Mwanaume usikubali kuuza nafasi yako uliyopewa na Mungu kama kichwa cha familia, hata umpende mwanamke kiasi gani nafasi yako ndio heshma yako

Mbona wameshaanza kujitetea mda sanaπŸ˜…πŸ˜…
Umesahau zile kauli za kuwa wanawake wanapenda fweza..mdogomdogo nafikiri watafika kwa mzee Abdu
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
nimecheka sana hahahahaaa

Wale wanaolalamika kwamba wanawake wanapenda fweza kwanza kabisa ijulikane ni wale wasiotunza wanawake wao bila kukumbushwa.... Nina uhakika hawajui wao ni kina nani na walipewa majukumu gani kiimani na kiasili

Ila Chakorii tuache utani hakuna mwanaume au mume mwenye raha na amani kama yule anayetimiza wajibu wake bila kukumbushwa na kuombwa
 
Tangu ijumaa tarehe 15 January 2021 imekua siku mbaya sana kwa bwana Abdul Jamaa aliyekua akijulikana kama baba Nasibu au Mzee Dangote.
Hii issue ya mzee Abdul itapita lakini sisi kama jamii tuna jambo kubwa sana kujifunza haswa kwenye mahusiano na hata kwenye malezi.

Kwa wale waamini wa Mungu vitabu vitakatifu vinatoa miongozo mizuri kuhusu tunavyotakiwa kuishi, na hata wale wasioamini kwa Mungu miongozo hii ni muhimu kwani ndio sheria na taratibu za kudumisha amani na nidhamu kwenye jamii.

Mungu alimuumba mwanaume kwanza kabla ya mwanamke, na alifanya hivyo akijua umuhimu wake wa kuwa hapa duniani na uwezo wake wa kubeba majukumu. Mungu alipoona amekua mpweke alimpa mwanamke ili awe msaidizi wake. Na katika maandiko pamoja na mambo mengine maandiko yanaongelea wajibu na majukumu ya mwanaume na mwanamke.

Wanaume vaeni viatu vyenu, hata kama una mwanamke anaweza kufanya baadhi ya majukumu usibweteke sababu wanawake hufanya vitu wakiwa na mapenzi ila mapenzi yakiisha hubaki kuwa fedheha kwa mwanaume.

Tumemwona mzee Abdul alivyokwisha dhalilika na anavyoendelea kudhalilika na kuumia. Huyu mzee inawezekana kabisa kwenye ujana wake alisahau nafasi yake sababu ya mapenzi tuu aliyokua anapata, akasahau kwamba mambo yanaweza kubadilika.

Yeye anadai nasibu ni mwanae kabisa bila wasiwasi wowote lakini pia ukimsikiliza utagundua utakwamba hakuwahi kubeba majukumu yake ndio maana anakosa hata pa kusimama walau kuutetea utu wake tuu. Mambo yamemuwia magumu sababu hajawahi simama kwenye nafasi yake kama baba au mume kijamii wala kiimani

1.Hakuwahi kumuoa mama Nasib kwa kufuata taratibu zozote za anasema, za kiserikali au za kimila. Kwa maana ya taratibu huyu mwanamke hajawahi kuwa mke wake kitu ambacho kilipelekea kuzaa
~Hapakua na makubaliano

2.Mzee Abdul Jumaa kama mwanaume hakuwahi kumiliki makazi akamchukua mama Nasib na kuishi nae ndani kama familia. Anasema yeye alihamia nyumbani kwao mama nasib, nyumba aliyokua wanaishi wazazi wa mama nasib pamoja na ndugu zake wengine
~Kuishi ukweni hata kama umeoa ni fedheha kubwa sana kwa mwanaume. Sasa hapa huyu kijana wa zamani alikosea sana maana hata hakuwa ukweni, hakuwa ameoa wala kulipa mahari

