Mwanaume wa Kitanzania yuko radhi kutumia Tshs laki 5 kufanya sherehe kumtoa mtoto siku ya 40 lakini si kununua vitu vya kujifungulia mkewe

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,596
3,639
Ni aibu iliyoje mtu unampa mimba mkeo au hawara yako kwa starehe zenu halafu unashindwa kuandaa mahitaji (vitu) ya/vya mama kujifungulia angalau elfu 50 tu ndani ya miezi 9 ya mimba.
Cha ajabu mtu huyo siku mtoto akitimiza siku 40 na anataka kumtoa nje atafanya sherehe ya Tshs laki 5 kwa ajili ya mtoto huyo. Hivi hizi ni akili au matope?
Hebu tubadilike jali mkeo au hawara yako uliyempa hiyo mimba. Tena wengine hizo mimba zimetungiwa Guest house ( chumba elfu 20, mkala chips kuku za elfu 10, ukampa hela ya sabuni elfu 20 kwa siku hiyo). Hivi kilawiki ukiamua kuweka akiba ya shilingi elfu 10 mpaka wiki 42 si utakuwa na shilingi laki 4? Kweli utashindwa kumhudumia mkeo mahitaji muhimu ya kujifungulia Hospitali? Aibu. Wanaume tubadilikelike
Screenshot_20190310-014015.jpeg
Screenshot_20190310-014029.jpeg
Screenshot_20190310-014043.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm ninachojua mke wangu anajiandaa kujifungua next 2 weeks, nimeshamnunulia kila kitu sitaki kusikia kitu BURE, najua bure aghali! Hata wahenga walishasema
 
Inategemea na makabila kwanza alafu mwanaume kuandaa shughuli ya kumtoa mtoto arobaini watu waje wacheze chura au? Hayo mambo ni ya kina mama wanawake ndo wana huo upuuzi ili watunzwe sasa me na midevu yangu namtoa mtoto arobain ili washkaji wanitunze au

Umeelewa topic? Vyovyote vile lakini lazima utatoa pesa ya huyo mtoto kufanyiwa sherehe. Je kweli utashindwa kuandaa mahitaji muhimu ya mkeo kujifungua?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm ninachojua mke wangu anajiandaa kujifungua next 2 weeks, nimeshamnunulia kila kitu sitaki kusikia kitu BURE, najua bure aghali! Hata wahenga walishasema
Ni vyema kujiandaa kuliko kusubiri vya bure.... Bure huleta tafrani

Ukiwawezesha wanawake umewezesha jamii
 
Umeelewa topic? Vyovyote vile lakini lazima utatoa pesa ya huyo mtoto kufanyiwa sherehe. Je kweli utashindwa kuandaa mahitaji muhimu ya mkeo kujifungua?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa huyo mwanamke kama ataona kipaumbele ni pesa ya sherehe ya mtoto huo upuuzi ni wa kwake kwa sababu sherehe ni mipango na mahitaj ya mtoto ni lazma mwana kulitaka mwana kulipewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa kuna zile maternity package zinazotolewa bure hosp, ni mkoba/mfuko unakuwa na vifaa vyote vya hosp ambao hutolewa bure hivyo mama atahitajika kununua khanga, beseni na vingine ambavyo si vya kitabibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha acheni ujinga, gloves zipo hospitali, ndoo na beseni yanini anajifungulia kwenye ndoo au hilo beseni?!
Kila siku tunasoma na kuona hospitali zimepewa vitanda vya kujifungulia, nyie mnanunua ndoo na mabeseni.
Yani hospitali gani haipati gloves mpaka mnunue?! Hospitali gani haipati au haina gauze mpaka mnunue?! Na hizo gauze na pamba mnazitumia wakati gani?!
Mwanamke anajifungua wanakata umbilical cord, placenta linatoka wanamsafisha kwa maji kwisha.
Mnajadili vitu gani na nyie?! Eti zitto naye yumo, angemuuliza Dr.Kugwangala au Dr.Ndugulile wange mueleza mazingira ya labor yako vipi na process iko vipi.
Jamani mmeshindwa kujadili issues mnajadili rushwa za watendaji wa hospitali?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha acheni ujinga, gloves zipo hospitali, ndoo na beseni yanini anajifungulia kwenye ndoo au hilo beseni?!
Kila siku tunasoma na kuona hospitali zimepewa vitanda vya kujifungulia, nyie mnanunua ndoo na mabeseni.
Yani hospitali gani haipati gloves mpaka mnunue?! Hospitali gani haipati au haina gauze mpaka mnunue?! Na hizo gauze na pamba mnazitumia wakati gani?!
Mwanamke anajifungua wanakata umbilical cord, placenta linatoka wanamsafisha kwa maji kwisha.
Mnajadili vitu gani na nyie?! Eti zitto naye yumo, angemuuliza Dr.Kugwangala au Dr.Ndugulile wange mueleza mazingira ya labor yako vipi na process iko vipi.
Jamani mmeshindwa kujadili issues mnahadili rushwa za watendaji wa hospitali?!

Sent using Jamii Forums mobile app
kwa maelezo haya ni aidha wewe ni tajiri au tasa
 
Tunalipa kodi kwa sababu gani? Kununulia ma VX na sio vifaa vya hospitali???
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom