Mwanaume mbembeleze mwanamke baada ya ugomvi, mtatuua kwa stress

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Kwenye mahusiano ya boyfriend na girlfriend au mahusiano yoyote yale lazima kunakuwepo na kuhitilafiana kwa hapa na pale

Linapokuja suala la kugombana ya wawili hao kinachofuata ni kusuluhishana mambo yaishe mapenzi yaendelee

Kunapotokea ugomvi wa kimahusiano sio siri sisi wanawake huwa tunaumia sana,na huwa tunapenda mahusiano yazidi kuwepo hasa kama uliyenaye ni yule wa moyo wako

Katika hali hiyo tunategemea mwanaume amuonyeshe mpenzi wake pamoja na kugombana bado anampenda na anampenda sana

Hapa tunamtegemea mwanaume baada ya kugombana,baada ya SAA moja mwanaume atakuwa na jukumu la kuweka mahusiano sawa,kwa kumtumia text za hapa na pale,za kumbembeleza mwanamke hata kama mwanamke ndo alikuwa na makosa,haijalishi nani kaanzisha ugomvi ila mwanaume ana jukumu kubwa la kuweka mahusiano sawa

Kwa sasa hali imebadilika sana kwa hawa wanaume,mnagombana,mnamaliza hata siku mbili hakutumii text,wala kukupigia sim,na kama mwanamke ataendelea kupiga kimya,kinachofuata ni mwanaume kuanza kuweka picha kwenye mitandao ya kijamii ambazo hazieleweki,mara aweke za mwanamke fulani,mara aweke za wanawake na status kibao,au akae online muda mrefu ambapo si kawaida yake

Unabaki unajiuliza ina maana mahusiano yameisha,mbona sielewi,mapicha picha ya nini tena

Ukweli ndo huu,tunapogombana na ukamaliza masaa 2 bila kutuma sms au kupiga sim hata kuulizia kitu fulani,yaani huwa tunaumia sana

Na kama tangu ugomvi yamepita masaa 5 hujatuma sms, huwa tunahisi kuchanganyikiwa,sms inaingia unadhani ni baby kumbe za watu wengine au mitandao maumivu huwa yanatuzidi

Nyie wanaume acheni kuwatesa wawapendao,hamjui tu tunavyoumia

Ndo maana muda mwingine unasema bora usiwe kwenye mahusiano

Tubembelezeni basi baada ya ugomvi,hata kama sisi ndo wakosaji au hata kama ni nyie wakosaji
 
huo uanaume wa darisalam nishaukataa.

wife akininunia au akanipa story za ajabuajabu huwa nanyamaza tu na sibishani nae. nikimuongelesha Mara tatu hajibu huwa natoka nyumbani naenda kitaa nalala huko, naunga hadi kazini.

nikirudi nyumbani saa9 hakuna msosi na haniongeleshi narudi tena, na kibegi changu cha nguo za kubadili hadi kesho yake tena. kuna kipindi nilifanya hivyo wiki nzima.

akiniongelesha tu ndo namvutia chumbani tunaweka heshima na kumdanganya danganya.

kwa nini nafanya vile?

nilipomuoa 2007 alikuwa kila mwezi ananyamaza kwa siku, nikawaza kulikoni hadi nikahisi ana tatizo la akili... kumbe analenga mshahara utoke nimkabidhi. maringo yalikuwa tar 27, siku ya mshahara tunaenda nae wilayani na phoenix yetu tumebebana.

ulipoisha mwaka nikamzoea nikaanza kuwa mwanaume na uvulana ukaisha. kipindi kile hata shamba sikutaka alime, lakini now anashinda shamba.

narudia, siwezi kubembeleza... hata mwaka unaisha.
 
Umkabidhi mshahara aupeleke wapi?
 
ME = Mtafutaji riziki, Mtoa matumizi, Mtongozaji, Mchumbiaji, Muoaji, Kichwa cha familia, Muamuzi mkuu/wa mwisho ktk mapenzi/ndoa.

KE = Mpokeaji matumizi, Mlezi wa watoto, Mshauri, msimamizi wa majukumu kifamilia/nyumbani.

Bado tena KE mkikosea ME tuwabembeleze hata kama ninyi ndiyo vyanzo vya migogoro pa1 na majukumu yote hayo tuliyonayo?

ACHENI UJINGA BASI AYSEEE...

"Don't be so much complicated coz life is not sufficiently longer to handle all of that responsibilities to your Boyfriends or Husbands"
 
Ila kwa kawaida tunategemea mwanaume ndo ambembeleze mwanamke baada ya ugomvi,na sio kujishusha
Hahah inategemea na kosa na kiwango cha thamani yako kwangu kilichobakia moyoni. Maana kero huwa zinashusha thamani ya upendo hasa zikiwa mara kwa mara.

Pia kuna wasichana ambao yeye anapenda attention sana ila hana mbinu za kiintelijensia za kuipata toka kwa mpenziwe, anachoona rahisi ni kuanzisha ligi ili mbishane tu mwishowe unamchoka sasa. Hii ni kwa wenye vile vi age vya 21-25! Kuna mmoja kala Red Card kwa sababu hio, mie sipendagi kelele af nashikwaga na hasira sana ila analazimisha msuguano ili tu asikie naongea tu hata kwa ubishani usio na maana...Really turns me off na sitakaa nikubembeleze kwa vitu vya namna hio.

Kanuni niliojiwekea, tukigombana nikachukia nikilala nikaamka nakuwa fresh kama kitu kibaya hakijatokea last night. Huwa si hold ugomvi au hasira, new day i'm refreshed na nashukuru mungu bibie amesha adopt hilo.

Hayo mambo ya kununiana week nzima au miezi naona ni utoto tu.
 
Back
Top Bottom