Mwanaume Mjamzito' Kujifungua Mtoto wa Tatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanaume Mjamzito' Kujifungua Mtoto wa Tatu

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Nov 10, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280

  [​IMG]
  Thomas Beatie ambaye mwaka 2008 alikuwa gumzo duniani akitambulika kama mwanaume wa kwanza duniani kupata ujauzito anatarajiwa kujifungua mtoto wa tatu muda wowote kuanzia sasa.
  Mwanamke aliyebadilisha jinsia na kuwa mwanaume na kisha kutambulika kama mwanaume wa kwanza duniani kupata ujauzito, anatarajiwa kujifungua mtoto wa tatu.

  Thomas Beatie, alijifungua mtoto wake wa kwanza aliyepewa jina la Susan mwezi juni mwaka 2008 na mwaka mmoja baadae alijifungua mtoto mwingine aliyepewa jina la Austin.

  "Ameishatimiza muda wake wa kujifungua na ameipita siku aliyotarajiwa kujifungua", alisema mdau mmoja wa karibu na familia hiyo.

  Thomas alizaliwa kama mwanamke akijulikana kwa jina la Tracy lakini mwaka 2002 alianza kutumia madawa ya homoni kubadilisha jinsia yake kuwa mwanaume lakini hakufanya operesheni ya kuzibadilisha sehemu zake za siri.

  Umbile lake lilibadilika na kufanana na mwanaume huku akifuga madevu ili aonekane kama mwanaume kweli.

  Alibadilisha kisheria jinsia yake kuwa mwanaume na jina lake alilibadili kuwa Thomas badala ya Tracy.

  Mwaka 2003 alifunga ndoa na mwanamke aliyeitwa Nancy ambaye alikuwa ni mama wa watoto wawili aliyepewa talaka na mumewe.

  Baada ya kugundua kuwa Nancy hawezi kupata ujauzito tena kutokana na umri wake, Thomas aliamua kushika ujauzito kwa njia ya upandikizaji ili familia yake iweze kupata mtoto.

  Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Thomas kujulikana duniani kama mwanaume mjamzito. Alipata mtoto wa kwanza mwaka 2008 na sasa anatarajia kupata mtoto wa tatu.


  source nifahamishe
   
 2. F

  Ferds JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyo c mwanaume, kozi hana kifaa cha kufanya awe au aitwe mwanaume, homon za kiume hata Semanya anazo lakini bado anaitwa mwanamke, na ndiomaana akabeba mimba, acha azae
   
 3. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #3
  Nov 12, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  i agree wit u 110%
   
Loading...