Mwanaume Mjamzito' wa Marekani Ajifungua Mtoto wa Pili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume Mjamzito' wa Marekani Ajifungua Mtoto wa Pili

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Jun 11, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Thomas Beatie wakati alipokuwa na mimba yake ya kwanza iliyompatia umaarufu Wednesday, June 10, 2009 6:59 AM
  Yule mwanamke-mwanaume wa Marekani ambaye alijipatia umaarufu mkubwa mwaka jana baada ya picha yake akiwa na mimba huku akiwa na midevu kusambaa duniani amerudi tena kwenye vichwa vya habari mwaka huu baada ya kujifungua mtoto wa pili. Thomas Beatie, au maarufu kama 'Mwanaume Mjamzito' amerudi tena kwenye vichwa vya habari vya magazeti baada kujifungua kwa mara ya pili mtoto wa kiume jana asubuhi.

  Picha za Thomas akiwa na madevu kibao huku akiwa na tumbo kubwa la ujauzito zilikuwa maarufu sana duniani mwaka jana kiasi cha kumfanya Thomas atajwe kama mwanaume wa kwanza kupata ujauzito.

  Thomas anaishi na mkewe Nancy ambaye ndiye atakayekuwa akimnyonyesha mtoto wao mpya kama alivyofanya kwa mtoto wao wa kwanza wa kike anayeitwa Susan Juliette aliyezaliwa mwezi juni mwaka jana.

  Thomas alizaliwa kama mwanamke lakini baadae alibadilisha jinsia kuwa mwanaume na kufanya upasuaji wa kuondoa matiti yake huku akitumia madawa ya homone za kiume yaliyomfanya awe na madevu kama mwanaume.

  Thomas hakufanya upasuaji wa kuondoa uke wake hali ambayo ilimwezesha kupata ujauzito wa mtoto wake wa kwanza baada ya kupandikizwa mbegu za kiume.

  Thomas ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 35 alisema kuwa aliamua kuzaa mtoto baada ya mke wake Nancy mwenye umri wa miaka 45 kutokuwa na uwezo wa kushika ujauzito.

  "Kuwa na mtoto hakuangalii kuwa wewe ni mwanamke au mwanamme, mimi pia ni binadamu na ninahitaji kuwa na mtoto" alisema Thomas.

  Thomas na Nancy bado hawajaamua wampe jina gani mtoto wao.
   
 2. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,187
  Likes Received: 681
  Trophy Points: 280
  Huyu ni mwanamke na atabakia kuwa mwanamke. Ukweli unapotoposhwa kwa kumwita mwanaume ili lionekane jambo la ajabu kwa mwanaume kupata jauzito ili hali alizaliwa na kukua kama mwanamke. Angeondoa uke na mfuko wa uzazi na kubandika pen*s labda angeweza kuwa mwanaume..!!,kitu ambacho naamini hakiwezekani!

  Kweli duniani kuna mambo! Kilichomrudisha nyuma na kubeba mimba/kuzaa ni nini wakati alikuwa keshaikana jinsia yake?!
   
 3. Nyaralego

  Nyaralego JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2009
  Joined: Nov 13, 2007
  Messages: 732
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  A totally preposterous claim...that she-man is still a woman. OMG...
  what a world we live in...
   
 4. M

  MTZ Halisi New Member

  #4
  Jun 12, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu wala sio mwanaume alizaliwa mwanamke ila baadae ndio aliamua kujibadilisha na kuwa mwanaume kwa hiyo sio kitu cha ajabu kabisa kama uliangalia 60 minutes alikuwa anahojiwa na Barbra Walters.

  Ndio Dunia jamani
   
 5. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2009
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ama kweli duniani kuna mambo!!!!!
  Mungu akisema leo ashuke, atapona kweli huyu?????? Si ataishia motoni tu!!!

  Wazazi wake wako wapi kumkanya na hii tabia ya kubadilisha jinsia????? Wazungu bwana kwa kupenda umaarufu kwa vitu vingine ambavyo havina mbele wala nyumba......
  Huko ni kumkufuru Mwenyezi Mungu tu..........
   
 6. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  WTF.. why do you even waste time discussing these sick sick people! He changes his sex to a man then takes D*C K.. I mean what kinda sick ish is that??
   
Loading...