3.Mzee Abdul anasema kisa cha kutengana ni kwamba mama Nasib alitoka akaenda kwa mwanaume mwingine hadi saa nane ya usiku akawa hajarudi
~Akufukuzae hakuambii toka. Hii familia walimchoka wakamuona mzigo sababu anaishi kwao, ndio maana mama nasib akawa na guts za kwenda huko anakosemekana kwenda ili jamaa aondoke

4.Baada ya kuondoka Mzee Abdul anasema hakuwahi kurudi wala kuwasliana na mama Nasib wala nasib hadi alipoanza kupa umaarufu
~Hii ni wazi kwamba mzee yalimfika hapaaa!!! Na kwakua hakuacha kitu (mke wala mtoto wa damu) haikua shida kwake kuwacancel na kuendelea na shughuli zake.... bila kujua kwamba na wao wamemcancel na kuendelea na mambo yao

Baada ya Nasib kupata umaarufu mzee Abdul alianza kurudi sababu anajua wazi nasib ameshakua maarufu na anatumia jina lake hakuna ambaye angeweza kumzuia... Mama nasib alivumilia sababu ya mwanae lakini anavyodai alikua akimwambia "wewe ulikataa majukumu....mtoto ungemtunza angekua wako..." Ila mzee Abdul aliendelea kukomaa na medias hadi yakatokea yaliyotokea.

Maskini hakujua wanawake wakibadilika wanabadilika jumla, hawajali aibu wala fedheha! Sasa mzee Abdul ataingia kwenye phase2 ya aibu kama DNA itafanyika japo yeye mwenyewe ameshagomea DNA kwa madai kwamba mtoto hagombewi!

Wanaume wanawake ni watu wazuri na wapole sana ila mnapoishi msiishie kuishi kama marafiki tuu. Waongozeni wanawake zenu kwenye imani, mila na desturi ili heshma na upendo viwe nguzo ya familia.
Binadamu sisi tuko kama tulivyo, jitahidini kuishi na sisi mkiwa wanaume maobeba majukumu yenu na mamlaka ndani ya mahusiano, familia na jamii. Mkilegea ndio tunaishia kutengeneza familia ambazo majukumu ya familia anabeba mama halafu akishayabeba yote anachukua na maamuzi nyumba inakua shubiri.


Salim Nyange RIP na mwanae Nasib Salim Nyange
View attachment 1679951

"Kwa wale waamini wa Mungu vitabu vitakatifu vinatoa miongozo mizuri kuhusu tunavyotakiwa kuishi, na hata wale wasioamini kwa Mungu miongozo hii ni muhimu kwani ndio sheria na taratibu za kudumisha amani na nidhamu kwenye jamii"

Umemaliza mama D

πŸ‘πŸ½
 
"Kwa wale waamini wa Mungu vitabu vitakatifu vinatoa miongozo mizuri kuhusu tunavyotakiwa kuishi, na hata wale wasioamini kwa Mungu miongozo hii ni muhimu kwani ndio sheria na taratibu za kudumisha amani na nidhamu kwenye jamii"

Umemaliza mama D

πŸ‘πŸ½
Kwa wazazi na walezi Mungu atupe busara ya kuweza kukuza vijana wa Kizazi kijacho.
Ni hatari sana familia na jamii inapokosa kiongozi na msimamizi
 
Namlaumu mama Nasib kwa kumkubalia Abdul kuja kumnanihino nyumbani kwao. Huo ni ujinga na dharau kubwa sana kwao kama familia na hata kwa huyo Abdul japo hadi leo haoni kama hilo ni tatizo
Kumnanihino !!!

sema kumkaza nyumbani kwa wakwe zake MKUU..

Usimung'unye maneno.
 
Eli79 sasa kama Abdul alikua analala na mama nasib nyumbani kwa wazazi wake alipopata uchungu angebaki nyumbani na mamamkwe halafu majirani ndio wampeleke Amana!?

Mama Nasib kasema ni kweli alimpeleka hosp lakini hajawahi mlea nasib...... inaelekea mzee nae alikua analelewa tuu
Huyo mama mwehu ni wa kupuuzwa.

