Mwanaume mbahili kwa mpenzi wake anamaanisha hivi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,438
Ice-Cream-Date-1024x683.jpg



KATIKA ulimwengu wa sasa, wapenzi wapo wa aina tofauti. Kuna wale ambao mwanamke anafanya kazi mwanaume hana kazi, mwanaume ana kazi na mwanamke hana kazi ama wote wanafanya kazi.

Katika mazingira hayo, fahamu kwamba mpenzi wako ana haki ya kuitumia pesa ya jasho lako. Hutakiwi kuwa na ‘mkono wa birika’ hata kidogo na unachotakiwa kufanya ni kumpatiliza katika mahitaji yake muhimu pale atakapohitaji msaada kutoka kwako.

Hapa sizungumzii kwamba mwanaume ndiye anayetakiwa kumfanyia hayo mpenzi wake bali hata mwanamke pia anatakiwa kumfanyia mambo fulani mpenzi wake kwa kutumia kipato chake. Kuna baadhi ya wanawake wao siku zote ni tegemezi tu kwa wapenzi wao licha ya kwamba wao pia wanafanya kazi. Si wanawake tu bali pia kuna hata wanaume ambao ubahiri wao umezidi. Unamkuta mwanaume anafanya kazi na anapata mshahara mzuri tu lakini mpenzi wake anaishi maisha magumu sana.

Ni kweli mapenzi na pesa ni vitu viwili tofauti lakini mpenzi wako akikulilia shida kama unao uwezo msaidie, hivi unadhani kama usipomsaidia wewe nani amsaidie. Pia usisubiri tu mpaka mpenzi wako awe na shida. Ukiona katika fedha zako kuna hela ya ziada waweza kuamua siku moja ukamnunulia zawadi, mkatoka ‘out’ mkatumia, hayo ndio mapenzi. Hivi unadhani mpenzi wako asipokifaidi kipato chako, nani akifaidi?

Ila unaweza kuwa na mpenzi ambaye kila wikiendi anakutoa OUT, anakupatiliza katika kile unachotaka lakini akawa hana mapenzi ya dhati licha ya kwamba katika mazingira hayo kidogo kunakuwa na matumaini ya kuwepo kwa penzi.

Achilia mbali wale walio katika uhusiano wa kawaida, hata wale waliooana wanaweza kusadiana katika kuchangia matumizi ya ndani ya familia kutokana na kila mtu kuwa na kipato. Maisha ya sasa ni kusaidiana na si kutegemeana, labda ziwepo sababu za msingi za mume kutegemea kipato cha mke ama mke kutegemea kipato cha mume.

Lakini tuna kila sababu ya kukaa chini na kujiuliza, kwa nini baadhi ya watu wanakuwa wabahiri kupindukia kwa wapenzi wao? Kweli mpenzi wako anakutembelea kisha unashindwa hata kumnunulia juisi? Anaondoka unashindwa hata kumpa nauli, inakuja kweli? Sawa! Tunajua kuna ulazima wa kuwa makini katika kila shilingi unayoipata, lakini umakini huo usizidi kipimo mpaka ufikie hatua hatua hiyo.

Nasema hivyo kwa sababu, kila utakachokuwa unamfanyia mpenzi wako kinadhihirisha mapenzi ya dhati uliyonayo kwake, pia unaonesha kumjali. Sisemi kwamba ni lazima umpe mpenzi wako pesa ama kitu flani kuonesha kwamba unampenda lakini kufanya hivyo kunaongeza chachu ya penzi lenu.


JU-1.jpg



Hilo ni kwa wale wenye uwezo kidogo kifedha ila kwa kwa wale wenzangu na mimi wasio na uwezo, hawatakiwi kujali wala kujiona kwamba labda kutowapa wapenzi wao fedha ama kuwanunulia zawadi wataonekana hawawapendi. Kumbuka mapenzi ya dhati ni yale yanayotoka moyoni.

Katika hili pia niwatahadharishe tu kwamba, unapomuona mwanaume ama mwanamke ni mwepesi sana wa kukupa pesa hata pale ambapo huzihitaji, penzi lake kwako litakuwa na walakini. Yawezekana anataka kununua penzi kutoka kwako wakati penzi hata siku moja halinunuliwi.

Ila sasa mpenzi wako anapokuwa na uwezo kifedha, kisha akawa mgumu sana kukusaidia pale unapokuwa na matatizo huyo hakupendi na kama anakupenda basi atahakikisha kwamba na wewe unakifaidi kipato chake.

Kwa kuhitimisha niseme tu kwamba, mapenzi ni baina ya wewe na mpenzi wako. Mapenzi ni kusaidiana, mapenzi pia ni kupeana raha. Mnapojaaliwa kuwa na uwezo kidogo, zitumieni fedha zenu katika kufanya mambo yatakayoyaboresha maisha yenu.
 
Back
Top Bottom