Mwanaume Mwenye Aleji na Mke Wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume Mwenye Aleji na Mke Wake

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Dr. Chapa Kiuno, Nov 3, 2009.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  </SPAN>


  Young hulazimika kuvaa gloves anapokuwa karibu na mke wake.
  Tuesday, November 03, 2009 8:33 AM
  Mwanaume mmoja nchini Uingereza amedai kuwa na aleji na mke wake na mapigo yake ya moyo huongezeka maradufu na mwili wake kuanza kuvimba kila anapomkaribia.


  Darren Young, 45, mkazi wa Yorkshire ana aleji na kemikali ya polyethylene glycol inayotumika kwenye krimu, losheni karibia zote pamoja na kwenye dawa za meno na hupata tabu sana mkewe anapojipaka losheni au krimu.

  Mapigo ya moyo wake huongezeka maradufu na wakati mwingine moyo wake hukaribia kusimama, mwili wake huvimba na kutoa vipele kila anapokuwa karibu na vitu hivyo.

  Young, ambaye ni dereva wa mabasi ya mji wa Sprotbrough, anasema kuwa huwa hawezi kumsogelea mkewe anapotumia losheni au krimu.

  "Unapofika wakati wa kulala, mke wangu Sue huwa hahitaji sababu yoyote ya kunikwepa au kunifukuza kitandani, huwa anatumia losheni", alisema Young alipokuwa akiongea na gazeti la The Sun la Uingereza.

  "Sio Sue peke yake, huwa nadhurika kila ninapoenda baa na kukaa karibu na mwanamke anayetumia losheni".

  "Madaktari hawajui nini kimenisibu na kunifanya ghafla niwe na hali kama hii", alisema Young.

  Young aligundulika kuwa na aleji hiyo wakati alipochomwa sindano ya steroid iliyokuwa na polyethylene glycol ili kutibu matatizo ya miguu yake.

  Uso wake ulivimba baada ya kuchomwa sindano hiyo na moyo wake ulisimama na ilibidi uzinduliwe tena kwa mashine.

  Young ametakiwa na madaktari awe makini sana anapogusa kitu chochote na amekuwa akitumia madawa mbali mbali kila siku.  Source: The Sun
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  heee huyo mwanaume mbona hatari
   
 3. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakuambia! Hivyo visa ss
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii habari si njema kwangu , maana mabinti wakigundua hiyo kemikali sijui tutawapata wapi tena maana ukimsogelea tu moyo unasimama na mwili kuvimba......
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hata mimi na 'Allergy' mbaya na wanawake wanaovuta sigereti na wanaokunywa bia!

  Huyo mke si aache tu kutumia hizo lotion na toothpaste kuinusuru ndoa yake?
  au ndio anataka kumtoa roho mzee wa watu maisha yaendelee?

  Wanawake wengine bana!
   
 6. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  yaani aache hata kutumia toothpaste, je mdomo na utakuwa na hali gani?
  mingine mitihani kwa kweli.
   
 7. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ila c abadili aina ya dawa jamani.
   
 8. Bang'a

  Bang'a Member

  #8
  Nov 5, 2009
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kwel huya mke anamtihan mkubwa. Ila usije kuta jamaa anazunga na kutembea na wadada poa!
   
Loading...