Mwanayumba...

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,879
MWANAYUMBA (Inspired by Chege’s song – Mwanayumba)

Ilikuwa mwaka 2002 Desemba.

Nilikuwa kidato cha Sita katika shule moja ya kutwa huko Moshi mkoani Kilimanjaro. Nakumbuka tulivyokutana...nakumbuka kama ilikuwa jana.

Nakumbuka baba akiniambia nijiandae kumpeleka mdogo wangu hospitali KCMC kwa ajili ya kliniki ya ngozi. Ilikuwa ni siku yake ya kliniki. Kitengo hicho cha ngozi ndiyo kwanza kilikuwa kimeanzishwa na kilianza kuchukua umaarufu mkubwa hasa kwa wagonjwa waliokuwa wakitokea mikoa ya Karibu na Kilimanjaro. Ilikuwa ni ahueni kwa wagonjwa wengi kwani hawakuhitaji kwenda tena Muhimbili kwa ajili ya matibabu au kliniki tu ya ngozi.

Kesho yake tuliamka vizuri na tukiwa njiani mara akaanza kulalamika kwamba hatakutana na rafiki yake waliyekutana wakati wa kliniki iliyopita kwani hakuwa na uhakika kama walipangiwa tarehe moja ya kurudi. Nilipuuzia hilo na tukafika hospitali tukakuta foleni tayari hivyo kutufanya tuchukue namba 68.

Basi tukakaa kwenye mabenchi yale kila mtu na kitabu chake tunajisomea huku tukingoja zamu yake ifike. Mara ghafla nikamsikia mdogo wangu akiruka kwa furaha, "Yuleeee..." Sikumuelewa kwanza ila baada ya kutupa macho kuelekea mlango wa kuingilia ndipo nilipogundua kilichomtia mshawasha namna ile.

Ni binti mmoja mrembo, mchanganyiko wa kihabesh..si ndo Ethiopia huko??? sijui ila alikuwa binti mmoja mrembo, mwembamba kiasi, mrefu mwenye maumbile yenye kuelezeka. Binti kama kachorwa kisha kabanduliwa akapewa pumzi na uwezo wa kutembea. Kama picha ya darasani unayoweza kugusa na kusema hiki ni kiuno..na wanafunzi wakaelewa.

Walisalimiana kwa kukumbatiana kisha walikuja nilipokuwa nimeketi akanisalimia. Akajitambulisha, tabasamu lake...

Binti yule alienda kujiandikisha na kupewa namba 74 na kisha kuja kukaa na sisi. Tukaanza kuongea na kupiga hadithi za hapa na pale. Moyoni tayari nilishavutiwa na binti huyu ila sikuwa na jinsi hasa kwa sababu ya mdogo wangu lakini pia kwa sababu sikuwa namfahamu vilivyo. Nilikuwa mvumilivu nikiendelea kummezea mate bila utatuzi wa kiu yangu.

Ulifika muda wa mdogo wangu kwenda kumuona daktari kwani namba yake ilikuwa imefikiwa. Na hapo ndipo nilipouona muda wa wokovu wangu umefika. Nikajisogeza panapo kisima walau niweze kuchota maji kuridhisha kiu yangu ya kutaka kumfahamu binti huyu wa Kihabeshi.

Nilitoa kidaftari changu kidogo nikamwambia na tucheze mchezo. Aniambie kuhusu yeye "Tell me about you" ni kama mchezo mmoja marufu wa STOP ukishindwa kubuni neno nakuuliza swali lolote kukuhusu na unatakiwa unipe jibu sahihi. Kiufupi niliweza kufahamu alikuwa Akiitwa Mwanayumba Salum. Mkazi wa Arusha nimesahau mahali ila ni karibu na soko mjinga kama sikosei baada ya uwanja wa mpira. Jamani Mwanayumba wangu, nikipata nauli nitakuja kukuulizia.

Mdogo wangu alitoka kwa daktari na baada ya kwenda kuchukua dawa tulitakiwa kuondoka ila alituomba tumngoje maana angetakiwa kungoja peke yake angejisikia mpweke. Tulimpa sharti moja kuwa endapo tungemngoja basi asingekuwa na budi kuja nyumbanikwetu kwanza kabla ya kurejea kwao Arusha. Alikubali!


Nasi bila hiyana tulimngoja na alipotoka tukaondoka wote kuja nyumbani. Nakumbuka siku ile tulikula wote ugali nyumbani kwetu, tena kutoka kwenye sahani moja.

fast forward...

Katika mchezo ule nilifanikiwa kuchukua namba yake ya simu (ilikuwa namba ya mama yake kama tu ambavyo na mimi nilikuwa nikitumia simu na namba ya mama yangu). Tulikuwa tukiwasiliana usiku. Ilikuwa mbinu ya kujua kama si mama mwenye simu lazima u-beep na mimi ni-beep ndo tunaanza kuwasiliana kwa jumbe za simu!

Kidogo tukazoeana na hisia zikaanza kukua. Nakumbuka yeye ndo alikuwa wa kwanza kuniambia ananipenda. Nikamwambia amejuaje hayo na kuna mengi sana ambayo tunatofautiana?

Najua siku hizi dunia imeshanichakachua ila kipindi kile niliamini na nilijua ukimpenda mtu ni lazima aje kuwa mkeo. Tulikuwa na dini tofauti na hata katika maongezi niliweza kujua kuwa wazazi wake walimbania sana, hasa baba yake. Baba yake alikuwa mtu wa dini sana. Aliniambia ameshafikiria yote hayo na yuko tayari hata kubadili dini. Sikutaka kufanya haraka kukubali hilo ingawa na mimi moyoni tayari niishamkubalia nafasi siku nyingi.

Tulipanga siku tuonane na mimi nikaamua ningeenda Arusha. Nilienda mwaka uliofuata, 2003, na tulikutana kama sikosei maeneo ya stendi..majina ya yale majengo yamenitoka kiasi ila kuna "jogoo" na "sabasaba"!?? Tulielekea kwenye 'geto' la kaka yako hata sijui ni wapi tena maana tulipita vichochoroni, tukakatisha soko (soko mjinga?) tukakuta uwanja ukanionesha kwa mbaaali nyumba yenu. Tuliongea sana siku ile...tukapanga mambo mengi ambayo kwa utoto wetu tuliona ni sahihi. Tukakubaliana kuwa pamoja kama zaidi ya marafiki. Nilirudi nyumbani kama mtu aliyezaliwa upya.

Sikujali kuwa nilikuwa nasubiria mitihani ya mwisho ya kidato cha sita au la! Ila furaha tu ya kuwa ndani ya penzi ilinizidi, ilikuwa raha isiyo kifani. Ulikuwa ukija mara kwa mara hata siku ambazo hauna kliniki ila sasa ilikuwa rahisi kumdanganya baba...basi tulionana sana na tukazoeana.

Nilifanya mtihani wa kumaliza elimu yangu ya sekondari kidato cha sita na kuanza kutafuta kazi ‘tempo’ mtaani. Nikajitahidi nikanunua kamobiteli changu. nikakupa kale ka mama alikokuwa ameacha kukatumia. Tukawa tunawasiliana mpaka usiku wa manane...Kwa hakika penzi letu lilikuwa tamu.

September 2003



Ilifika kipindi nikatakiwa kwenda chuo kuendelea na masomo. Nakumbuka kipindi hicho ndo ulikuwa unamalizia kidato cha nne. Nilitakiwa kwenda kusoma nje ya nchi. Ukataka kujua mstakabali wa uhusiano wetu.

Nakumbuka nilienda kumuuliza mama kwa kutumia mwamvuli wa rafiki yangu, Salva. Nikamwambia mama, “Rafiki yangu Salva ana rafiki yake wa kike anampenda sana ila binti huyo ni muislamu na amesema yuko tayari kubadili dini ili tu wawe wote.



Mama ni kama alikuwa akiongozwa na roho Mtakatifu kwani alinigeukia na kuniambia, "Mwanangu Mentor! angalia sana hao mabinti. Anaweza kusema lolote leo alimradi tu awe nawe. lakini mkishaoana akarudi kwenye dini yake utafanyaje? Utamuacha? Kumbuka haturuhusiwi kutalikiana!" Mh! maneno yale yaliniingia sana.

Kabla sijaondoka kwenda masomoni tulikutana Haria hotel Moshi pale double road nikamwambia, "Mwanayumba, mimi naenda kusoma lakini ukipata mwingine huku nyuma tafadhali endelea tu nisikuzuie!" Alilia sana Mwanayumba wangu siku ile. Hakujua kwanini nilimwambia vile ila ndo nilikuwa nampoteza Mwanayumba wangu. Sikujua! Alilia nikambembeleza ila sikutaka kumwambia nafanya vile kutokana na ushauri wa mama yangu.

