Mwanawake humwachia nuksi/mikosi au kismati kwa mwanaume aliyetoka naye

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,628
6,669
Salamu wakuu

Ni muda sasa nimekuwa nikichunguza kwa upande wangu nimekuja gundua kwamba kuna wanawake ukijaribu kuchepuka nao mwisho wa siku hukuachia nuksi, gundu na mikosi kibao inaweza kukupata mwanaume.

Wanawake wengine wa hukuachia kismati tu, yaani ukitoka nae lazima mambo mazuri tu yakupate mfano utapata pesa nk

Hii imenikuta ni juzi tu siku ya valentine nilipojaribu kuchepuka na mwanamke mmoja hivi alikuwa ananifuatiliaga saaana! Kiukweli huyu mwanamke nachelea kusema kaniachia nuksi sijui ndio gundu au mikosi wakuu, yaaani tu ile siku nimeachana naye nikapata ajari ya bodaboda lakini sikupata majeraha.
Wakuu kibaya zaidi tangu siku hiyo pesa imepotea kabisa mfukoni mwangu!

Aisee huyu dada gundu kabisa. Vipi kwa wanaume wenzangu na hii kitu ishawakuta?

Tuwe makini sio kila mwanamke unayetoka nae atakuachia kismati wengine nuksi mjini hapa
 
huyu jamaa ni kilaza sana,sijui ana umri gani,yaani hadi aibu kujua kama ni mwanaume mwenzetu kwa huo utumbo..
 
Aiseeee!
Namba inasomwa hadi wanasingiziwa mademu, Magu legeza kidogo mtaani mambo si shwari

Kiujumla pesa haipatikani kwa sasa!
Hizi ni imani tu piga kazi mkuu pesa utapata
 
Salamu wakuu

Ni muda sasa nimekuwa nikichunguza kwa upande wangu nimekuja gundua kwamba kuna wanawake ukijaribu kuchepuka nao mwisho wa siku hukuachia nuksi, gundu na mikosi kibao inaweza kukupata mwanaume.

Wanawake wengine wa hukuachia kismati tu, yaani ukitoka nae lazima mambo mazuri tu yakupate mfano utapata pesa nk

Hii imenikuta ni juzi tu siku ya valentine nilipojaribu kuchepuka na mwanamke mmoja hivi alikuwa ananifuatiliaga saaana! Kiukweli huyu mwanamke nachelea kusema kaniachia nuksi sijui ndio gundu au mikosi wakuu, yaaani tu ile siku nimeachana naye nikapata ajari ya bodaboda lakini sikupata majeraha.
Wakuu kibaya zaidi tangu siku hiyo pesa imepotea kabisa mfukoni mwangu!

Aisee huyu dada gundu kabisa. Vipi kwa wanaume wenzangu na hii kitu ishawakuta?

Tuwe makini sio kila mwanamke unayetoka nae atakuachia kismati wengine nuksi mjini hapa
Kumbe we ni hako ndio unaita nuksi

Mwenzio alimaliza kuchepuka tyuuu
1. Akapigiwa cm kua kasimamishwa kazi
2. Ile hajakaa sawa akiwa anataharuki, akapokea simu duka lake limeungua hakijaokolewa kiti

3. Wakati anashangaaa hivi, ikaja samasi kuwa amejenga kwenye kiwanja cha mjane mmoja.

4. Huku akivuta subira, akapokea sms inayomjulisha kuwa akaunti yake ya benki ina matatizo, yawezekana kuna mtu kamtapeli.

KOMESHA YA YOTE, WAKATI ANAWAZA HAYO
YULE MCHEPUKA AKAMPIGIA KUWA AKITOKA P, ATAMJULISHA
 
Ile ni Dhambi ambayo ina ambatana na maagano.
Uliza madereva wa masafa watakuambia kuna sehemu singida ukigonga demu safari huwa nzito,kuharibikiwa,ajali na mara nyingine vifo.
 
Back
Top Bottom