Mwanaume usipokuwa na hela fuga hata ndevu. Say no to 'kidevu flat'

Wazee wa logic naomba tukae pembeni kidogo. Hii siku imeanza kwa kuvurugwa na hotuba ya Rais, na mimi naona bora niendelee kuivuruga kama kichwa cha habari kinavosema hapo juu.

Ni kuhusiana na ndevu kwa mwanaume, nimekuwa nikifanya kautafiti kidogo kwa mke wangu, nimegundua kwamba anavutiwa sana na tabia yangu ya kufuga ndevu ambayo naona imeshamiri na kutia fora kwa miezi ya hivi karibuni.

Yaani ile furaha yake wakati tunaanza mahusiano ambapo nilikuwa sifugi masharubu na furaha yake ya sasa hivi imekuwa tofauti kabisa.

Kwa upande wa kazini sio haba pia, tangu nianze ku appear ki mbuzi mbuzi, naona hata wale warembo wa 'Mkaburi' shobo zimekuwa nyingi sana pale ofisini. Hata wanaume wenzangu pia nao macho ya kisirisiri naona yamekuwa mengi, yaani ni kama wana u feel huu udevu, wanatamani kama vile uende kwenye videvu vyao ila unakataa.

Kuna kitu kingine pia nimekigundua baada ya kuamua kuwa mbuzi, nimekuwa nikijiamini sana yaani sana. Yaani hizi ndevu zimenizidishia uanaume wangu maradufu.

Ushauri wangu jamani

Mwanaume fanya chochote uwezavyo, ufuge ndevu. Wewe hujiulizi kwanini ukiangalia picha za watu wakubwa wa zamani, wote walikuwa na midevu mikubwa. Hujiulizi kwanini? Wewe hujiiulizi ni kwanini Simba dume amepewa yale manywele kichwani? Wewe hujiulizi ni kwanini dume la mbegu la beberu lazima liwe na ndevu za haja?

Hawa wanawake wapo huku pia ni mashahidi, ni ngumu sana mwanamke kutongozwa na mtu mwenye mdevu na kuwa na guts za kumkatalia. Yaani siri ni kwamba wanawake ni wadhaifu sana kwa wanaume wenye ndevu.

Honestly, eti unakutana na mtu anajiita mwanaume halafu kidevu kipo flat bila ndevu, mimi huwa nawadharau sana.

Yaani kama, wanaume tunavowaponda wanawake wasio na tak0, basi kwa mwanaume kukosa ndevu utakuwa upo kwenye kundi hilo hilo la kudharaulika. Yaani unakuta vijana wa kileo, ndevu zote kanyoa mpaka aibu.

Yaani unakuta mtu analalamika maisha magumu hana pesa, halafu unakuta hata ndevu hana, kitu Mungu alichokupa bure unashindwa kukitunza na kuringa nacho, unadhani utabarikiwa na vingine?

Ni hayo tu, ruksa kuvurugana kama mada imekuchoma maana hii ni siku ya kuvurugana.

Kama unakubaliana na mimi, ongezea madini hapa yajae maana very soon, tutazindua kitabu cha ‘Sanaa ya Uanaume wa Kweli’.

View attachment 1442131

View attachment 1442134

View attachment 1442139
Huna hela halafu una ndevu zitaota hadi puani ili ukose hewa ufe
 
Back
Top Bottom