Mwandishi amchoma Mahanga mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwandishi amchoma Mahanga mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by engmtolera, Mar 16, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  MWANDISHI wa Habari wa gazeti la Mwananchi, Aziza Masoud ameieleza Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwa, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Milton Mahanga alikamatwa na sanduku la kupigia kura kabla ya kutangazwa kwa matokeo.

  Aziza alidai hayo jana wakati akitoa ushahidi katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 wa Jimbo la Segerea yaliyomtangaza Dk. Mahanga kuwa mshindi.

  Aziza alidai kuwa, Novemba mosi mwaka 2010 alipokea simu kutoka kwa mawakala wa kuhesabu kura ambao hawakutaja majina yao, wakidai Mahanga amekamatwa na polisi katika eneo la Buguruni akiwa na masanduku hayo.

  Alidai kuwa baada ya kupata taarifa hizo, alizungumza na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai wanalifanyia kazi na watatoa taarifa kwa wagombea wa jimbo hilo.

  Awali Wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatara alipomuuliza Aziza kuwa aliripoti habari gani za uchaguzi katika jimbo la Segerea? Na Aziza alidai, Novemba 2 mwaka 2010 aliripoti habari ya mgombea ubunge wa jimbo hilo kukutwa na sanduku la kupigia kura lakini hakutaja jina la mgombea wa chama chake.

  Mahakama ilipomtaka ataje jina la mgombea huyo bila kuogopa, Aziza alidai ni aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Segerea Dk. Makongoro Mahanga.

  Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Jerome Msemwa, uliuliza kwa nini alipopata taarifa za kukamatwa kwa Mahanga hakupiga simu kwa Kamanda wa Polisi kuuliza na kwanini hakuwataja watu waliompa taarifa?

  Aziza alidai kuwa, baada ya kupata taarifa alimpigia Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ambaye alimwambia ofisi yake bado haijapata taarifa hizo, ndipo wakati akiwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Fuime , mwandishi wa habari ambaye hakumbuki jina lake aliuliza swali hilo na Fuime kuthibitisha.

  Aliendelea kudai kuwa, maadili ya uandishi wa habari yanaruhusu kumlinda mtoa taarifa endapo hakutaka kutajwa jina au kama anaweza kupata matatizo kutokana na taarifa hiyo na kuongeza kuwa, hata katika habari aliyoiandika hakumtaja Dk. Mahanga wala chama chake.

  Aziza alidai kuwa, endapo mwandishi anaandika habari kama hizo, jina la mtoa taarifa linahifadhiwa ofisini ili msomaji asilijue lakini unaweza kulitaja endapo mtu atatoa sababu za kisheria.

  Novemba mwaka juzi Mpendazoe alifungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo ambayo yalimtangaza Mbunge wa sasa Dk. Mahanga kuwa ndiye mshindi kwa sababu uchaguzi huo ulikiuka matakwa ya sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010..

  Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Dk. Mahanga, wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.

  Chanzo; HABARILEO
   
 2. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Tuseme nini basi!!!! Mpendazoe kaa mkao wa kula Mahanga ajiandae kuachia utukufu na arudi kijiweni kama watu wengine akauze genge
   
 3. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mahanga kwenye kesi hii naona maji hayako shingoni tena bali yameshavuka pua karibu yanafunika mwili wote.
   
 4. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ukiona HABARI LEO wameandika basi kuna kitu
   
 5. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Chadema anzeni kupasha jimbo hilo la kwetu.....
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sijui Mahanga atavukaje hiki kizingiti? Watu wake walishikwa 'live' wakiwa na hot-pot zilizojaa makaratasi ya kura wakijidai kuwa wameleta chakula cha wahesabu kura!
   
 7. Q

  Qedalong Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM matumbo moto
   
 8. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  habari leo?.
   
 9. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Naona hali inazidi kuwa mbaya kwa Mahanga,wasi wasi wangu ni jaji anayesikiliza hiyo kesi
   
 10. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Naona hali inazidi kuwa mbaya kwa Mahanga,wasi wasi wangu ni jaji anayesikiliza hiyo kesi
   
 11. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mimi hata siamini hawa wanasheria wetu, wanavyopindua pindua sheria! Ila kusema kweli wanasheria nao wanachangia sana kuturudisha nyuma!!
   
 12. N

  Naytsory JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 1,590
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tunamwomba mwenyenzi Mungu aanike uovu wote unaofanywa ndani ya nchi hii. Maana haki nyingi za watu zime/zinadhulumiwa.
   
 13. m

  mbwagison Member

  #13
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makongoro a.k.a masupu, ogelea! ogelea! piga mbizi! ama kweli za mwizi 40.
   
 14. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Na sakata hili litakuwa moja ya kigezo muhimu katika kupima haki. Je, Jaji atatoa hukumu stahiki bila kujali/kushinikizwa na muhimili mwingine. Ngoja tuzidi kufatilia kwa ukaribu zaidi.
   
 15. B

  Baikoko Senior Member

  #15
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Labda Baba M anaandaa mazingira ya kumpumzisha
   
 16. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hii nayo kali mkuu, inabidi kutafutiwa namna ya kuieleza mahakama!! Kama majaji watasimamia haki, viongozi wengi wa chama tawala wazeekea jela hapo mbeleni!!
   
 17. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mpendazoe alishinda makongoro akachakachua, lakini huyu jaji profesa juma c rafiki wa kikwete c atachakachua!
   
 18. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu, Ushahidi wa hili ulipelekwa mahakamani?
   
 19. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Unayoyasema ni ya kweli mkuu, na hali halisi iliyotokea jimbo la SEGEREA 2010 wanasegerea hawatasahau, lakini tatizo la hizi mahakama ni pale mtu anaponyimwa haki yake si kwa kuwa sheria inamnyima, au kwa kuwa ushahidi haujitoshelezi bali ni kwa technicalities za kisheria.
  Sitashangaa sana huyu jaji akitoa hukumu not on the point of fact or law but kwa sababu ya technical mistake
   
 20. K

  Keil JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nina imani na Prof. Ibrahim Juma ... unless awe amebadilika mara baada ya kuteuliwa kuwa Jaji.
   
Loading...