Mwanaume, usifanye ngono na mwanamke unayetaka kumuoa, ni laana

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Heshima kwenu wakuu,

Leo naomba niwashauri wale ambao hawajaoa.

Hii ni siri ya kambi namba mbili.

Usifanye ngono na mwanamke unayetaka kumuoa kama kweli unataka kuwa na familia bora yenye kuheshimiana.

Hii pia inawahusu wanawake, ila mimi nazungumzia wanaume sababu ndo wanaomba mchezo.

Kama hutasikiliza ushauri huu yatakayokupata, usilaumu.

Kuna matatizo yanayotokana na ngono kabla ya ndoa. Yaani hapa namanisha yule unayetaka kuolewa naye au kumuoa.

1. Mkifanya mapenzi, upo uwezekano mkubwa 80% ndoa ikayeyuka, sababu uzuri wa ubora na sifa nzuri za mwanamke zinaisha pale unapotembea naye. Inabaki mazoea tu.

2. Kimungu sisi tunaoamini Mungu ni kwamba ukifanya ngono na mke wako mtarajiwa, unaingiza laana ya uzinzi ndani ya nyumba. Matokeo yake mkishaonana michepuko haiishi sababu ni laana.

Unakuta mtu ana mke lakini anachepuka, mke ana mume lakini anachepuka. Mke au mume ana ndoa lakini wanazaa nje ya ndoa.

Watu hawajui sababu, ya yote haya, sababu ni laana ya uzinzi mliuoingiza ndani ya familia.

3. Wengi wenye migogoro ndani ya ndoa, ni wale walioleta laana ndani nyumba. So hutaishi kwa furaha ndani ya ndoa, iwe mke au mume.

4. Ukianza ngono nje ya ndoa, utatia aibu ndani ya familia kwani utaonywa na kusutwa uache ngono na watoto wako wa kuwazaa. Ndo maana unaona babu mtu mzima 50yrs anatongoza mtoto wa miaka 14. Ni laana

Kikubwa hapa ni kujielewa. Tofautisha rafiki wa ujana na mke mtarajiwa. Mkifanya ngono ni dalili hamheshimu miili yenu na ni sawa na kubikri tabia ya familia itakavyokuwa.

Kama ulifanya hivyo kabla, sasa ni wakati wako wa kujisahihisha. Nendeni kwenye dini zenu mkatubu hiyo dhambi ya laana.

Mimi nikitaka kuoa, siwezi fanya ngono na mke wangu mtarajiwa. Ni kuidhurumu nafsi. Hata siku ya ndoa hamuinjoy sababu kila mtu anamjua mwenzie, hamna msisimko. Matokeo yake mnaanza kula Ugali kwa picha ya samaki, upo na mpenzi wako wa ndoa kitandani kisu kwenye ala lakini mawazo yapo kwa mwanaume/mwanamke mwingine.

Ujumbe huu ni kwa watu wazima na vijana. Hii elimu hutaipata popote bali JF tu.
 
Sawa Mkuu mtu akinitongoza akisema anataka kunioa simpi.
Mkiwa mnapendana, sio lazima yeye aseme anataka kukoa, hata wewe unaweza kusema unataka akuoe. Na kumpa mwanamume ili akuoe atawapa dunia nzima na hawatakuoa. Ngono ni laana na kizazi cha nyoka ndo kinasababisha ngono, wizi, mauaji, na maasi yote. Nakushauri kama wewe ni bikra basi subiri hadi ndoa. Lakini tatizo ni kuwaka tamaa.

Wasichana wengi wanatumia ngono ili wapate nafasi ya kuwarubuni wanaume kwa ufundi wao wa kitandani ili waolewe, so wanawake walio wengi wanatumia ngono kama silaha ya kupata wanaume wanaopendeza macho yao, bila kujua Mungu ukimuomba anatenda
 
Tatizo tunaogopa kununua mbuzi kwa gunia 99% wanawake mabinti washatumika
Kwahiyo utaweza kujua ambaye ametumika na kutokutumika kwa kufanya naye ngono. Hiyo mashine yako ni tester ya kujua iloyotumika sana au mara chache? Acha mawazo ya kiasherati. Kama unampenda, utavumilia mapungufu yake kama anavyo vumilia yako. Watu wameoa wake waliozaa mara nne na bado wanaishi vizuri. Mimi nmekupa angalizo. Neno langu sio sheria. Tembea na wanawake wote hadi uwamalize uone kama hata robo yao utafikia. Tulia omba Mungu akupe mke oa. Tangu uanze mambo ya ngono umetembea na wangapi? Je uliwaoa? Kama umetembea na wake wengi na bado hujaona wa kuoa, unataka utembee na nani ili uoe? Huu ujumbe nmewaandikia watu wenye kutakia mema ndoa zao. Sijawaaandikia wazinzi na washerati.
 
Siwezi uziwa mbuzi kwenye gunia..miwanaume ya siku hizi bila kuijaribu usikubali kabisa,utakuta lina uume umelegea kama mlenda sasa wa nini huyo
Kwakuwa unafuata ngono lazima useme hivo. Umeolewa sababu uume haujalegea? Unajua siku mume wako uume ukilegea na upo ndani ya ndoa nini kitafuata?
 
Yaani unawashauri wafanye ngono kwingine, akitaka kuoa huyo anyemuoa ndo asifanye nae hadi waoane.

Sijui wa wapi wewe, bora usingetaja neno dini kwenye uzi wako.
Umenielewa vibaya. Sijashauri hivyo.
 
Back
Top Bottom