Mwanaume ni kichwa

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,271
29,877
KUTOKANA na ubize wa maisha, wanaume wengi sana wamekuwa wakishindwa kutimiza majukumu yao.

Mwanaume anashindwa kufanya mambo yanayompasa kufanya kwa mwenzi wake na kujikuta akiingia kwenye migogoro na mwenzi wake. Ubize huu upo wa aina nyingi.

Kuna ambao majukumu ya kazi yanawabana wanajisahau lakini kuna ambao wanafanya makusudi kwa kubebwa na zile kauli za ‘atanifanya nini mimi si ndiyo mwanaume.’

""WANAKOSEA""

Mapenzi yana vikorombwezo vingi ili yaweze kuwa na tija. Mwanaume anapaswa kumpa ulinzi mwanamke ili aweze kujivunia kuwa na mwanaume wake.

Anataka atambe kuwa na mwanaume ambaye ndiyo shujaa wake. Ukimtimizia mahitaji yake, atajiona wa thamani na atakuheshimu zaidi.

Mwanaume unapaswa kumpa ulinzi wa kutosha mwanamke wako kwa kuhakikisha unampa mahitaji yote anayoyahitaji.

Mwanaume unapaswa kuwa bosi wa mkeo. Kwa kawaida mwanaume ni kichwa cha familia.
Hilo liko wazi na halihitaji mjadala. Usiwe kichwa katika kutoa amri za kufuliwa nguo, kuwekewa chakula na mambo mengine lakini ukasahau suala zima la kuwa mwezeshaji.

Mwanaume unapaswa kuwa mwezeshaji ili uweze kuibeba dhana ya ‘kichwa.’

Unaanzaje kubebwa tu maisha yako yote na mwanamke?
 
Wanawake wa siku hizi wanataka sifa sana; wanatafuta hela kuliko wanaume acha tupumzike
 
Back
Top Bottom