SoC02 Mwanaume ndiye Mtu wa kwanza kuzuia Mimba zisizopangwa

Stories of Change - 2022 Competition

The Gojo

Member
Feb 27, 2014
31
11
UTANGULIZI:

▪︎Mimba zisizotarajiwa zimekuwa tatizo sugu kwa miaka mingi katika jamii yetu. Nataka kusaidia kuondoa mimba zisizopangwa kwa kumuelimisha mtoto wa kiume ambae ndiye huweka mimba.
Ni rahisi, mwanaume anatakiwa ajue na kuelewa mzunguko wa hedhi wa mwanamke kwa usahihi. Hitaji la elimu ya afya ya ngono ni dhahiri na ya lazima kuanzia ngazi ya sekondari, vyuoni hadi mtaani.

▪︎ Kingine ninachotaka kuelimisha ni kwa wanaume walioko katika ndoa ambao hawajui kwa usahihi ni jinsi gani ya kupata mtoto wa jinsia fulani.

Mfano ukitaka kupata mtoto wa kiume unafanyaje?

NADHARIA:
Elimu ya mzunguko wa hedhi ya mwanamke ndiyo njia bora zaidi na rahisi kuzuia mimba zisizopangwa kwa 80% na kuamua jinsia ya mtoto.

Kwa miaka mingi, mimba zisizopangwa, zimekuwa zinatungwa. Matokeo yake ni majuto, ndoa za kulazimisha, utoaji mimba,kukatiza masomo kwa watoto wa kike, ongezeko la watoto wa mtaani, kwenda jela,migogoro na vifo. Kiukweli, kuna ndoa nyingi zimetokana na mimba iliyoingia bila mpango. Matokeo yake, ili kukwepa aibu na fedheha, wenza hulazikmika kuoana hata kama hawakupendana na hawakuwa na mpango huo. Wakati mwingine wazazi au walezi hulazimisha ifungwe ndoa baada ya mimba hiyo.

Mara nyingi matatizo kama haya yanapotokea anaelaumiwa ni mwanamke pekee. Lakini kama mwanaume angejua kuwa leo ni siku mbaya, lazima angefanya juhudi fulani kuzuia hiyo mimba kuepusha madhara hapo baaaae.

● KUEPUKA MIMBA ZISIZOPANGWA:
Mwanaume, lazima ujue kuhesabu siku za mwenza wako sawasawaa.
Mzunguko wa hedhi wa wanawake wengi hutofautiana kulingana na sababu za kibiolojia. Kuna wanaotumia siku 28, 30 hadi 35. Wengine hupata hedhi mara mbili kwa mwezi. Lakini muhimu ni kumjua mwenza wako kwa kuanza kuhesabu tarehe aliyoanza hedhi.

Ileweke kuwa mimba hutungwa wakati yai lipo katikati ya safari yake yaani siku ya 14, 15au 16. Hii ndiyo siku ya hatari [ovulation]. Mfano kama mwenza wako alianza tarehe 1, ili kuepuka mimba, inabidi ujizuie siku tatu kabla ya hii tarehe yaani tarehe 11. Subiri zipite siku 6 mbele yaani 18. Tarehe inayofuata endelea kushiriki bila wasiwasi. Mfano kama alinza tarehe 12,unajumlisha 11. Yaani, 12+11= tarehe 23. Kutoka tarehe 23 hadi 28 usikutane nae kabisa. Anza kushiriki tena tendo la ndoa tarehe 29.

Mimba hutungwa katika mirija iitwayo Fallopian tubes. Siku za hatari ni kati ya 3-8 kutegemeana na hali aliyokuwa nayo mwanamke kwa mwezi huo. Ili mwenza wako asipate mimba, hakikisha usishiriki tendo la ndoa baada ya siku ya 11 tangu siku alipoanza hedhi. Kama hutaki mimba, mtafute baada ya siku 6.

Zingatia, safari ya yai huathiriwa na vitu vifuatavyo.
1. Homa
2. Kubadili mazingira, mfano hali ya hewa
3. Kubadili chakula
4. Masongo wa mawazo
5. Matumizi ya kemikali

Sababu tajwa hapo juu husababisha kuwahi au kuchelewa kwa yai katika safari yake ya kawaida. Mfano kama mwenza wako alikuwa na homa, basi yai litachelewa. Pia kama amepata habari ya kushtua mafano kifo au mstuko, hedhi inaweza kuanza ghafla. Hivyo kama alipitia changamoto hizo unatakiwa uwe makini zaidi. Changamoto hizo huvuruga safari ya kawaida ya yai. Ni vizuri kujizuia hadi atapoona siku zake ukishiriki kwa uhakika.

● JINSIA YA MTOTO.
Japokuwa binadamu wote tunamtegemea Mungu na ndiye huamua kila kitu ikiwemo jinsia ya mtoto, sisi pia tunatakiwa kufanya juhudi ili kutawala mazingira yetu. Unaweza kuamua uzae mtoto wa jinsia gani, kama umejaaliwa mbegu za aina zote. Kwa kawaida mwanaume ana mbegu za aina mbili yaa X na Y. Wakati mwanamke ana X pekee. Zifuatazo ni sifa za mbegu za mwanaume, x na y.

■Sifa ya Y
• Ina mwendo mkali
• Huishi si zaidi ya masaa 48
• Hufa haraka

■Sifa ya X
• Ina mwendo mdogo
• Huishi masaa 72
• Haifi haraka
Tarehe na muda hedhi inapoanza kwa mwanamke ndiyo siku na muda huohuo yai jingine linaanza safari kutoka katika ovary.

■SIKU ZA HATARI.
1. Mwanamke kuwa na hamu ya mapenzi
2. Ute mweupe mwepesi unaotoka asubuhi
3. Jotoridi la mwili kupanda
Hii ni hali ya kibioloji kama ilivyo kwa wanyama wengine.
Wasichana wengi wanaobalehe mfano wanafunzi ambao hawana elimu ya ngono, ni wahanga wakiwa katika siku hizi,ni rahisi kukutana na mwanaume na kupata mimba. Jambo hili katika shule za sekondari na vyuo ni dhahiri.

■ MTOTO WAKIUME:

•HAKIKISHA UMESHIBA

Hutokea siku za hatari yaani 14,15 au 16 tangu mwanamke aanze kuona siku zake.Hii ni baada ya mbegu ya Y na X kukutana. Mwanamke akiwa katika siku za hatari, hupenda kukutana na mwanaume, hata kama hampendi na mara nyingi huishia kushiriki tendo la ndoa. Ndiyo maana ni vizuri kwa mwanaume kujua hali ya mwenza wake ili asije kufanya maamuzi yenye madhara kwa baadae.

• HAKIKISHA NI SIKU YA HATARI
Mwenza wako lazima awe katika siku za hatari, yaani siku ya ovulation ili kupata mtoto wakiume kwaurahisi. Kumbuka Y ina speed kuliko X. Katik utungaji wa mimba ni mbegu moja tu katika mamilioni ya mbegu huingia kwenye yai. Siku unapoenda kushiriki tendo la ndoa ili kupata mtoto wa kiume,kula vizuri, mlo kamili wenye nguvu na umeshiba vizuri.

■ MTOTO WAKIKE
Hutokea ukikutana na mwenza wako siku ya 12, 13 tangu mwanamke aanze kuona siku zake. Baada ya mbegu ya X na X kukutana.

●USHAURI:
Ninatoa rai kwa serikali na wadau mabilmbali kuwekeza zaidi katika maarifa na elimu kama hii ili kuwasaidia vijana wengi. Kuzaa kwa malengo ni njia sahihi ili kuwa na uchumi imara katika jamii na taifa lolote duniani.

SULUHISHO:
Lengo langu ni kuandaa vitabu, vipeperushi, vipindi vya television, michezo matamasha na midahalo kuanzia shule za sekondari, vyuo vya kati, vyuo vikuu na mtaani ili kuwafikia wanaume na kuwaelimisha kuhusu MZUNGUKO WA HEDHI wa mwanamke. Elimu hii itakuwa bure, maalumu kuzuia mimba zisizopangwa na elimu ya afya ya ngono kwa ujumla. Lengo ni kuandaa jamii imara isiyokuwa na watu tegemezi waliotokana na ngono zembe na ukosefu wa elimu rahisi kama hii. Imani yangu ni kuwa, ukimuelimisha kijana wa kiume, umezuia mimba zisizotarajiwa kwa 80%. Hii itakuwa ni suluhisho la madhara ya mimba zisizopangwa.

HITIMISHO:
Njia za uzazi wa mpango ni nzuri sana, lakini mara nyingi zimekuwa zinatumiwa zaidi na wanawake, zinasaidia kutunza maadili kwa watoto.

Mwanaume akijua mzunguko wa hedhi, uzazi wa mpango itakuwa ni rahisi sana. Wakielimika watakuwa walimu wazuri kwa baadae. Hii ni maalumu kwa wanaume.
 
Back
Top Bottom