Mwanaume, tambua jukumu la kutunza familia ni la kwako

kwamtoro

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
4,922
3,234
Wanaume wa kileo, wengi wetu hatutaki kutambua/kufanya majukumu yetu kama wanaume. Imefikia mahala tunachaguwa mwanamke mwenye uwezo wa kutafuta pesa, ndio tunaona ni wife material. Yote hayo sababu ya kukimbia majukumu yetu ya kutunza familia kama wanaume.

Mimi ni mmoja wa watu ambao sifikiri na sitaki kushare majukumu ya kutunza familia na mke wangu, pamoja na kuelewa fika kwamba yeye ni mfanyakazi, pesa zake sizipigii hesabu wala sihoji matumizi yake.

Sababu mwanamke ambaye anashare naye majukumu ni rahisi sana kushare maamuzi na wewe. Kama pesa yake itatumika kwa nini na yeye asiwe na sauti, ndipo hapo inapelekea wanaume wa siku hizi wengi wetu kulalamika kukosewa adabu, kutoheshimiwa na kadhalika.
 
Labda iwe ni tatizo la makuzi ya muhusika tu.Kwa miaka mingi tumelelewa na kufundishwa majukumu yetu ktk familia na jamii kwa ujumla wake.Uhuru wa habari una halalisha watu kuishi kwa hisia kuliko facts.
 
Sio mbaya garama za maisha za familia zikachukuliwa na mwanaume. Lakini tatizo la wanawake wa kileo hata majukumu yake ya kijamii(yasiyohusu pesa) hataki kuyatimiza. mfano mwanamke hata kumuogesha mwanawe mpaka apigiwe kelele na mwanaume,kuangalia maendeleo ya mtoto kielemu hata kumfundisha a,e,i,o, u mpaka mwanaume umwambie afanye hivyo. Hapo ndipo wanaume huamua kuchagua wanawake wa kuowa na kuchangia garama maana hata majukumu yake hawezi yafanya kwa nini asichangie anachopata kwa familia?
 
mkuu kwa ninavowajua wadada wa JF
bila shaka PM yako inakosa pumzi mda huu
tegemea LIKE za kutosha toka kwa wadada tegemezi
 
Mwenye mkono mrefu kwenye kapu la familia mara zote ndiye mtawala na ndiye mtoa amri(mamlaka) Sasa itashangaza uwe bingwa wa kuamuru kwenye kitu usichokitolea jasho!
Naunga mkono hoja!
 
uuuh how i dream of this kind of man......ntakupa kila heshima unayostahili duniani,chezeyaa kuniweka mjini...
 
Kwamtoro, umeongea ukweli nusu badala ya ukweli kamili. Sasa kama mke naye ni mfanyakazi, pesa zake zinatumikaje? Mimi naamini wote wawili wana wajibu sawa ktk kutunza familia.
 
Unaweza kuhudumia kila kitu na bado ukaingiliwa kimaamuzi.Kumshirikisha mke kwenye majukumu ya kuhudumia familia haina maana kuwa atainglia maamuzi yako,by the way sioni tatizo kama mke wako ataingilia maamuzi yako as long as ana point ya msingi.

Binafsi naamini kwenye kumshirikisha mke kwenye kufanya maamuzi caz ni moja ya mantiki ya ndoa,kusaidiana.wether familia naihudumia mimi peke yangu au tunashirikiana lazima asilimia kubwa ya maamuzi nimshirikishe maana kuna kesho lolote laweza tokea halafu asiwe na taarifa.
 
unajua, kwa dunia ya sasa tuliyofikia, sidhani kama unachokisema kina mantiki. Mimi naamini mwanaume ndiyo kichwa cha familia, hilo halina ubishi, lakini when it comes to finance planning ya familia, unatakiwa wewe na mkeo muwe kitu kimoja, yaani mshauriane kipi kinafaa na kipi hakifai, haijalishi nani anaingiza kipato kibubwa.. mnachokipata wote mnakiweka mezani mnakijadili ni asilimia ngapi ifanyie hiki na ngapi ifanye kitu kingine na ngapi iwe akiba. its obvious kama mke ni muelewa na anajua wewe ni "kichwa" atakusikiliza wewe kwanza(kitu ambacho wadada wetu wa siku hizi wengi wao hawana), lakini anapoona unaenda chaka kidogo atakushauri, na wewe kama ni mume muelewa utauzingatia na kuufuata ushauri wake.
Sasa ukisema anachokipata mke kikitumika nyumbani basi na yeye atapaza sauti, basi wewe utakuwa umempata mwanamke siye. Au umempata anayefaa lakini yeye kukushauri kuhusu uchumi wa familia wewe ukaona kana kwamba anapaza sauti, basi ni wewe ndio ujiangalie vizuri. kwa hiyo sometimes inategemea na mke anakushauri kitu gani, maana kuna ushauri utaona kabisa kwamba anataka kujilinganisha na wewe, hataki kufuata maamuzi yako wakati unaona fika kwamba ni maamuzi mazuri kwa familia.
 
Kama ni mama wa nyumbani hapo sawa ukute mkeo mmelingana elimu kama una jiwe na yeye ana jiwe lake, kama ni kazi wote mko sehemu nzuri na pesa almost ziko sawa, so kuna haja ya kugawana majukumu kwa maendeleo yenu wenyewe kama mtu hana heshima hana tu hata kama utamwekea Mtu wa kumwogesha na kumfanyia kila kitu hela zake atatapanya na kwenda kujifanyia anasa zake na wewe utabaki na mfumo dume wako wanaume wengine wanapewa hela bure usiwe mwoga, fanya hivi matumizi ya nyumbani muachie wife kwa asilimia kubwa ila akibanwa pia atakwambia ila maendeleo ya familia kama kukuza biashara, ujenzi au ununuzi wa assets kama mashamba n.k ni kazi ya mwanaume endapo mke wako atatoa support unamshirikisha. na mwanaume wa ukweli anataka mke atakae mchallenge kidogo sio kama masai kila kitu mwanaume mke anamweka group la watoto, something new mweke mke wako mezani mfanye discussion na ndio maana kamili ya msaidizi. Mtoa uzi anapenda mfume dume sasa what if your wife earn 2m and you earn 1m so your still want equality mawazo yako still yamekaaa kizamani zamani.
 
unajua, kwa dunia ya sasa tuliyofikia, sidhani kama unachokisema kina mantiki. Mimi naamini mwanaume ndiyo kichwa cha familia, hilo halina ubishi, lakini when it comes to finance planning ya familia, unatakiwa wewe na mkeo muwe kitu kimoja, yaani mshauriane kipi kinafaa na kipi hakifai, haijalishi nani anaingiza kipato kibubwa.. mnachokipata wote mnakiweka mezani mnakijadili ni asilimia ngapi ifanyie hiki na ngapi ifanye kitu kingine na ngapi iwe akiba. its obvious kama mke ni muelewa na anajua wewe ni "kichwa" atakusikiliza wewe kwanza(kitu ambacho wadada wetu wa siku hizi wengi wao hawana), lakini anapoona unaenda chaka kidogo atakushauri, na wewe kama ni mume muelewa utauzingatia na kuufuata ushauri wake.
Sasa ukisema anachokipata mke kikitumika nyumbani basi na yeye atapaza sauti, basi wewe utakuwa umempata mwanamke siye. Au umempata anayefaa lakini yeye kukushauri kuhusu uchumi wa familia wewe ukaona kana kwamba anapaza sauti, basi ni wewe ndio ujiangalie vizuri. kwa hiyo sometimes inategemea na mke anakushauri kitu gani, maana kuna ushauri utaona kabisa kwamba anataka kujilinganisha na wewe, hataki kufuata maamuzi yako wakati unaona fika kwamba ni maamuzi mazuri kwa familia.
Nice quote, big mind
 
Back
Top Bottom