Mwanaume: Ukiwa mkristo kabla ya kuoa tafakari sana usikurupuke

Baba jayaron

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
3,994
5,437
Wasalam!

Hii habari ni mwendelezo wa matukio yangu halisi.

Ni muda sasa kama mwaka tangu nitengane na mke wangu kutokana na swala LA uzinzi ambapo aliamua kuondoka kuishi maisha yake na hawara wake.

Muda haukuwa mrefu aliomba kurudi kwangu kienyeji enyeji ila hali swala lilishafika kanisani baada ya kuona mwenzangu ameamua kuishi maisha yangu hivyo na mimi niangalie usawa wangu maana bado kijana na nna nguvu za kutosha kuvutia mrembo yeyote.

Swala langu lilipofika kanisani halikuwa rahisi kwamaana huyo mwanamke alipoitwa alikana na kudai hana mahusiano yoyote isipokuwa nilimfukuza nyumbani baada ya kushawishiwa na ndugu zangu so akaamua aondoke na kuniachia watoto wetu wadogo.

Ilikuwa vuta nikuvute, hakubali na anakataa kwa kilio akiwa na viongozi wa kanisa lakini akiwa na mimi anadai nimsamehe turudiane tuu hivyo wakati bado anawasiliana na hawara wake.

Nilipofanikiwa kunasa sauti zinazothibitisha mahusiano yao ndo ikabidi akubali mbele ya viongozi wa kanisa, lakini sasa anadai anahitaji ndoa yake na si kuachana.

Maajabu ya utaratibu wetu sisi wakristo ni kulazimishana kurudiana watu tulioumizana kiasi kikubwa kwa kigezo cha kusameheana.... Yaani ni lazima nimsamehe turudiane vinginevyo sitoruhusiwa kuoa maisha yangu yoote labda mpaka huyo mwanamke aolewe.

Binafsi kipindi hiki kifupi nimekuwa mzinifu kiani kwakuwa nipo mpweke na ni maisha ambayo naya fake kwakuwa sikuwa na mazoea hayo.

Viongozi wa kanisa wananikazia nimrudie kwakuwa eti kuna watu wanalea watoto si wao ila bado wapo na wake zao, eti ishu yangu ni ndogo tuu.... Yaan hawajui kejeli, dharau na matusi niliyotukanwa mimi na mama yangu kwa mbwembwe na hawara wa huyo mwanamke na mwanamke mwenyewe, hawajui ni magumu kiasi gani nimepitia hata sasa niko hai sababu ya hili swala, woote wapo upande wa mwanamke.

Mwanaume mkristo mwenzangu usikurupuke unapofikia hatua wa kuoa, utamu wa kyuma usikuzibe ufahamu ukashindwa kumng'amua mwanamke unayetarajia kumuoa vinginevyo utajuta.
 
Watu wa dini wanawashika sana akili sasa huruhusiwi kuoa kwani wenyewe ndo waowaji..?
😂
Upuuzi kama huu haufai mambo mengine yaajabu tu! Kuna maamuzi mengine hutakiwi hata kushirikisha watu amua kwa usahihi unaouona atakaekuja kuhoji alistahiri mwambie asipoelewa shauri yake!.
 
Watu wa dini wanawashika sana akili sasa huruhusiwi kuoa kwani wenyewe ndo waowaji..?😂
Upuuzi kama huu haufai mambo mengine yaajabu tu!,kuna maamuzi mengine hutakiwi hata kushirikisha watu amua kwa usahihi unaouona atakaekuja kuhoji alistahiri mwambie asipoelewa shauli yake!.
Ndio imani tulizozikuta na kuzikubali wenyewe tutafanyaje sasa.
 
Wasalam!

Hii habari ni mwendelezo wa matukio yangu halisi.

Ni muda sasa kama mwaka tangu nitengane na make wangu kutokana na swala LA uzinzi ambapo aliamua kuondoka kuishi maisha yake na hawara wake.
Hiyo Dini ya kikristo paka leo sielewi utanilazimishaje niishi na mwanamke mzinifu, hata ukiwa wewe ni Yesu mwenyewe katika hilo swala ntakugomea tu.
 
Wasalam!

Hii habari ni mwendelezo wa matukio yangu halisi.

Ni muda sasa kama mwaka tangu nitengane na make wangu kutokana na swala LA uzinzi ambapo aliamua kuondoka kuishi maisha yake na hawara wake.
Kuna falsafa moja huwa naikubali sana! " Ukishapata mchumba kabla hujamuoa, kwanza muoe mama yake" hapo umemaliza kila kitu. Kitakachoendelea ni wewe mwenyewe kusuka au kunyoa.
 
Mkataba wowote lazima uwe na terms and conditions, mmoja wenu akizivunja mnamalizana kila mmoja anaendelea na mambo yake.

Mwanamke akishakuwa Mzinifu kuna hatare sana kwa Mwana mume maana anaweza hata akashirikiana na Jamaa kukung'oa kabisa.

Ni mara chache sana Mwanamume kushirikiana na Hawara yake kumdhuru Mkewe ila ni tofauti kwa upande wa pili akisuguliwa akasugulika sawasawa anaweza hata akaratibu hujuma dhidi yako.
 
Hiyo Dini ya kikuristo paka leo sielewi utanilazimisha je ni ishi na mwanamke mzinifu, ataukiwa wewe ni Yesu mwenyewe katika hilo swala nta kugomea tu.
Yesu mwenyewe amesema mtu anaweza kumpa mkewe talaka isipokuwa tu sababu ya uzinzi.

Kama mwanamke amekubali alikuwa anazini kanisa wanakosea kumkatalia kutoa talaka.

Jamaa woga tu anaweza kuoa bomani fasta au kuoa ndoa ya kimila.

Hapo baki ndoani kulea watoto tu si kwa sababu ya kukataliwa kuvunja ndoa na kanisa.

Haya makanisa na madhehebu ya dini na dini nyingine tofauti ya ukristo yameingiza mambo mengi ya uzushi ambayo si amri za Mungu, ni tamadauni zao au zina maslahi na walioziingiza kwenye dini.
 
Yaan nilazima nimsamehe turudiane vinginevyo sitoruhusiwa kuoa maisha yangu yoote labda mpaka huyo mwanamke aolewe.
Wanakulazimisha tu lakini ukikomaa unataka muachane inawezekana na inakuwa rahisi zaidi kama ushahidi unao.

Process ni ndefu ila ukiamua unaweza. Hawawezi lazimisha ndoa iwepo kama mmeseparate muda mrefu na hakuna dalili ya kurudiana.

Kama una nia ya kuvunja ndoa pambana, ila tu uzijue sababu zinazofanya ndoa kubatilishwa. Tafuta kitabu cha misingi ya sheria ya ndoa katoliki, kitakupa muongozo.

Mahakama ya ndoa ipo kule Kurasini kwa askofu karibu na uhamiaji. Nenda huko ukapate muongozo..uachane na huyo mwanamke kama unataka.

Inahitaji uvumilivu na usiwe na haraka. Hakuna kisichowezekana. Ila kama vipi mrudie tu.

Hata biblia inasema uzinzi unavunja ndoa, sababu unayo.
 
Back
Top Bottom