Mwanaume mwenzangu unaitatuaje HNdugu zetu na wake zetu acheni vita

Ulirchdov

JF-Expert Member
Apr 4, 2019
356
258
Salaam kwenu wakuu!!
Mara nyingi sana imekuwa ikitokea kwamba wake zetu na ndugu zetu kuna uhasama,ubabe au migogoro midogo midogo inayotokea, huenda ikawa kati ya wazazi wetu hasa mama zetu na wake zetu au dada zetu na wake zetu. Dada zetu wamekuwa ni watu wazuri siku zote kiasi kwamba wao hawakosei wala hawajawahi kukosea katika ndoa zao, wamekuwa wakosoaji wa wake zetu na ndoa zetu kwa ujumla. ukioa single mama utasikia mara ooh kaoa mkosi, ukioa mgumba mara ooh familia yetu haijawahi kuwa na wagumba huu ni mkosi mkubwa, ukioa mwanamke mweusi mara ooh umepewa bure hadi unajiuliza hivi hawa ni ndugu zangu au watani zangu au walishawahi kuwa na mgogoro na huyu mwanamke kabla sijamuoa?
Cha ajabu zaidi unaweza kukuta hawa dada zetu muda mwingine ni watu wa kuzalishwa tu nyumbani hawajawahi kuwa na ndoa wala hawajui ndoa ila wanavyomsimanga mtoto wa watu utafikiri wanafundisha taaluma ya ndoa, ni mara chache sana kuwakuta dada zetu wakielewana na wake zetu.
Kulikuwa na Mama fulani alizaa watoto wawili wa kiume, alikuwa amejenga nyumba na mumewe, miaka michache baadaye mumwe alifariki, alilea watoto wake huku akiwasomesha kwa shida lakini siku zote Mungu akikupa kilema hakunyimi mtambao, Mwenyezi Mungu amemjalia juhudi za upambanaji kuhakikisha anawalea watoto wake, ghafla wifi zake(dada wa mume) wakaanza visa maneno lukuki wengine wakisema alimuua kaka yao, wengine wakisema kaka yao alikosea kuoa hakuwa mtu wa kuoa mwanamke kama yule na mbaya zaidi wakamfukuza kwenye ile nyumba aliyojenga na mumewe wakidai hana cha kusubili. Huwa najiuliza kwamba hawa mawifi wanavyosema kaka yao alikosea kuoa je hawaoni kama wanawaathiri kisaikolojia watoto aliowazaa kaka yao na huyu mwanamke? Na je, wanavyosema alikosea wana maana kwamba hata hawa watoto hawakutakiwa kuwa damu yao? Je,walivyomfukuza kwenye ile nyumba hawakuwathamini hawa watoto wa kaka yao kwamba wanahitaji kulelewa na mama yao katika ile nyumba iliyoachwa na baba yao? Cha ajabu zaidi kuna shemeji zake wawili nao wanashirikiana na dada zao. Ni jambo ambalo nimekuwa nikimwomba Mungu siku zote mke wangu na wanangu wasije kunyanyasika, kukandamizwa na dada zangu au kaka zangu.
Ndugu zetu wa kike na wa kiume yawapasa kuishi na wake zetu vizuri kwasababu hatujui hatima yetu, vile mnavyotupenda na kutuita kwa mbwembwe zote tukiwa hai mjitahidi kuwapenda watoto wetu hata tutakapokuwa tumetangulia kaburini, kumbukeni kifo tumeandika ila kutangulia hatujaandikiwa huenda ukatangulia ukawaacha wanao ilihali wakiwa hawana msaada ndipo nitakapolazimika kuwachukua na kuishi nao, je huyu mke wangu uliyeishi naye kwa uhasama mkubwa atawalea wanao pasipo visasi?
Wake zetu pia jitahidini kuishi na ndugu zetu vizuri tambueni hakuna mkamilifu na hakuna haja ya kuishi kwa visasi wakati mapungufu ya dada na Kakazetu mnayajua, ipo siku mtabaki na ndugu zetu au watoto wetu watabaki yatima ambapo watalazimika kulelewa na hao mawifi au mashemeji mlioishi kwa bunduki na mabomu, yawapasa kuishi kwa amani na kwa hofu kubwa juu ya vizazi vyenu ili msije kuacha mizizi ya chuki ambayo hata sio rahisi kuoza.
Wanaume wenzangu tuishi kwa tahadhari kubwa tujitahidi tuwezavyo kuepusha uhasama kati ya wake zetu na ndugu zetu, tusiwe na upande panapo mgogoro ila tuwe watu wa kutafuta suluhu ya amani yenye kuleta usawa pasipo kuathiri upande mwingine, tujitahidi kuepusha visasi kwasababu watoto wetu ndiyo wanaoumia zaidi, kwanini tuwatese watoto wakati migogoro inatuhusu sisi wakubwa? Kila mmoja katika ndoa yake atengeneze mahusiano mazuri na ndugu zake ingawa ni vigumu lakini tujitahidi kadri ya uwezo wetu kufanya jambo lenye tija litakaloamua msitakabali mzuri kwa vizazi vyetu.
 
NB: Title ya hii post imekosewa kidogo wakuu ila naomba isomeke hivi "Ndugu zetu na wake zetu acheni vita"
 
Mkuu utakua umeoa na kuleta mke nyumban kwenu....
Familia iko moshi mm naish sumbawanga
Mke yuko bize na kaz zake na wifi zake hvyohvyo nao wanapambana na stress za ndg za waume zao, hapo ugomv utatokeaje

Cha muhimu mkanye mkeo mwambie wale ni wifi zake sio mashost mazoea yakizid ndipo dharau zinapoanza na dada zako pia wape the same warning
 
Mkuu utakua umeoa na kuleta mke nyumban kwenu....
Familia iko moshi mm naish sumbawanga
Mke yuko bize na kaz zake na wifi zake hvyohvyo nao wanapambana na stress za ndg za waume zao, hapo ugomv utatokeaje
Cha muhimu mkanye mkeo mwambie wale ni wifi zake sio mashost mazoea yakizid ndipo dharau zinapoanza na dada zako pia wape the same warning
La hasha! nimeandika kulingana na uzoefu nilionao nimeona watu wengi sana wanajitegemea na miji yao lakini vita vipo tu, kama huyo mama niliyemtolea mfano hapo kwenye andiko yeye na mumewe walikuwa wanajitegemea lakini yalimpata mabomu ya mawifi.
Mimi pia nina mji wangu, nia ya uzi huu ni kupeana ushauri na kujua tunajisahau wapi kwa niliyoyaandika hayana uhusiano na ndoa yangu isipokuwa nimeandika kwa uzoefu wa matukio ambayo mara nyingi nimekuwa nikiyashuhudia kwa watu wengine.
 
Back
Top Bottom