Mwanaume Vyakula gani unaweza kupika?

Napika vyakula karibu vyote.. Ila kutumia nazi ndio sijui kwa kweli...

Na hii sikutaka kujifunza kwa sbbu sipendi mafuta ya naz
Ahahaaa umenifurahisha sana..upo kama mimi..ila mie kwenye vitafunwa aisee navijua kwelikweli..na kila siku najifunza vipya....hongera sana.
 
Mimi nilikuwa namuona Baba yetu..mama akisafiri tuu au kuumwa.basi yeye alikuwa anaahirisha outing zake zote sijui kunywa au marafiki baa...akitoka kazini anawahi home.

Anatupikia yaani saa 11 jioni chakula cha usiku tayari..SAA12 mezani mnakula..dah saa mbili wote kulala..tulikuwaa tunachukia...utoto tuu tulikuwa hatuelewi.

Anatufulia nguo,anatunyoshea na mengine mengi tuu.

Nilijifunza mengi sana..suala la mwanaume kupika kufua ni mtizamo tuu..

Kuna kipindi nikakaa kidogo huko nje ndio nikajifunza zaidi.
Maisha yangu yote ya gheto nafurahia chakula nachopika mwenyewe...

Nikiwa ofisini nikitamani chochote nawauliza staff wenzangu ambao ni wanawake wanifundishe ..wanielekeze kupika aina fulani ya Chakula..nanunua mahitaji nikiwa home napika mwenyewe nafurahia maisha..kwa njia hiyo nimejifunza kupika vyakula vingi sana sana.

Hata nilipokuja kuoa aaa wife ndio anajua raha yake..nikajifunza mapishi mengi kwake..nikawa bora zaidi..

Kwangu kupika sio ishu kabisa kabisa..nilifundishwa tangu darasa la kwanza na mama na ilikuwa lazima tukakua tumezoea naona poa tuu.
Hongera aisee
 
Chips, pilau, chapati, pizza, biriani, Tender chicken, wali ata kwenye gasi, mboga zote tena kwa karanga au nazi,rosti la nyama na Main ya kuku, samaki rosti, Tambi za nazi, mandazi na keki.

Inshort najua vingi vingine nimejifunza kupitia youtube vingine utundu n vingi n mazingira sisi tusiokua na wazazi malezi yalitufany tujifunze vyote kupika mpk kazi nyingine
Hongera aisee unajua vingi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom