Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,744
- 25,445
GEITA.
Jeshi la Polisi mkoani Geita linamsaka mwandishi wa habari wa moja ya kituo cha runinga hapa nchini, kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Emaco iliyopo mjini Geita.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 12 kabla ya kubakwa alirubuniwa kwa vitu mbalimbali ikiwamo simu ya mkononi.
Amesema mtuhumiwa amekuwa akimrubuni mtoto huyo kwa kumnunulia manukato, simu ikiwa na ‘line’iliyosajiliwa kwa jina la mwandishi huyo pamoja na kumpa fedha.
“Tukio hili la ubakaji unapaswa kulishughulikia kwa umakini mkubwa ukilikosa unaharibu ushahidi wote. Huyu ni mtoto mdogo na tumejitahidi kukusanya ushahidi wote ili tukifika mahakamani haki iweze kutendeka bila kuacha shaka”amesema Mwaibambe.
©Mwananchi