Mwanaume wa miaka 50 ampaujauzito binti wa miaka 12 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume wa miaka 50 ampaujauzito binti wa miaka 12

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by lutayega, Jul 7, 2012.

 1. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,215
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Naandika habari hii nikiwa na masikitiko yaliyochanganyikana na hasira zilizopitiliza.Leo asubuhi baada ya kupata kifungua kinywa, nilanza kujiandaa kufua nguo zangu kama mnavyojua leo siku ya mapumziko, mara akatokea binti mmoja akiwa kabeba mtoto kama wa miaka 2 hivi. Nikamkaribisha na baada ya kusalimiana akaniuliza kamaanaweza kupata kazi yoyote ile, kabla sijamjibu nikaona anaishiwa nguvu akakaa chini ili kuepuka kuanguka. Ikabidi nimuulize kama anatatizo lolote lile la afya, akanijibu kuwa hajala toka janamchana, pia ikanibidi kumuuliza mtoto aliyembeba ni wa nani akanijibu kuwa ni mtoto wakekiukweli sikumwamini mpaka nilipoona anamnyonyesha kwasababu huyu binti kama ana umri mkubwa ni miaka 13. Ilibidi nimpatie chakula ili kupunguza njaana baada ya kula niliamua kumpatia kazi ya kufua nguo nilizokuwa nataka kuzifuaalipokuwa anafua alimuweka mtoto wake chini, mtotot huyo nipomwangalia alikuwa na upeleupelemwili mzima nikamuuliza mtoto wake anaumwa nini akanijibu kuwa mtoto anaumwa kaswende ambayo alizaliwa nayo, ndo akaanza kunisimulia kuwa akiwa ana miaka 9 kuna baba wa miaka kama 50alimwomba wawe na mahusiano ya mapenzi kwa makubaliano kuwa atamnunulia simu na cherehani pia atamwoa, hivyo binti alianza kumpa penzi huyo babu. Walidumu katika mahusiano hayo kwa mda wa miaka 2.Akiwa na miaka 12 alishika mimba na alivyomweleza huyo baba huyobaba aliikataa mimba na kuwambia kuwaakiendelea kumfuatilia au kumwambia mtu atamchinja. Baada ya wazazi wake kugundua kuwa ni mjamzito walimuuliza nani mhusika kwanza aligoma kuwambia lakini baada ya kupigwa na kulazwa juu ya mti kwa muda wa siku mbili aliamua kuwaeleza ukweli nao waliamua kumshitaki mhusika kwa mtendaji wa kijiji. Mhusika baada ya kuona anafuatiliwa alitoroka. Yule binti naye alifukuzwa kwao na mpaka anaponisimulia kisa hiki hana pakuishi na chakula chake ni pale anposaidiwa na wasamalia, pia mtoto wake anaumwa kaswende yeye kwa upande wake hafahamu kama ana kaswende au la.Kinachonitia hasira zaidi ni kwamba huyu baba aliyempa mimba ameshatoka mafichoni na hajachukuliwa hatua yoyotena hatoi huduma yoyote kwa huyu binti na kwa mtoto wake.Kutokana na hilo naomba msaada wa mawazo, wa kimatibabu na wa kisheria kumsaidia huyu binti. Nimemwambia aje jumamosi ijayoili niweze kumsaidia
   
 2. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Very depressing story! Msaidie Mungu atakuzidishia.
   
 3. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Umeconclude vizuri kua utamsaidia go ahead God will bless you!
   
 4. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,215
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  tunachotakiwa kufanya ni kutoa mawazo yatakazoyewezesha huyu binti kutatua tatizo la afya ya mtoto nayake mwenyewe pia kumsaidia kupata haki ya mtoto wake toka kwa huyu mwanaume dhalimu
   
 5. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mbaya sana hii
  1. Unamfahamu huyo mwaribifu?
  2. Wazazi wa huyo binti unawafahamu?
  3. Wewe ni wa jinsia gani?

  Fanya uchunguzi ujue huyo mwaribifu anakaa wapi ama anapatikana wapi.
  Ukishajua fika kwenye vyombo vya dola na ushirkiane na watu wa ustawi wa jamii karibu na mahali hapo
  Uchunguzi ufanyike ili kuthibitisha hayo madai. Then sheria ichukue mkondo wake.
  Kama unawajua wazazi wa huyo binti shirikisha hao watu wa ustawi wa jamii waelimishwe jukumu lao kwa mtoto wao hata kama keshatenda kosa. Waelewe kuwa mateso aliyokwisha yapata sio rahisi kurudia tena kosa.
  Watu wa ustawi wa jamii wasaidie kuhakikisha huyo mtoto na mtoto wake wanapata tiba stahiki!
  Wewe ukiwa kama mtu mzima unaweza kumsaidia kumhifadhi na kumpatia matibabu kama utapenda. Sasa hapo ndo nataka kujua jinsia yako maana kama ni mmbaba na hukai na familia inaweza kukuwia ngumu kidogo! Kwa mwanamke anaweza kumsaidia akitaka as they can share the even a single room.
  Tungependa tusikie jumamosi umemsaidia nini!
  Kila la kheri
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,699
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  Da huyu mzee noma!
   
 7. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mpeleke ustawi wa jamii akashtaki naimani watamsaidia sana
   
 8. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  alaniwe fataki
   
Loading...