Nilikwenda kusoma. Tuliwasiliana kwa muda mfupi baadaye gharama zikawa nyingi tukapunguza kuwasiliana. Mwanayumba ulinipa anuani yako ya barua pepe ila kila nikikutumia ujumbe haufiki. Huyu mjamaa anaitwa Mailer Daemon ananirudishia ujumbe wangu.

Mwanayumba nakumbuka tulikutana kipindi fulani pale Shoprite Arusha. Tuliongea sana Mwanayumba. Ukaniambia unafundisha sasa. Nadhani ilikuwa 2008. Ukanipa namba za simu. tukawasiliana kwa kipindi kile nilipokuwa nyumbani. Niliporudi shuleni tena nikapoteza line yangu ya Tanzania. Ndo ukawa mwisho wa mimi kukusikia na kuwasiliana na wewe.

Leo, December 10, 2012



Mwanayumba…umeenda wapi Mwanayumba? Mwanayumba ulikuwa binti niliyekupenda kuliko wote niliowahi kuwapenda. Mwanayumba, kila ninapokutana na vicheche vya jiji hili nakukumbuka binti wewe wa Kihabeshi. Popote mnioneapo Mwanayumba wangu mwambieni nampenda! Huenda alishaolewa sasa...ila atabaki kuwa Mwanayumba wangu, binti niliyempenda kuliko wote hadi sasa.


Wasalaam wapendwa,
Mentor.





MWANAYUMBA: PART II

Juni 2015

Ilikuwa siku ya Jumamosi, mwanzoni kabisa mwa mwezi huu wa sita. Nilikuwa nikiendesha gari kutokea baharini kwa kupitia njia hii ya kati ya Ikulu yetu ya Magogoni na Ikulu ndogo ya Zanzibar kama unaelekea hospitali ya Ocean Road. Safari yangu ilikuwa ikielekea Chuo cha Utalii. Nilipofika eneo la round about ile nikitaka kukunja kushoto kuendelea na safari yangu macho – yasiyo na pazia – yalielekea upande wa kulia ambapo kuna lango la kuingilia hospitali hiyo ya Ocean Road.


Niliiona sura ambayo ama kwa hakika haikuwa sura ngeni kabisa machoni pangu.

Itaendelea...
 
Last edited by a moderator:
Ishi zako kwa amani hapo Kigamboni Mentor! FYI Mwanayumba ndiye Catherine Magige ambaye ni mbunge wa kuteuliwa wa hapa Arusha, (just google her) kwenye jf anatambulika kama Catherine. Pole sana kwa kukubali ushauri just from mama... Mentor wewe...
 
Last edited by a moderator:
Wengi wamekutana na maswahibu kama yako. Ni wachache sana waliowaoa/olewa na wale waliowapenda sana! Pole sana Mkuu! Hiyo sasa ni historia. You cant change ila usikubali kuiishi.
 
