliondoka kwenda eneo la mkutano waliloelekeza .
  Hata hivyo pamoja na mjumbe huyo kupinga kuandaliwa mkutano katika shule hiyo mkuu wa shule hiyo Mkeremi aliwaeleza viongozi wa Chadema na waandishi wa habari kuwa darasa moja ndilo ambalo liliombwa na vijana hao wa CCM kwa ajili ya kufanya kikao chao .
  Wakati huo huo Ridhiwan Kikwete amesema njaa ya matumbo imeendeleza makundi yaliyotokana na kura za maoni katika jimbo la Iringa Mjini na kumpa wakati mgumu mgombea wao ubunge Monica Mbega ambaye ni mgombea ubunge wa CCM jimbo hilo la Iringa mjini.  Alisema katika ziara yake hiyo jimbo hilo alichojifunza katika kampeni ni kwamba baadhi ya wanaCCM wanaendelea kulea na kushabikia makundi kwa faida ya matumbo yao.  “wanaCCM hao hawana budi kufahamu kwamba CCM kama chama kinatetea maisha ya watu na wala hakitakuwa tayari kutetea matumbo ya watu na ndio maana wameendelea kuwasihi wanaCCM wa aina hiyo waache tamaa na matarajio waliyokuwa nayo kutoka kwa wagombea ambao hawakupata nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho”  “Ndio maana tangu kampeni zianze viongozi mbalimbali wa kitaifa kwa kuijua hali hiyo wamekuja mjini hapa na kufanya vikao na wanaCCM ili kuwasihi watangulize maslai ya chama kwanza na watu baadaye kama kauli mbiu yetu ya kukijenga chama inavyosema chama kwanza mtu baadaye,” alisema.


  Nimelazmika kuambatanisha na habari hizo ili kutoa nafasi kwa yeyote anayelalamika kuchukua hatua za kisheria badala ya kunitishia kifo ,ambacho kimsingi hupangwa na Mungu pekee.

  Napenda ifahamike hakuna hata mmoja wetu anayetambua siku zake za kuishi hapa duniani zaidi ya Mungu pekee hivyo sioni sababu ya mimi kuogopa kifo wala adhabu ya aina yeyote dhidi yangu .

  Mungu ubariki uchaguzi mkuu wa Tanzania umalizike kwa amani na utulivu Amina
   
 2. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  Haha haaa hawataki umwandike Uday Saddam Hussein al-Tikriti wa Bagamoyo a.k.a Riziwani. Waambie uma wa Watanzania umewachoka. Rais mwenye mawazo ya kimatonya matonya hafiri hata siku moja jambo la maaana..............
   
 3. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mimi Namshauri Ndugu Godwin alipeleke hili suala katika Mamlaka Husika, aende Polisi akafungue kesi ya Kutishiwa Maisha, vile vile Aende TCRA maana wanahusika na Usajili wa Simu, tunaamini namba zote za simu zimesajiliwa ili kupunguza mambo kama hayo. Ndugu Godwin maana unazo namba za waliokupigia nakushauri nenda mbele hawa watu wanafahamika
   
 4. akashube

  akashube JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2010
  Joined: Dec 24, 2009
  Messages: 411
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  UMRI ni kitu cha kuzingatia sana. Huu uchafu wa Ridhiwani unamharibia sana Kinana kazi aliyopewa na CCM. Ridhiwani anaendesha kampeni kitoto mno.

  Lakini niulize swali......hivi aliyesema kuwa serikali ni Kikwete na familia yake nani?

  Ridhiwani usijeanzisha jambo usiloweza kulimaliza. Kizazi alichopita baba yako sio hiki unachopita wewe........tunaweka record. Hata hao watishaji ni binadamu tu kama sisi.

  Nchi hii ikilipuka....hakutakuwa na mfano dunia nzima kwa jinsi itakavyobomokea mbali, hata somalia ina afadhali. 'mtoto wa geti kali akidata anadata kweli, hapindi ananyongorota' ...hapa mliokaa nje ya nchi muda mrefu tusameheane.....message sent.
   
 5. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Godwine, kama wewe ni member hapa au kama ukisoma hii post, tuwasiliane mkuu. Hii case yako ni kubwa sana.
   
 6. Mantissa

  Mantissa JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2010
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Godwin eeee! kila ambaye pua yake imeinamia chini lazima afe. Sasa kama kuna mpumbavu wa kutishia maisha wenzake, akome.

  Kifo ni lazima, Tumia taaluma yako, lakini pia naomba ufungue kesi mahakamani.
   
Loading...