Mwandishi anapoomba safari za kwenda UN, Seriously!

Inasikitisha sana kusikiliza maswali yanayoulizwa na Waandishi. Unauonaje uraisi? Tupewe safari za UN, tupewe nafasi ya matangazo? Kweli?

Wametanguliza maslahi yao zaidi si maslahi ya taifa.

Ndiyo maana wanataka mgao wa pesa kama bunge na mahakama. Wanahitaji kujua watahusishwaje kwenye Corona pia hawajioni kwenye mpango wa miaka 5 wa serikali.

Sera ya vijana kuwaengua wao kwenye teuzi na wao CCM hoyeee kuachwa nje ya teuzi.

Pathetic!
 
Hatuna waandishi wa Habari

tunawachumia tumbo tu,
Fikilia anayejiita eti mhariri

D,Balile,
anapata nafasi ya kumuuliza maswali Raisi wa Nchi anashindwa kuuliza swali hata la wale wabunge wa gareji kina Mdee na genge lake kweli?
 
Naomba uniorodheshee maslahi ya taifa mkuu. Nna mtihani kesho. Shukrani

Uli truncate bandiko langu sheikh ungeli lirejelea kwanza.

Hitajio la uwepo wa katiba mpya, kuheshimiwa kwa haki, uhuru wa watu na utawala wa sheria hayawezi kuwa maslahi binafsi.

Jambo lolote ambalo kibinafsi walenga kujipatia fursa zaidi mbele ya rais hilo liko fyongo.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Hitajio la uwepo wa katiba mpya, kuheshimiwa kwa haki, uhuru wa watu na utawala wa sheria hayawezi kuwa maslahi binafsi...
Nafikiri kabla ya katiba mpya tungepata kuainisha hizo maslahi za taifa kwanza maana hazijulikani huwa tunaishia tu kusema "kwa maslahi ya taifa" je ni ardhi dhahabu tanzanite usalama wa nchi au?

Yaani kuwe na kitu kinacho julikana ukisema maslahi ya taifa hata dogo wa kayumba std 5 na zile fm akademia wnasema jibu 1 mkuu.
 
Sasa
Matangazo mpaka upigiwe pande? Wajiongeze ili wateja waende kwao sio mpaka Boss aseme?
Wateja wataendaje wakati kanun zilibadilishwa kimya kimya ili matangazo ya serikali yasiende kwenye vyombo binafsi?? Unaona hiyo billion nane wanayoudai serikali kuwa n ndogo?
 
Back
Top Bottom