Alisema Mzee Abdul alimkuta akiwa na mimba ya miezi 6 lakini,
--Akakubali kulea mimba.
--akazaliwa mtoto akaitwa naseeb Abdul.
-- baada ya miaka 6 ya kuishi pamoja kama family,, mama diamond akarudi kwa Mzee Salum idd nyange..

Hyo ni baada ya ugomvi wa kurudi saa nane za usiku huku akiwa kalewa.

Iweje Mzee Abdul awe hajamlea diamond?
Hivi kipindi chote cha miaka 6 pamoja diamond alikuwa ananyonya? Au anakula nguvu za Mzee Abdul?

Huyo mama nikiangaliaga mdomo wake,,una jieleza yote ya sirini kwake.
 
Huyo mama mwehu ni wa kupuuzwa.

Alisema Mzee Abdul alimkuta akiwa na mimba ya miezi 6 lakini,
--Akakubali kulea mimba.
--akazaliwa mtoto akaitwa naseeb Abdul.
-- baada ya miaka 6 ya kuishi pamoja kama family,, mama diamond akarudi kwa Mzee Salum idd nyange..

Hyo ni baada ya ugomvi wa kurudi saa nane za usiku huku akiwa kalewa.

Iweje Mzee Abdul awe hajamlea diamond?
Hivi kipindi chote cha miaka 6 pamoja diamond alikuwa ananyonya? Au anakula nguvu za Mzee Abdul?

Huyo mama nikiangaliaga mdomo wake,,una jieleza yote ya sirini kwake.

Alikubali kulea wakati yeye mwenyewe alikua analelewa ukweniπŸ™„πŸ™„πŸ™„

Wapi alitafuta geto lake akambeba gelofriend kuishi nae!? Yaani wewe unatumia nyumba ya ukweni, chakula cha ukweni, kitanda cha ukweni, shuka ya ukweni, choo cha ukweni na bado unmtumia binti yao hadi unapasua vyombo huku mahari hujalipa hata thumni halafu umesema umenyonwa!?

mwandende Hebu acha kutetea huu uzembe, kemea tabia mbovu hizi ili Kizazi kijacho wajue madhara ya mwanaume kutokujielewa.
 
Kwa hiyo yeye na mkwe wake asubuhi wanapanga foleni na mataulo yao wanaenda bafuni.

Alafu hata baba yake mama D naye anakosa,utamfugaje mtu ambaye hajatoa mahali kwa binti yako nyumbani kwako na hata kama angetoa mahali still haijakaa vizuri,mtoto wa kiume kukaa ukweni.
 
Alikubali kulea wakati yeye mwenyewe alikua analelewa ukweni

Wapi alitafuta geto lake akambeba gelofriend kuishi nae!? Yaani wewe unatumia nyumba ya ukweni, chakula cha ukweni, kitanda cha ukweni, shuka ya ukweni, choo cha ukweni na bado unmtumia binti yao hadi unapasua vyombo huku mahari hujalipa hata thumni halafu umesema umenyonwa!?

mwandende Hebu acha kutetea huu uzembe, kemea tabia mbovu hizi ili Kizazi kijacho wajue madhara ya mwanaume kutokujielewa.
Hivi hakuna mwanaume anayeishi ukweni lakini anafanya shughuli zake za kujiingizia kipato?
Na 90% ya vyombo vya ndani amenunuwa yeye?

Huyo mama ni muhuni wa tandale ,
,msitetete uzinzi.
 
Haijalishi sisi tunamwonaje...... Watoto wake wanaelewa alikopita nae kuwafikisha walipo

Read my signature
Ni kweli kabisa,,
Kawafikisha walipo,,,,hadi muda huu diamond yupo njia panda hajuwi baba yake halisi ni yupi?
 
Ni kweli kabisa,,
Kawafikisha walipo,,,,hadi muda huu diamond yupo njia panda hajuwi baba yake halisi ni yupi?
Wewe ndio humjui baba yake halisi ila yeye na mama yake wanajua. Kwani kuna shida?
 
Back
Top Bottom