Kwa heshima na taadhima,ilikuwa mwaka 2009,ndio naanza maisha nilienda moshi maeneo ya kiboroloni kumsalimia rafiki yangu MROMBO .kwa kweli hali ya hewa ya pale moshi ilinipa shida sana kwa kuwa sikuwahi kukaa sehemu yenye baridi kali kiasi kile niliyoikuta moshi,nakumbuka siku moja ya jumatano ya february 2009,tulitoka na rafiki yangu kwenda changbay karibu na magereza na wakati huo nilikuwa nimeanza kusumbuliwa na kifua,,nakumbuka ndio tulikuwa tumeingia ktk hiyo supermarket tulipomaliza tukawa tunaenda kumsalimia rafiki yetu manoah ambaye alikuwa anaishi shantytown kwa kuwa aliugua kichaa kwa karibu miezi 2 ndipo ghafla nikazidiwa na fahamu zikanitoka.nilipokuja kuzinduka nilijikuta nipo KCMC nimewekewa drip,nikaja kugundua nilikaa pale kwa muda wa siku 2 sijitambui na nilipofumbua macho kwa mbali nikaanza kuona watu ingawa sikuweza kuwatambua,baadae nikaja kuwatambua kuwa alikuwepo manoah MROMBO na wazazi wao wote pamoja na binti mmoja ambaye nilikuja kutambua kuwa ni mfanyakazi wa kina manoah,alikuwa amebeba mtoto mmoja mgongoni na alikuwa amevaa nguo za kawaida lakini hazikuweza kulificha umbo lake zuri na usoni nikaona tabasau lakini lenye huzuni na siri kubwa ndani yake.huyu binti ndie aliyekuwa akiniandalia chakula na kuniletea kutokana na ukaribu wa familia ya MROMBO na manoah walijikuta wanaishi zaidi ya undugu hasa katika matatizo.ilikuwa jumatatu tulivu,hali yangu ipo vizuri nasubiri kupewa ruhusa ya kutoka nikapata muda wa kukaa na yule mfanyakazi wa familia ya manoah..kwa kweli baada ya kuisoma hiyo stori yako nilishtuka kwa sababu naye alinieleza vivyohivyo.kilichotokea anasema akiwa arusha alikutana na kijana mmoja ambaye yupo ktk rika la utuuzima ukimwangalia kwa makini,alikuwa amekuja arusha ila sikuweza jua alikua ameenda kufanya nini na ndipo alipopata mimba na baada ya kumueleza yule kijana,yule kijana aliruka mita mia,na baada ya kugundulika kwao binti alifukuzwa na wazazi wake na ndugu walimtenga kwa sababu walikuwa watu wa dini na waliona huyo binti angewaharibia sifa yao,ndipo alipoenda alipokuwa anaishi yule kijana la kumbe alimkuta mwenyeji wake na akaambiwa kuwa jamaa alifungasha mizigo alfajiri na kuelekea bukoba kwao ingawa inasemekana hakwenda bukoba alienda dar,binti akaanza kutafuta kazi ndogondogo za kumuwezesha kuishi mjini huku akilala stand,akaja kujifungua mtoto ambaye alizaliwa njiti,na huyo mtoto wake wa kwanza nina wasiwasi na baba yake either ni Ruttashobolwa ama Bishanga ,ndipo alikuja kukutana na mwanaume mmoja aliyetokea kumpenda sasa alikuwa ametoka arusha na alikuwa moshi kwa huyo mwanaume, lakini aliishia kuzalishwa na huyo mwanaume mtoto wa pili na kuachwa,na alifukuzwa na huyo mwanaume na ndipo alipopata kazi kwa kina manoah. Kwa maelezo zaidi nipm ama muone manoah,anaweza kukupa direction
 
Last edited by a moderator:
Ndo matatizo ya kuwakumbuka wapenzi wenu wa zamani mkiwa mmekunywamo tu cérveja
 
kaka inabidi tu umsahau huyo mrembo Mwanayumba, kashakuwa mama mwenye nyumba huko kwingine.

Nimejaribu kumsahau ila jana usiku hisia zilinizidi...hasa baada ya shemeji/wifi yenu kuniboa jana jioni.

Huyu "Mwanayumba" atakuwa yupo humu humu JF!.
Yegomasika, pliz tel me this is true!

Ishi zako kwa amani hapo Kigamboni Mentor! FYI Mwanayumba ndiye Catherine Magige ambaye ni mbunge wa kuteuliwa wa hapa Arusha, (just google her) kwenye jf anatambulika kama Catherine. Pole sana kwa kukubali ushauri just from mama... Mentor wewe...
Arushaone, nisaidie tu majina sahihi ya hayo maeneo nataka disemba nije mwenyewe nimtafute. (af naona unantafutia bifu..haya tu... ujumbe: HATUACHANI)

Wengi wamekutana na maswahibu kama yako. Ni wachache sana waliowaoa/olewa na wale waliowapenda sana! Pole sana Mkuu! Hiyo sasa ni historia. You cant change ila usikubali kuiishi.

Nlikuwa nshaisahau ila si unajua kuna mengi yaonwayo na macho ila ni machache yafikayo moyoni..hili ni mojawapo!
 
Last edited by a moderator:
Ndo matatizo ya kuwakumbuka wapenzi wenu wa zamani mkiwa mmekunywamo tu cérveja
Chimbuvu, mh! sidhani...alikuwa binti mpole sana mtulivu asiye na papara na maisha...inawezekana kweli!?? manoah na MROMBO vipi hii hadithi ni real ama!??
Baba V..situmii kilevi chochote isipokuwa DOMPO once in a while..na jana i was very sober..at least i think i was!:confused2:
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom