Mwanaume mwenye mapenzi ya kweli,mrefu,mweusi na handsome asome hapa!

nasikitikaa

Member
Apr 20, 2012
47
24
Habari kaka,natumai mwenye sifa tajwa hapo juu ndo unayesoma hapa' mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 30,nipo serious na natafuta
mwanaume mwenye sifa hizo kwa kuwa mwenyewe nina sifa za mwanamke mrembo shepu namba 8.yaani juu mwembaba chini Mungu nampa sifa zake,kwani kanijalia kusema ukweli na ni original kabisa,rangi yangu ni maji ya kunde with Excelent Health!

Elimu ya chuo,na ni mwalimu wa Secondary hapa Dar na najitegemea na naendelea na masomo. Swali,je kwa nini nimeamua kuchagua njia hii ya JF kumtafua mpenzi wa kweli? ni kwa kuwa nimeona wengi wanaotumia FORUM HII wana upeo mzuri na waelewa na si wahuni,na hawatachukulia suala hii kama joke ndo mana sijaenda kule kwenye chit-chat so you have to be serious here! kama sio wewe mlengwa naomba upite tu nitakushukuru.

Jambo jingine ninalopenda kuweka wazi ni kwamba kabla ya kuchukua uamuzi huu mgumu nilikuwa na mpenzi ambaye awali nilijidanganya kama nimepata kumbe sivyo,kwa kuwa hakuthamini mapenzi yangu ya dhati kwa kunichukulia kiutani huku miaka ikiwa inapita pia nikatambua kwamba hatuendani kwa mambo mengi,mfano ni mlevi wa kupindukia,hapendi kujituma nikiwa na maana ya maendeleo hata ya kupiga hatua moja mbele ki- maisha,hakuwa anaonyesha Real love ya kusema mimi naweza kujivunia hata kwa marafiki kama nina mpenzi muda mwingi nikawa lonely yeye akiwa Busy na ulevi uliokithili.Ivyo tukielewana ukinipa sifa zako tutaonana live .

So if you are lonely out there you are welcome and just be realistic and affectionate!
 
Kila la heri katika kutafuta mwenzio.

 
Last edited by a moderator:
BAK, nilistuka nikajua unachangamkia tender.
Dada mpendwa, naweza kuku-book kwa ajili ya mtu?
 
Last edited by a moderator:
BAK, nilistuka nikajua unachangamkia tender.
Dada mpendwa, naweza kuku-book kwa ajili ya mtu?


Mhhhh! Best King'asti hunitakii mema weye! LOL! "mbook" huyu binti fasta fasta kabla wajanja hawajamnasa :):)....Anaonekana katulia halafu kulikuwa na uzi hapa kwamba Walimu wanafaa sana katika ile idara ya mke na mume.
 
Last edited by a moderator:
Umenifurahisha kweli. Kumbe watu ka wewe mpo. Mungu akubariki... Goodluck, mi umri bado nakua...
Ahsante kwa kuikubali JF,
 
kaka Bak,hii Shalamar ndo nini?ok naomba unielekeze mtu akisema ni Pm ndo nini
ni private sms or what na unafunguaje ili kuzisoma?mana mi bado mgeni humu na ukiielimisha nitashukuru sana.
 
kaka Bak,hii Shalamar ndo nini?ok naomba unielekeze mtu akisema ni Pm ndo nini
ni private sms or what na unafunguaje ili kuzisoma?mana mi bado mgeni humu na ukiielimisha nitashukuru sana.


shalamar ni muziki kakuwekea video kama dedication usikilize click kile kialama cha mshale katikati kama kny radio ...usikilize...,na PM ni private message ndio ila sijui kukuelekeza ufungue vipi?
 
natafuta mke wa pili (japo mimi mkristo), ukikosa huyo bwana mwenye mapenzi ya dhati usisite kunitafuta japo utakuwa mke wa pili, mpo wengi sana duniani, lazima tufanye balance walau ya kuoa wake wawili kuliko kuhenya henya nje.
 
natafuta mke wa pili (japo mimi mkristo), ukikosa huyo bwana mwenye mapenzi ya dhati usisite kunitafuta japo utakuwa mke wa pili, mpo wengi sana duniani, lazima tufanye balance walau ya kuoa wake wawili kuliko kuhenya henya nje.
You must be kidding,then nilisahau Dini jamani mimi ni mkristo na napenda mkristo
sitaki uke wenza mana nina wivu sana,na Dini yangu hairuhusu ivyo,halafu nani kakwambia
kama sisi wanawake tupo wengi?hata kama idadi ipo ivyo,lakini Mungu kampangia kila mtu na wake na mimi yupo tu najua atakuja;Aksante,
 
Nina sifa zote ulizozitaja, ila sina moja tu, mapenzi ya dhati, sijui nafaa.
 
Inaonekana umeomba Mungu kabla ya kuja hapa. Yaani nilivyosoma nimeogopa sana na presha kunipanda coz umenilenga mimi hadi najiuli umejuaje?
Mimi naona topic ifungwe sababu umeshanipata. asante kwa upendo wako. Mmwaaa...!! Love you..ntakupm soon nasikitikaa. Hugs..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom